Ujenzi wa Bomba la Mafuta la Uganda.Watanzania tuchangamkie fursa badala ya kulalamikia Serikali.

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Habari Wakuu.

Kwa mujibu wa EWURA wanaoratibu kampuni zitakazoshirikishwa kwenye ujenzi wa Bomba la Mafuta la Uganda kutoka Hoima hadi Tanga,wameinesha kusikitishwa na muamko mdogo wa kampuni za Kitanzania zilijitokeza kusajiliwa.

Licha ya usajili kuwa bure na elimu kutolewa lakini ni makampuni 200 plus tuu ya Kitanzania yamejitokeza dhidi ya makampuni zaidi ya 2,000 kutoka Uganda.

EWURA ndio imepewa mamlaka kisheria kuratibu hili zoezi.

Ikiwa ujenzi umeanza na robo tatu ya ujenzi utafanyika Tanzania lakini ndio hivyo tena WaTzn tunasubilia kuja kulalamika,kulaumu na kutukana Serikali.

Sijui nani alituroga au ndio hatuna uelewa wa haya mambo au?

Msije kusema hamkuambiwa.Soma hapo chini 👇

Screenshot_20210908-071546.png

Screenshot_20210908-071634.png
 
Kwa akili yako unafikili Holo bomba ndiyo la Kwanza kuwa nalo?
Bomba la mafuta TAZAMA limepita mikoa mingapi na wilaya ngapi? je maisha ya wananchi wa huko yamebadilika.
 
Kwa akili yako unafikili Holo bomba ndiyo la Kwanza kuwa nalo?
Bomba la mafuta TAZAMA limepita mikoa mingapi na wilaya ngapi? je maisha ya wananchi wa huko yamebadilika.
Umekurupuka,kakojoe afu urudi kusoma upya ndio uchangie kima wewe.
 
Kwa akili yako unafikili Holo bomba ndiyo la Kwanza kuwa nalo?
Bomba la mafuta TAZAMA limepita mikoa mingapi na wilaya ngapi? je maisha ya wananchi wa huko yamebadilika.
Anaongelea kipindi hichi cha mchakato wa ujenzi Mkuu sio kipindi baada ya ujenzi.
 
Back
Top Bottom