Ujenzi Ubungo interchange wafikia 25%

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
1062434


WAKALA wa Barabara nchini (Tanroads) umesema ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange), umefanyika kwa asilimia 25 mpaka sasa na umeanza kudhihirisha ukimalizika, utamaliza tatizo la msongamano wa magari huku ukijenga taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, pamoja na hatua hiyo, kumefanyika mabadiliko ya ujenzi wa barabara hizo kutoka mchoro wa kwanza, baada ya kufanyika mapitio ya usanifu wa kina uliowezesha kuwa na mabadiliko hayo. Taarifa ya Tanroads kwa gazeti hili, ilieleza kuwa kasi ya ujenzi wa barabara hizo za juu zinazojengwa katika makutano ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela, ni nzuri na mabadiliko hayo ni madogo.

Mradi huo unaojengwa na mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya China, China Engineering Construction Co-operation (CCECC), unatarajia kutumia miezi 30 mpaka kukamilika huku ajira kwa Watanzania zikiwa asilimia 90 na wageni asilimia 10 kwa takwimu za Februari mwaka huu. Awali, mchoro uliozinduliwa na Rais Magufuli ulionesha kuwa barabara itakayoruhusu magari kupishana (Mwenge-Mbezi, Mbezi-Buguruni, Buguruni- Mjini, Mjini-Mwenge) ni ngazi ya katikati na ngazi ya juu ni ya magari ya moja kwa moja kutoka Mwenge kwenda Buguruni huku barabara ya chini ikihusisha mabasi ya mwendo kasi na magari yanayoenda moja kwa moja mjini.

Hata hivyo, kumekuwa na mchoro mwingine unaoonesha magari yatapishana katika barabara ya chini inayotumika na mabasi ya mwendo kasi na ngazi ya kwanza itahusisha magari yanayoenda mjini moja kwa moja na ngazi ya juu ni ya magari yanayotoka Mwenge kwenda Buguruni moja kwa moja. Kwa mujibu wa majibu ya Tanroads kwa gazeti hili yaliyotolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Chrispianus Ako, mchoro wa awali ambao magari yanapishana katikati .

Mchoro unaoonekana kwenye mitandao ya kijamii unahusisha usanifu wa awali, baada ya mapitio ya usanifu huo kwa kina, mchoro huo umebadilika kidogo ingawaje umebaki na ngazi tatu kama ule wa awali,” ilieleza taarifa ya Tanroads kwa gazeti hili. Ako katika taarifa hiyo alisema kuwa, awali kulikuwa na changamoto ya kuhamisha miundombinu ya gesi kilometa 1.2, mabomba ya maji sa kilometa 2.6, mawasiliano kilometa 2.6 na umeme kilometa 17 iliyokuwa chini ya ardhi ambayo sasa imekamilika.

“Kwa sasa hakuna changamoto ambayo itaathiri mradi usikamilike kwa wakati,” ilieleza sehemu ya majibu ya Tanroads kwa maswali ya mwandishi wa habari hii. Kuhusu Watanzania waliopata ajira katika mradi huo, Ako alisema ajira za moja kwa moja na za muda lakini idadi inatofautiana mwezi hadi mwezi kulingana na kazi zilizopo.

“Idadi ya wafanyakazi kwa mwezi wa pili mwaka huu ilikuwa jumla 754, Watanzania walikuwa 679 sawa na asilimia 90 na wageni walikuwa 75 sawa na asilimia 10. Katika eneo la tukio, juzi msimamizi wa mradi raia wa China aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa CCECC ambaye hakuwa tayari kutaja jina kwa madai si msemaji, alisema wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Serikali ya Tanzania na wanaamini watamaliza ndani ya muda.

Baadhi ya wafanyakazi waliokuwa katika ujenzi huo juzi, walisema hakuna ubabaishaji katika malipo yao na kueleza kuwa, wanafanya kazi kwa uzalendo na umakini kwa kuwa mradi huo ni kwa manufaa ya watoto na wajukuu wao. Walithibitisha taarifa ya Tanroads kuhusu matumizi ya barabara hiyo na kufafanua kuwa, barabara ya chini itaendelea kutumiwa na mabasi ya mwendo kasi na magari yatakayopishana kutoka Mwenge-Mbezi, Mbezi-Buguruni, Mjini- Mwenge na Buguruni-Mjini.

“Hizi barabara zikiisha tusahau kuhusu foleni, mwendo kasi itabaki chini pamoja na magari yanayopishana, juu wanaotoka Mwenge moja kwa moja kwenda Buguruni na katikati ni wa moja kwa moja Mbezi kwenda Mjini,” alisema fundi aliyejitambulisha kwa jina moja la Alex, huku akiungwa mkono na wenzake waliokuwa wakiendelea na ujenzi katika eneo la daraja la njia panda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kukamilika kwa mradi huo unaogharimu Sh bilioni 200.7 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), utawezesha zaidi ya magari 65,000 yanayotumia makutano ya barabara hiyo kupita bila msongamano uliopo sasa. Mwaka 2017, aliposaini mkataba wa ujenzi huo na CCECC, Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, alisema mradi unatarajia kutumia zaidi ya Sh bilioni 177.4 na alimtaka mkandarasi kuhakikisha kazi inaanza na inakamilika katika kipindi cha miezi 30 kwa mujibu wa mkataba.

“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha Sh bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya dia kwa wananchi walioguswa na mradi huo,” alisema Mfugale. Mradi wa Ubungo Interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia, Serikali kwa upande wake imelipa dia ya zaidi ya Sh bilioni 2.1 kwa wananchi waliohamishwa kupisha mradi huo.

Akizindua mradi huo kwa kuweka jiwe la msingi Machi 20 mwaka 2017, Rais Magufuli alisisitiza ujenzi wa kiwango na utekelezaji unaozingatia makubaliano ya mkataba. Rais wa Benki ya Dunia, Dk Jim Yong Kim, alishiriki katika uzinduzi huo.
 
Hatua njema kabisa hii.
Kwa hatu hii watu watahamasika sasa kukaa maeneo ya nje ya mji kuanzia mbezi kwenda mbele huko maana kuingia mjini haitakuwa bugdha tena
 
jengo la Tanesco vipi lishakuwa kifusi, au tumehairisha?

Hongera JPM kwa kuwaletea maendeleo wanaumbungo ambao wengi ni Wanachadema. Maendeleo hayana VYAMA.
 
Eti tatizo la foleni litakuwa limekwisha.Wanaota hawa.
Foleni haitakwisha; ila itapungua, au kuhamishiwa eneo jingine.
 
Kwa mabadiliko hayo ya mchoro ina maana juu kutakua na madaraja mawili kama la tazara moja linatoka mwenge kwenda Tazara jingine mbezi kwenda kariakoo na interchange itakua barabara ya chini. Hii ina maana pale chuni still tutakua na traffic light zitakazoruhusu magari kupishana yanapotoka mjini kwenda mwenge na Tazara kwenda kariakoo...

Ubahili utatuua...
1554368113381~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom