PreGE2025 Ujenzi wa Shule Mpya 35 za Msingi na 148 za Sekondari Umefanyika Katika Maeneo Yasiyopimwa

PreGE2025 Ujenzi wa Shule Mpya 35 za Msingi na 148 za Sekondari Umefanyika Katika Maeneo Yasiyopimwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
OR-TAMISEMI imekuwa ikitekeleza mradi wa BOOST ili kuimarisha upatikanaji sawa wa elimu bora katika shule za awali na msingi kote Tanzania Bara. OR- TAMISEMI inatekeleza pia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa elimu ya sekondari, kuweka mazingira wezeshi ya kujifunzia kwa wasichana, na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari kwa wasichana na wavulana. Miradi hii imekuwa ikifadhili ujenzi wa shule mpya za sekondari na msingi sehemu mbalimbali nchini.

Ili kuhakikisha uendelevu wa miradi hii, Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI kupitia barua yenye Kumb. Na. DB.291/297/04/51 ya tarehe 22 Machi 2023, aliagiza mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha shule hizo zinajengwa katika maeneo yaliyopimwa na hati miliki za viwanja husika zinapatikana ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya agizo.

Mapitio ya nyaraka na ziara za ukaguzi wa miradi zilibaini kuwa shule mpya 35 za msingi zenye thamani ya Shilingi 15,819,500,000 na shule mpya 148 za sekondari zenye thamani ya Shilingi 109,327,133,843 zilijengwa katika maeneo ambayo hayakupimwa, kinyume na maelekezo.

Ufuatiliaji hafifu wa maafisa masuuli katika kupata maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ulisababisha hali hii, hivyo kuziweka shule hizo katika hatari ya migogoro ya ardhi kama vile migogoro ya umiliki na mipaka.

Ninapendekeza menejimenti za Mamlaka za Serikali za Mitaa ziharakishe ufuatiliaji ili maeneo yaliyojengwa shule hizo yapimwe na hati miliki zipatikane bila kuchelewa zaidi
 
Back
Top Bottom