Ujenzi wa lenta kwa nondo 3 unafaa?

IMG_1991.jpg

IMG_1762.jpg

IMG_1763.jpg

IMG_1764.jpg

C
IMG_0006.jpg

A
IMG_1937.jpg
IMG_1938.jpg
IMG_1939.jpg

Call/whatsapp +255718892233 njoo kwa design kali za nyumba kulingana na matakwa yako
 
Attachments

  • 08282101-9eb4-4bf1-8f55-668cf4fe2397.jpg
    08282101-9eb4-4bf1-8f55-668cf4fe2397.jpg
    232.3 KB · Views: 26
swali,je nondo ulizifunga kwa bangili?
Ndiyo zilifungwa na bangili na binding wire,pia nyumba ilikuwa na nguzo permanently zimetoka chini kabisa kwenye zege la mwanzo kabla hazijalazwa tofalo.

Mkuu,naposema nyumba ipo strong namaanisha kweli ipo strong labda idea uliyoitoa hapo juu kuna maeneo inatumika but kwa mazingira nilipofanya ujenzi wangu nondo ndo zilikuwa sahihi.
 
Wewe ni muhandisi uliesoma na kuelewa.

Ukipitia huu uzi vizuri utawakamata wahandisi uchwara waliokariri uhandisi wa vitini vya chuoni na google.

Bado tuna tatizo la wahandisi wenye weledi nchini, wengi ni degree za makaratasi na kukariri kwingi, hawawezi kuelezea mantiki ya walichosomea.
watu wengi mara nyingi wamekuwa wakichanganya lenta(lintel) na ring beam...lenta ni kipande kifupi tu kinachofungwa kwenye uwazi(openings) kama milango na madirisha, ring beam ni ile unafungu kuzunguka nyumba kwa kuzifuata kuta zote za nje na za ndani wengine huchagua kuta zinazobeba mzigo tu(load bearing walls).

turudi kwenye mada, ufungaji wa nondo kwa level ya juu pia hutegemea sana uzito utakaobebwa kutoka juu, tu-assume mzigo ni course chache tu za tofali na paa la kawaida la mbao na bati na kama mleta maada alimaanisha lenta kwa definition niliyotoa hapo juu pamoja na ukweli kwamba standards nyingi zinataka nondo nne lkn nondo tatu za 12mm kwa sura ya mzigo niliyoelezea hapo juu zinatosha kabisa lkn zifungwe pamoja na nondo au waya angalau wa 6mm, 8mm zinaweza tumika pia.

kama mleta maada lenta alimaanisha ring beam (kama wengi wanavyoichanganya lenta na ring beam) nondo tatu kwangu ni uharibifu wa hela (is a wastage of resources), nondo mbili za 12mm is more than enough.

kumbuka zege liwe la angalau lenye mchanganyo wa ratio ya 1:2:4 cement:mchanga:kokoto...hii kwa makadirio inakupa zege lenye nguvu ya 20Mpa au grade 20 au class 20 though itategemea na ubora wa mchanga na kokoto
 
So

Mkuu kwahiyo ushauri wako ni kwamba nondo mbili za 12mm zinaweza kutumika kwenye ring beam badala ya nondo tatu?
 
Habari wakuu,katika kubana matumizi fundi kaniambia ujenzi wa lenta kwa kusuka nondo 3 unafaa,naomba ushauri wananzengo
Kama ni banda la mbuzi ama kuku 3 sawa, ila kama unatarajia kulala wewe na watoto wako fuata kanuni za ujenzi, weka nondo 4
 
Kitaalamu haufai kabisa.

Kwa sababu hiyo lenta(linta) ndiyo inapokea mzigo kutoka juu na kuleta msawazo wa jengo lako. Kwa sababu linta inapokea mzigo inatakiwa iipokee kwa usawa.

Kwanza kazi ya nondo ni nini kwenye linta??

Kazi ya nondo kwenye linta ni kuzuia kani(force) za mvutano ndani ya jengo lako!

Kwa nini sasa nondo tatu hazifai??
Ni kwa sababu standards zinashauri nondo lazima zifungwe symmetrically arranged. Ili zinapopokea mzigo na kuusambaza uwe sawa sawa.

Nondo tatu siyo symmetrically arranged. Sasa mzigo ukizidi kudogo tuu, jengo unaanza kuliona limeeanza nyufa na hata hiyo linta unaanza kuiona inapinda.

Suluhisho!

Ongeza nondo nyingine ziwe nne ili angalau ulete msawazo wa upokeaji wa mzigo na usambazaji wake.

Pia weka na nguzo kwenye kila kina na maungio ya jengo lako (kama ni nyumba kubwa na unataka idumu muda mrefu).

Ila kama ni banda tuu, komaa na aina ya ujenzi wako. Ila kama ni dream house, fuata hako kaushauri.
Tatizo la madaftari hili kuna watu hawaweki kabisa lenta, kinapigwa ki slab flan uchwara kwenye madirishà na milango Tu na nyumba zina miaka Zaid ya 30 na bado zipo vizuri kabisa. Madaftari na uhalisia tofauti kabisa
 
Mbeya niliwahi kuona nyumba nyingi za makazi ya watu hazina lenta(nondo) na tofali zake ni mbichi, hawachomi. Wanakuambia ukizichoma ndo unaharibu ubora na nyumba zao ni imara kuliko za blocks. Hata fensi zao hazina lenta na hazianguki.
 
Mondo moja= 22000 sasa mkuu kwa nini kama uwezo huna usisubiri kidogo? Kwa nini ufanye kitu chini ya kiwango ukijua baadae kitaleta majanga?

Usinunuwe vifaa vyote kama uwezo huna.
Mwambie fundi akupe idadi ya vifaa andika kwenye karatasi.mf. Mwezi huu nunua nondo tu 15 ×22000 zinatosha.
Mwezi ujao nunua mabati etccccc

Bora ufanye kitu kidogo ila quality hata kama ukichelewa kumaliza.

Vifaa vya ujenzi vina gharama inategemea nyumba unayotaka kujenga.
Juzi kuna mtu mwenyewe mipesa yake aliniomba nitafutie fundi professional nimpeleke site anihesabie gharama na vifaa nimtumie budget, ahaa kwa nyumba anayoitaka msingi tu ni mil 21 vifaa sasa tukaenda dukani nikauliza bei ndo nilijua kujenga sio mchezo.
Msingi mil 21
 
Ila keshokutwa yaweza kuanguka?
Hata keshokutwa haianguki pia.
Tatizo unaangalia sana rinta kuliko msingi.

Zamani miaka ya '70 na '80, enzi vifaa vya ujenzi vilikuwa adimu kupatikana ama kutopatikana kabisa, watu walijenga nyumba za block na rinta ikawekwa kwenye vizingiti vya madirisha na milango tu na nyumba hizo mpaka leo zipo zinadunda bila ya tatizo lolote kama msingi wake ulitoshelezwa kwa racial za material.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom