Ujenzi wa lenta kwa nondo 3 unafaa?

Chrisvern

Chrisvern

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Messages
1,901
Points
2,000
Chrisvern

Chrisvern

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2011
1,901 2,000
Mkuu nondo katika ujenzi wa nyumba za kawaida ni fito kwa lugha nyingine.

Kama fundi kanyoosha msingi na ukuta ukapanda bila kupinda, nondo 2 za mm12 zinatosha.
Sidhani kama watakuelewa mkuu.
 
severinembena

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Messages
1,993
Points
2,000
severinembena

severinembena

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2018
1,993 2,000
Hivi sehemu iliyo tambarare kati ya kuweka msingi Wa mawe na Matofali upi bora? Na upi unaokoa gharama?
 
ChoiceVariable

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
3,003
Points
2,000
ChoiceVariable

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
3,003 2,000
Huo ni umaskini na kutojua kazi za nondo afu mafundi wenu hawaelewi chochote zaidi ya kukulahisishia ili usije kosa hela ya kumlipa,kama nondo tu zimezua ishu hizo stirrups itakuwaje,fundi ukimwambia stirrups zinafaida gani hajui utasikia kufungia nondo😂😂😂😂
 
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Messages
10,414
Points
2,000
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2014
10,414 2,000
Mondo moja= 22000 sasa mkuu kwa nini kama uwezo huna usisubiri kidogo? Kwa nini ufanye kitu chini ya kiwango ukijua baadae kitaleta majanga?

Usinunuwe vifaa vyote kama uwezo huna.
Mwambie fundi akupe idadi ya vifaa andika kwenye karatasi.mf. Mwezi huu nunua nondo tu 15 ×22000 zinatosha.
Mwezi ujao nunua mabati etccccc

Bora ufanye kitu kidogo ila quality hata kama ukichelewa kumaliza.

Vifaa vya ujenzi vina gharama inategemea nyumba unayotaka kujenga.
Juzi kuna mtu mwenyewe mipesa yake aliniomba nitafutie fundi professional nimpeleke site anihesabie gharama na vifaa nimtumie budget, ahaa kwa nyumba anayoitaka msingi tu ni mil 21 vifaa sasa tukaenda dukani nikauliza bei ndo nilijua kujenga sio mchezo.
 
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Messages
1,696
Points
2,000
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2014
1,696 2,000
Mm nilijenga yangu huku kijijin kwa hizo 3 nimezalia huko watoto wangu 2 na mpaka sasa ninaishi humu humu asubuh kwichi kwichi si za kitoto

Jenga tu mkuu 3 ni standard kabisa
 
Eli79

Eli79

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
22,930
Points
2,000
Eli79

Eli79

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2013
22,930 2,000
Unaweza kutumia nondo nne(kama standards zinavyosema) lakini ukawa umevurunda sehemu nyingine za nyumba hivyo weakness ikawepo sehemu nyingine.

Labda tuulize chini/foundation umeijenga vipi(kwa standards zipi), je uliweka beams/nguzo kwenye pembe za nyumba? Ulitumia matofali yenye viwango vya juu/kati/chini?(kumbuka siku hizi tunauziwa tofali za ajabu sana).

Tukumbuke kuwa nyumba ni kama mwili wa binadamu tu, kila sehemu inategemea mwenzake.

Kama ulijenga chini vizuri, nyumba haijapinda, then hizo nondo tatu zinaweza kustahamili force kitoka juu .
 
J

J.wawatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Messages
235
Points
500
J

J.wawatu

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2013
235 500
Kitaalamu haufai kabisa.

Kwa sababu hiyo lenta(linta) ndiyo inapokea mzigo kutoka juu na kuleta msawazo wa jengo lako. Kwa sababu linta inapokea mzigo inatakiwa iipokee kwa usawa.

Kwanza kazi ya nondo ni nini kwenye linta??

Kazi ya nondo kwenye linta ni kuzuia kani(force) za mvutano ndani ya jengo lako!

Kwa nini sasa nondo tatu hazifai??
Ni kwa sababu standards zinashauri nondo lazima zifungwe symmetrically arranged. Ili zinapopokea mzigo na kuusambaza uwe sawa sawa.

Nondo tatu siyo symmetrically arranged. Sasa mzigo ukizidi kudogo tuu, jengo unaanza kuliona limeeanza nyufa na hata hiyo linta unaanza kuiona inapinda.

Suluhisho!

Ongeza nondo nyingine ziwe nne ili angalau ulete msawazo wa upokeaji wa mzigo na usambazaji wake.

Pia weka na nguzo kwenye kila kina na maungio ya jengo lako (kama ni nyumba kubwa na unataka idumu muda mrefu).

Ila kama ni banda tuu, komaa na aina ya ujenzi wako. Ila kama ni dream house, fuata hako kaushauri.
Acha ubabaishaji hapa, mondo Tatu zinafaa kabisa ili mradi nyumba iwe imefungwa mkanda kwenye msingi!
 
deonova

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Messages
730
Points
250
deonova

deonova

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2013
730 250
Nondo 3 zinafaa kabisa, lakini ziwe za mm 12, asije kukushauri uweke mm 10 hazitafaa. Hizo za mm 12 azisuke katika umbo la pembe 3 (yaani mbili chini kwenye base ya linter na moja juu, yaani ikae umbo la pyramid) lengo hapa ni kupata balance), fundi anaweza akazisuka na binding wire au anaweza asisuke pia; inategemea na ustadi wake katika kuzipanga inavyotakiwa. Mimi nimejenga nyumba yangu kubwa tu ya room 3, sebule kubwa tu, dining, jiko na store; na linter yake nimetumia nondo 3 za mm 12, juu ya linter nimeweka tofali za course 3, so naelezea kitu nnachokifahamu.
 
MC44

MC44

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Messages
515
Points
1,000
MC44

MC44

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2019
515 1,000
Sisi tunafungia NONDO 1 hata 10mm inatosha na nyumba inakaa huoni ufa
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
8,432
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
8,432 2,000
Mbili zinakaa fresh tu acha ubishi.

Kikanuni kabisa inatakiwa 4.
Ila kiuchumi ndio mtu inabidi ubane tu matumizi.
Tatu afadhari sasa mbili zinawekaje Ballance ya kubeba mzigo?
 
deonova

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Messages
730
Points
250
deonova

deonova

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2013
730 250
Tunaweka zile zenye upele upele ...sementi kali
Ndio si ndo zile makonde? na ndo zinazofaa kwa linter

Ambazo sio makonde (zisizo na upele) hazifai kwa linter
 

Forum statistics

Threads 1,316,064
Members 505,493
Posts 31,877,568
Top