Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi 2023

Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo katika mwaka ujao wa fedha. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa alibainisha jana kuwa hawatalazimika kusubiri zaidi wawekezaji
Safi wamesikiliza mawazo yetu ya Serikali kuanza ujenzi bila kusubiria wanaoitwa Wawekezaji..

Ushauri hizo industrial parks ziwekewe miundombinu yote kama kule kwala investors watakuia wenyewe bila masharti ya ajabu ajabu..

Hope by 2030 itakuwa imekamilika .
 
Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo katika mwaka ujao wa fedha. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa alibainisha jana kuwa hawatalazimika kusubiri zaidi wawekezaji kuanza ujenzi wa bandari hiyo.
Hawezi kusubiri?...ana hela? Huyu Mbossa vipi hapa tulipo miradi kibao haiendi...anataka kuiba sio....hii nchi ina watu wa ajabu sana..
Anataka kutuambia hizi zilizopo zimezidiwa sio...
Nchi imebanwa kila kona aisee maombi ni muhimu ..
Na ukiona kitu kinakazaniwa hivi lazima ni dili...
 
Mie nadhani zingelekebishwa hizo bandali3 zilizopo Tanga, Dar, Mtwara zingetosha kabisa wazipanue na kujenda njia za leli zinazotoka kwenye hizo bandali kwenda nje ya nchi nadhani itapendeza zaidi kuliko hiyo inayotaka Kuanzisha, #UPIGAJI TU#
 
Hapo cha kuangalia sana sana kwa vijana ni ajira kuhusu hayo mambo mengine ya kisiasa sio muhimu sana.. Kwasababu watu wenye professional ya bandarini wengi wao wanaishia kuwa mtaani tu
 
Miradi inayojengwa na serikali mingi bado haijakamilika mfano SGR, Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, Ujenzi wa Meli mpya ziwa Victoria, Daraja la Kigongo-Busisi. Serikali ikamilishe kwanza hii miradi ndio ianze ujenzi wa mradi Bandari ya Bagamoyo sababu unatumia pesa nyingi kukamilika kwake.
 
Upotevu wa pesa za bure kuwafurahisha wakina kikwete. Bandari ya Tanga ambayo tayari kuna mafuta ya uganda yanakuja tusijenge pale tutumie pesa kujenga bandari ya pili Dar. Hii ni miradi binafsi
Kweli kabisa ingawa bagamoyo ni pwani lakini tanga inapigwa vita sana,kama vipi tungewauzia tu Kenya
 
Bandari ya Bagamoyo ni sawa, ila SGR itasevu pakubwa katika kuongeza ufanisi wa bandari yetu ya Dar es salaam kwa kuongeza Kasi ya kupakua na kusafirisha mizigo kwa haraka. Hivyo tungesubiri impact ya SGR na ambayo ingetusaidia kujenga bandari hiyo ya Bagamoyo pasipo maumivu kwa wananchi.
 
Huu utapeli wa kijinga, hatuna uwezo wa kujenga bandari itakayogharimu $10b, reli na bwawa lenyewe ni mwendo wa kinyonga, ndio itakuwa bandari ya $10b? Sana sana waseme watasafisha eneo linalotarajiwa bandari kujengwa.
Hapa lazima mchina anakuwa behind the scene, maana huu mradi unalazimishwa na kufosiwa lazima kuna makando kando.
 
Hivi ukiulizwa sababu hasa inayofanya bandari za Tanga, Dar na Mtwara zionekane haifai ila suluhisho ni kuanza kujenga mpya unajua?
Kwani kuna sehemu wamesema bandari za Dar Tanga na Mtwara hazifai?

Don't get the facts twisted.

Zingekua hazifai serikali isingeziboresha.
 
Hapa ni kila mzalendo aombe kwa Mungu wake walahi
Huu mradi ni mkubwa sana sana na kwa kweli hatuuitaji kabisa
Ehh Mwenye Enzi Mungu tunakuomba usitutupe wanao wa Tanzania jamani!
Tuonee huruma nakila tunapo kuita uitikie na utende ehhh Mwenye Enzi Mungu uwiii
 
Upotevu wa pesa za bure kuwafurahisha wakina kikwete. Bandari ya Tanga ambayo tayari kuna mafuta ya uganda yanakuja tusijenge pale tutumie pesa kujenga bandari ya pili Dar. Hii ni miradi binafsi

Umeona ehh!
Ehh Mungu jionyeshe utukufu wako kwa hawa watu wakuogope jamani
 
Back
Top Bottom