Ujenzi wa lenta kwa nondo 3 unafaa?

Ujenzi ukifatisha ushauri mwingi hujengi utaona gharama, We jenga Tu as long as fundi anaekushauri ashajenga nyumba kadhaa unazoziona zimedumu kuanzia 10yrs kuendelea.

asije tu kuwa fundi wa kufanya majaribio kwenye nyumba yako. ila kama n mzoefu anajua anachoshauri unajenga tu..
 
Kitaalamu haufai kabisa.

Kwa sababu hiyo lenta(linta) ndiyo inapokea mzigo kutoka juu na kuleta msawazo wa jengo lako. Kwa sababu linta inapokea mzigo inatakiwa iipokee kwa usawa.

Kwanza kazi ya nondo ni nini kwenye linta??

Kazi ya nondo kwenye linta ni kuzuia kani(force) za mvutano ndani ya jengo lako!

Kwa nini sasa nondo tatu hazifai??
Ni kwa sababu standards zinashauri nondo lazima zifungwe symmetrically arranged. Ili zinapopokea mzigo na kuusambaza uwe sawa sawa.

Nondo tatu siyo symmetrically arranged. Sasa mzigo ukizidi kudogo tuu, jengo unaanza kuliona limeeanza nyufa na hata hiyo linta unaanza kuiona inapinda.

Suluhisho!

Ongeza nondo nyingine ziwe nne ili angalau ulete msawazo wa upokeaji wa mzigo na usambazaji wake.

Pia weka na nguzo kwenye kila kina na maungio ya jengo lako (kama ni nyumba kubwa na unataka idumu muda mrefu).

Ila kama ni banda tuu, komaa na aina ya ujenzi wako. Ila kama ni dream house, fuata hako kaushauri.
Safi injinia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom