watu wengi mara nyingi wamekuwa wakichanganya lenta(lintel) na ring beam...lenta ni kipande kifupi tu kinachofungwa kwenye uwazi(openings) kama milango na madirisha, ring beam ni ile unafungu kuzunguka nyumba kwa kuzifuata kuta zote za nje na za ndani wengine huchagua kuta zinazobeba mzigo tu(load bearing walls).
turudi kwenye mada, ufungaji wa nondo kwa level ya juu pia hutegemea sana uzito utakaobebwa kutoka juu, tu-assume mzigo ni course chache tu za tofali na paa la kawaida la mbao na bati na kama mleta maada alimaanisha lenta kwa definition niliyotoa hapo juu pamoja na ukweli kwamba standards nyingi zinataka nondo nne lkn nondo tatu za 12mm kwa sura ya mzigo niliyoelezea hapo juu zinatosha kabisa lkn zifungwe pamoja na nondo au waya angalau wa 6mm, 8mm zinaweza tumika pia.
kama mleta maada lenta alimaanisha ring beam (kama wengi wanavyoichanganya lenta na ring beam) nondo tatu kwangu ni uharibifu wa hela (is a wastage of resources), nondo mbili za 12mm is more than enough.
kumbuka zege liwe la angalau lenye mchanganyo wa ratio ya 1:2:4 cement:mchanga:kokoto...hii kwa makadirio inakupa zege lenye nguvu ya 20Mpa au grade 20 au class 20 though itategemea na ubora wa mchanga na kokoto