UJENZI na shilingi 252 bilioni

UJENZI na shilingi 252 bilioni

Sasa mlitaka madeni yasilipwe? hivi nyie watu vipi ? Halafu wakandarasi wangegoma mngemlaumu nani?

Umerukia treni kwa mbele, what does it take for someone to become a great thinker? Soma habari yote kwanza mkuu, vinginevyo kama kweli umesoma na bado unaleta post hii, moja kati ya yafuatayo au yote ni sahii.
1. Wewe ni gamba original na umekosa jibu
2. Wewe ni mtoto wa gamba na unamtetea mama/baba yako
3. Wewe ni mke/mme wa gamba na unamtetea mme/mke wako
4. Wewe ni mjukuu wa gamba na unamtetea babu/bibi yako
5. Wewe ni mamluki wa ile ndoa ya mseto kule zenji
****HATUKATAI MAWAZO YAKO, BILA KUJARI UBORA, UOZO AMA UTOTO ULIOJAA, HII NDIYO JF*******
 
kweli CCM kiboko, yaani wanalidanganya hadi Bunge? hawna hata aibu machoni?
 
Ndugu yangu nadhani huijui vizuri Tanzania inayolalamikiwa hapa.Mfumo uliopo kwa sasa hivi ni mahususi kwa ajili ya kulinda Maovu kama haya.Kama ambavyo Zitto ameeleza hapo juu Mamlaka ya kuanzisha mchakato wa kisheria kwa jambo hili ni CAG lakini kama ambavyo imeelezwa tayari ameshapewa maelekezo kutenda kunyume cha matakwa ya utendaji wake kisheria.Mambo kama haya si ya kuachia mtu mmoja kuyashughulikia ila kinachotakiwa ni kwa ujumla wetu kama wananchi wa Tanzania kukataa kutawaliwa kwa mfumo huu wa kutuingiza katika umaskini usio wa lazima.Nionavyo mimi Magufuli ndani ya CCM sasa anaonekana ni shujaa kwani katika harakati za kusaka hela za kampeni 2015 anaonekana ni mshika Bango mzuri.

Nakubaliana na wewe kua mfumo wa Nchi yetu unalinda maovu! Sasa Mh Zitto na na wengine wenye nafasi ya uongozi waangalie namna Ingine ya kuweza kutengeneza mfumo wa kuweza kuzibiti Haya mambo au kuwafikisha kwenye sheria! Kwasababu kutoa ripoti ni sawa lakini swali ni kwamba ripoti zitatolewa mpaka lini?
 
ahsante Mhe Zitto kwa taarifa mhimu sana haswa tunapoelekea 2015, hapo ni kutonesha tu watu hoi.
 
usiongee kama kasuku.... zito kasha play part yake ya ku expose ufisadi nadhan yeye hana jeshi la polisi wala mahakama ni muda wa vyombo husika kulichukua na kulifanyia kazi pamoja na wewe kama mwananchi kupiga kelele na kushinikiza lifanyiwe kazi badala ya kuto concern zako tu hapa mtandaoni!!!!

Anza kupiga kelele wewe uone Kama utasikika....! Zitto ajaribu kuangalia namna ingine pamoja na wenzake kuyashughulikia Haya mambo kisheria! Itafutwe mbinu ingine au mfumo mbadala wa kushughulikia Haya mambo! Lakini kuja na hizi ripoti kila Mara huku mafisadi wakiendelea kupeta tu hakusaidii kitu!
 
Sasa mlitaka madeni yasilipwe? hivi nyie watu vipi ? Halafu wakandarasi wangegoma mngemlaumu nani?

Sio unaandika porojo ili kuhakikisha hiyo buku 7 kama una uhakika wa kulipwa hao wakandarasi lete ushaidi humu. Pia kummbuka wanachoshitakiwa hawa mawaziri ni kulidanganya Bunge wewe unakuja na viroja humu.
 
Bongo kila kitu kinakanushwa tu kwa maslahi ya kisiasa.Hakuna uzalendo.Hata CAG?
Ngoja nizame kwenye kamusi nitafute maana ya "bongo-bongo land..."
 
Tatizo hili si la kwanza wala la pili, kuna viporo vingi kama hivi vimefichwa kwa jina la 'tume' n.k.
Wanoafanya hivi wanatujua vema Watanzania na wala hawana wasi wasi.
Matatizo yapo wapi?

1. MTAZAMO , kwa bahati mbaya taifa hili halina watu wa taaluma ya uandishi. Kila mmoja anaweza kuwa mwandishi.Habari hizi zilitakiwa ziandikwe kwa lugha rahisi na inayoeleweka kwa mwananchi.
Hakuna wa kufanya hilo, tuna reporters hatuna journalists. Pasco prove me right or wrong

2. Ujinga wa Wananchi.
a) Wananchi hasa wanachama wa CCM ni kikwazo katika kupata suluhu. Suala la linalogusa maisha yao watalifanya la kisiasa. Utawasikia wakiimba nyimbo za kubariki uozo huu, kwa bahati mbaya wao si sehemu ya mgao.Mwisho wa siku watalala kama nguruwe pale muhimbili, wakiamka na afadhali wanatudi kuisaga lami

b)Wananchi kudhani kazi yao imeisha baada ya uchaguzi na mbunge anakuwa kiongozi wa taifa na si wao.
Endapo wananchi wangesimama bila kujali itikadi za kisiasa leo kila jimbo lingemwita mbunge wake na kumwambia ima atoe majibu au atokomee kabisa wasimuone tena. Wananchi wa Tanzania uzezeta umetujaa

c)Sisi sote ni sehemu ya tatizo: Tunadhani kuwa mwenye uwezo ni Zitto au wapinzani.
Ukisoma maoni ya wengi wameacha sualalishughulikiwe na Bunge.

Hawa mawaziri ni wabunge na Wabunge wetu mnawajua viwango vyao, leo unamkabidhi nyani kesi ya tumbiri kula mahindi yako.Hawa walioshindwa kutetea Simcard. wazungumzie ulaji wao kweli!
i)Tuwasaidie wanaofichua maovu .kwa pamoja tutie shinikizo hadi wahusika wawajibishwe
ii)Tuwabane wabunge majimboni waache kutudanganya'wanaleta maendeleo', kodi zetu wanaziteteaje!
iii)Kuishinikiza serikali itupe majibu hela zimetoka kwa utaratibu gani, zimelipa madeni gani
 
Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu Matumizi ya shilingi 252 bilioni katika Wizara ya Ujenzi. Kamati ya PAC ilikutana na Wizara ya Ujenzi wiki iliyopita na hapo ndipo kashfa hii ilianza kuandikwa kwa uzito wake. Ikumbukwe kuwa suala hili Kambi ya Upinzani Bungeni ilianza kulihoji mwaka 2011 kutokana na Wizara kuomba fedha nyingi sana kama 'KUANZA miradi maalumu ya Barabara nchini' na maelezo ya Mawaziri wote kuonyesha kuwa huu ni mfuko maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa barabara na hakuna mahala hata pamoja ambapo Serikali ilisema hizi ni fedha za kulipa Madeni mpaka pale Taarifa ya CAG ilipotoka na kuonyesha kuwa huo mradi ulikuwa mradi hewa.

Kulipa Madeni sio tatizo hata kidogo, suala hapa ni kwanini Serikali iombe fedha Bungeni 'kuanza miradi maalumu ya barabara' wakati inajua inaomba Fedha kwa ajili ya kulipa Madeni? Ingesema inaomba fedha kulipa Madeni Bunge lingekataa? Ndio maana PAC imeamua kuwapeleka kwenye kamati ya Maadili Mawaziri Magufuli, Mwakyembe na Lukuvi kwa kulidanganya Bunge wakati wa kuomba Fedha hizo.

Suala la pili, ni je Fedha hizo zimetumika kulipa madeni yepi wakati kila mradi una kasma yake? Katika hili PAC iliamua kuwa CAG akague matumizi ya Fedha hizo kisha atoe Taarifa kwenye Kamati.

Serikali kwa nini inahaha sana kuhusu suala hili? Katibu Mkuu wa Wizara alipewa muda wa kutosha kabisa katika Kamati kujieleza. PAC huruhusu waandishi wa Habari kuhudhuria vikao vyake na kushuhudia mahojiano kati ya Kamati na Makatibu Wakuu. Ni vema Katibu Mkuu asubiri uhakiki wa Fedha hizo na zilivyotumika. Ni vema pia aache suala la Kamati ya Maadili liende Kamati ya Maadili ambapo Mawaziri hao, Magufuli, Mwakyembe na Lukuvi watajieleza kwa nini walidanganya Bunge wakati wa kuomba Fedha hizo.

Nimesikia CAG kaitwa na Katibu Mkuu Kiongozi na kumtaka awasafishe. Ukweli ni kwamba PAC ilitumia taarifa ya CAG na ni yeye CAG aliyeita matumizi haya kuwa ni matumizi hewa na mradi wenyewe kuwa ni mradi kivuli. Taarifa ya Kambi ya Upinzani Bungeni imenukuu kauli za Mawaziri wakati wa mjadala wa Bajeti za Serikali na Taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni, 2012. Sehemu ya Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni hii hapa

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA BARABARA
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwenye bajeti ya mwaka 2011/2012 tulihoji kuhusiana na fedha zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililojulikana kama “special road construction project” , na tulisema ifuatavyo; Nanukuu hansard ya tarehe 01.08.2011 “Mheshimiwa Spika, Miradi maalum ya ujenzi wa barabara (kasma 4168).kitabu cha Miradi ya Maendeleo (sehemu-A juzuhu iv) katika fungu 98, kasma 4168 utaona kuwa mradi unaitwa “Miradi ya ujenzi wa barabara maalum” (special road construction projects) na fungu hili limetengewa kiasi kikubwa kuliko miradi mingine yoyote ya ujenzi wa barabara katika mwaka huu wa fedha kwani zipo jumla ya sh. 348,075,000,000/= na hizi zote ni fedha za ndani. Kwa hakika hizi ni fedha nyingi sana na hasa ikizingatiwa kuwa kitabu hicho kimeonesha miradi yote ya ujenzi wabarabara ambayo itatekelezwa katika mwaka huu wa fedha, ila hii miradi maalum haijaoneshwa ni miradi ya barabara gani na zitajengwa wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kasma hii kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na 2010/2011 haikuwa imetengewa kiasi chochote cha fedha na ndio maana imetustua kuona mwaka huu fedha nyingi kiasi hicho zinatengwa kwa miradi isiyojulikana kuwa itajengwa wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata ukiangalia maelezo yaliyotolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Miundombinu juu ya mpango na bajeti ya mwaka 2011/2012, kasma 4168 haipo kwenye randama na hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhusiana na fedha hizo ambazo zimetengwa. (Makofi)

Kambi ya Upinzani, tunataka kupata maelezo ya kina ni miradi gani hii ambayo haiwezi kuandikwa na inatengewa fedha nyingi kiasi hicho? Kwani hii italiwezesha Bunge kuweza kupitisha bajeti inayoifahamu na kuisimamia Serikali kwa kuweza kufuatilia utekelezaji wa miradi husika”.

Mheshimiwa Spika, wakati wa mjadala kuhusiana na hotuba ya wizara ya uchukuzi 2011/2012 ilipowasilishwa , Mhe.Mbunge wa Ukerewe Salvatory Machemli alihoji fedha hizi na kusema , naomba kunukuu Hansard ya tarehe 03.08.2011 “Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaja mwanzoni kwamba reli inakufa wakati watu wanaiangalia na Serikali haisemi kitu chochote kazi yao kuomba Miongozo tu hapa, pesa zipo nyingi. Wakati mimi nawasilisha hotuba yangu kwa Wizara ya Ujenzi, nilihoji kiasi cha pesa shilingi bilioni 348 ambazo hazikuonyeshwa zinafanya kazi gani kwenye Wizara ile. Mheshimiwa Magufuli jana wakati anafanya majumuisho hakutaja, amemeza tu japokuwa aliona ni chungu lakini akameza kama chloroquine, nataka sasa hizi shilingi bilioni 348 ambazo zimeonyeshwa kwenye vote 4168 ambazo matumizi yake hazikuonyeshwa basi wapelekewe reli ili tuimarishe reli, tuweze kuokoa barabara zetu kuliko kuziacha tu, jamaa wanatia mfukoni, wanachukua wanaweka waa, kama ilivyo kawaida yenu Chama cha Mapinduzi, mnakwenda kujenga masinagogi Ulaya. (Makofi)”

Mheshimiwa Spika, katika mjadala huo aliyekuwa naibu waziri wa Ujenzi Mhe.Dr.Harison Mwakyembe alijibu kuhusiana na hoja hiyo na kusema , nanukuu hansard ya tarehe 03.08.2011 “NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili Mheshimiwa Mbunge asiendelee kupotosha na kujenga mahekalu hewani, nilitaka kumueleza kwamba hizo pesa zilizopitishwa hapa jana ni za Mfuko Maalum ambao unaisaidia Serikali pale ambapo mfadhili wa nje kwa mfano, anaamua kufadhili ujenzi wa barabara fulani na anasema Serikali ichangie ten bilioni, utaitoa wapi kama wewe huna Mfuko Maalum? Serikali ikaona logic ya kuweka Mfuko Maalum ili isitulazimu tena kuitisha Bunge kupitisha pesa hizo, sasa zianze kuleta maneno, kutufanya wote ni wahuni kama yeye na hii siyo vizuri kusema kwamba tutapeleka hizo pesa wapi? Ahsante. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 04.08.2011 wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Mhe.waziri Mkuu alitoa kauli ya serikali kuhusiana na fedha kuongezwa wizara ya uchukuzi na alisema, nanukuu hansard ya tarehe husika…..’Kwa hiyo, baada ya Kamati ya Miundombinu kupitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kuishauri Serikali kuongeza bajeti hiyo kwa shilingi bilioni 95, jambo ambalo tuliliridhia na kulikubali, lakini hatukuweza kufikia kiwango hicho kama ilivyokuwa imeombwa. Kikao cha jana kimewezesha Serikali kufanikiwa kupata fedha hizo ambazo zitatumika kwenye maeneo matatu yafuatayo: Reli ya Kati, Kampuni ya Ndege Tanzania na Usafiri wa Majini yaani Meli katika Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Kiasi hicho cha shilingi bilioni 95 ni kiasi ambacho Wizara ilikuwa imeji-commit au imejiahidi mbele ya Kamati kwamba, zikipatikana zitawezesha huduma za msingi katika maeneo hayo matatu kuweza kuendelea bila matatizo makubwa. (Makofi)’

Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati ya matumizi wakati wa kupitisha mafungu ya wizara ya uchukuzi Mhe. Tundu lissu aliomba ufafanuzi kama ifuatavyo, nanukuu hansard “ …..Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba nifafanuliwe, kama Bajeti ya Wizara ya Ujenzi ilishapitishwa mafungu yote yalishapitishwa, hii bilioni 95 iliyochotwa kutoka fungu la miradi maalum ya barabara na kuletwa kwenye miradi ya maendeleo ya Wizara ya Uchukuzi ambayo ni Vote tofauti kabisa zimechotwa kwa idhini ya Kanuni ipi, mimi naomba nipewe angalau msingi wa Kikanuni au wa kisheria wa kuchota fedha ambazo tayari zimeshatengwa na Bunge hili bila kupata authorization ya Bunge hili. Ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, majibu yafuatayo yalitolewa,kwa mujibu wa Hansard “ WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu alichokisema Mheshimiwa Tundu Lissu kipo ukurasa 276, Kifungu kidogo cha 4168. Hizi ni fedha ambazo zimewekwa katika Kifungu hiki katika Bajeti hii ya ujenzi lakini ni mfuko maalum, hela hizi hazijawa committed kama unavyoziona. Ukiangalia miradi yote iliyomo katika kfungu hiki ina barabara tayari. Fedha hizi ziliwekwa maalum kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya miundombinu hasa katika maeneo ambayo ipo miradi kadhaa ambayo tuna uzoefu, imekuwa inachangiwa inatolewa na wafadhili, lakini hii tulifikiri sehemu nyingine miradi hii imekwama kwa sababu sisi tulikuwa hatujajitayarisha kuweka counterpart fund. Kwa hiyo, hizi fedha zimewekwa hapa kwa ajili hiyo, miradi yote ambayo Serikali ya Tanzania itafanya kutoka kwenye fedha za wafadhili hizi ni fedha ambazo zimewekwa, ni fungu ambalo haliko committed. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hizi fedha zimechukuliwa hapa zimepelekwa ujenzi kwa maana ya kwamba ni fedha ambazo ziliwekwa kwa ajili ya mfuko wa miundombinu. Zimekuwa voted lakini Mheshimiwa Tundu Lissu atakuja kupata ukweli wa mambo haya yote wakati wa Appropriation Bill. (Makofi)


Mheshimiwa Spika, baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu“malipo ya madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi usiohalisi shs.252,975,000,000. Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi” (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98)

Mheshimiwa Spika, fedha hizi “zilizopotea”au “kulipwa kifungu hewa” ni sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara zifuatazo kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014;
i. Barabara ya Usagara-Geita-Kyamyorwa (KM 422)
ii. Barabara ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza-Kaliua-Tabora (KM 443)
iii. Barabara ya Nangurukuru-Mbwemkulu (KM 95)
iv. Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (KM 112)
v. Barabara ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264)
vi. Barabara ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda (KM 359)
vii. Barabara ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi-Londo-Lumecha/Songea(KM- 396)
viii. Kuondoa msongamano barabara za Dar (KM- 102.15)

Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane (800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya –Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu –Goba (KM 9), zimepotea kutokana na ufisadi huu.

Kambi rasmi ya upinzani, inataka kupata majibu yafuatayo kuhusiana na suala hili;
i. Fedha hizi zilizokuwa zimetengwa zilitumika kwa ajili ya kufanyia shughuli gani? Kwani majibu yaliyotolewa na wizara na serikali Bungeni sio yaliyotolewa kwa mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
ii. Ni madeni gani yalilipwa kama kweli yalikuwepo?au wajanja wachache walijinufaisha ? na wahusika wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa.
iii. Nini kauli ya serikali kuhusiana na Ufisadi huu, mbele ya Bunge na watanzania kwa ujumla .
iv. Je, Tunaweza kuendelea kuamini kauli za viongozi wa serikali hii ndani ya Bunge kama hii ndio hali halisi ?
v. Nini kauli ya serikali kuhusiana na Ufisadi huu.


Muhimu
Tusifanye kila jambo ni siasa. Hili ni suala la Uwajibikaji. Hoja hii iliibuliwa na Kambi ya Upinzani Bungeni tangia Fedha hizi hazijaidhinishwa na Bunge. Tumekuwa very consistent katika jambo hili. Tumeendelea kulihoji baada ya Taarifa ya CAG kutoka.

Tumeendelea kuhoji kwenye Kamati ya PAC ambapo Katibu Mkuu wa Wizara alitoa majibu yaliyodhihirisha kuwa Serikali iliomba Fedha Bungeni kwa udanganyifu, haikusema ukweli fedha hizo wanataka kufanyia nini? Hapakuwa na sababu ya Mawaziri kusema uwongo Bungeni ili Bunge liidhinishe Fedha. Wasipowajibishwa kwa haya, wataendelea kuwa wanasema uwongo.

Kama fedha hizo zilitumika vema bila ufisadi wowote uhakiki wa CAG utaonyesha hivyo na tutasema wazi. Kama CAG akiueleza umma kuwa hakuna ufisadi bila ya yeye kufanya uhakiki itakuwa ndio yale mambo ya Jairo ambayo yalimvunjia heshima. Naamini kuwa atafanya ukaguzi huo na kutoa taarifa kwa umma maana hoja ya ukaguzi ni yake na kama pasingekuwa na makosa asingeiweka kwenye taarifa yake ya mwaka aliyoitoa Bungeni mwezi Machi mwaka 2013.

Kamwe tusikubali majibu mepesi mepesi kwenye masuala ya fedha za Umma. Kamwe tusikubali kugeuza kila jambo ni siasa.

Fedha za Umma zinaombwa hadharani kupitia Bunge la Bajeti. Matumizi ya Fedha za Umma lazima yafanyike hadharani kwa kamati za mahesabu kufanya vikao vyao kwa uwazi na kuruhusu vyombo vya habari


Naomba tupitie hizi cli za video kwa mtililiko huu ili pia kuona nani ni mkweli katika hili:

1. HOJA ILIYOKUFA YA MH.ZITTO VS DR.MAGUFULI NA UPOTEVU WA TSH 252 BILION (SOURCE : YOUTUBE)

HOJA ILIYOKUFA YA MH.ZITTO VS DR.MAGUFULI NA UPOTEVU WA TSH 252 BILION - YouTube

2. WIZARA YA MAGUFULI YAMJIBU ZITTO KABWE(SOURCE:JF)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Yah: USAHIHI WA MATUMIZI YA KASMA MAALUM YAUJENZI WA MIRADI YA BARABARA NCHINI SHS. 252,975,000,000.00


Tarehe 22/08/2013, Wizara ya Ujenzi ilikutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa ajili ya kujadili Hesabu zilizokaguliwa za Fungu 98 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kikao hicho kilifanyikia katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Mhe. Gaudence Cassian Kayombo Mbunge wa Mbinga Mashariki, ambaye alitoa maamuzi na maelekezo rasmi ya Kamati.

Katika kikao hicho hoja kadhaa zilijadiliwa ikiwamo hoja kuhusu Matumizi ya Kasma Maalun ya Ujenzi wa Miradi ya Barabara nchini ambayo ilitengewa kiasi cha Shs. 252,975,000,000.00.

Katibu Mkuu (Afisa Masuhuli) wa Wizara ya Ujenzi alikiarifu kikao hicho kuwa fedha za Mradi huo Maalum zilitumika kwa ajili ya kulipia madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mipango na bajeti ya Serikali. Katika ujenzi wa barabara; jukumu la msingi kwa Wizara ni kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri.

Aidha, alifafanua kwamba Mradi huu umekuwa na matokeo mazuri kwani ulifanikisha shughuli za ujenzi wa barabara nchini. Afisa masuhuli aliendelea kufafanua kwamba mradi huu wa barabara haukuwa mradi kivuli bali ulikuwa ni mradi maalum kwa lengo la kufanikisha programu ya barabara na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Tarehe 22/08/2013 na tarehe 23/08/2013 zimetolewa taarifa za upotoshaji na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ukweli wa suala hili ambapo baadhi ya vyombo hivyo vilinukuliwa kusema kuwa kumekuwepo na ufisadi, matumizi tata na ubadhirifu katika mradi huu.

Wizara inapenda kuudhibitishia umma kwamba katika utekelezaji wa mradi huu hapakuwepo na ufisadi, ubadhilifu, au matumizi tata.

Ukweli huu umethibitishwa kwa maandishi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwamba hoja ya ukaguzi huu haikuhusu ubadhirifu au matumizi mabaya yoyote ya fedha bali ni suala la uandishi wa vitabu vya fedha uliohitaji kuboreshwa.

Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia tena umma kwamba hakuna upotevu wowote wa fedha kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimetaka ieleweke.

Taarifa hii imetolewa na;


Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU (AFISA MASUHULI)
WIZARA YA UJENZI


3. CAG AKANUSHA MADAI YA KUWEPO UFISADI KATIKA MRADI MAALUM WA WIZARA YA UJENZI (SOURCE: YOUTUBE & Michuzi)

CAG LUDOVICK UTOUH BIL.252/- ZA WIZARA YA UJENZI - DR.MAGUFULI ALISHUTUMIWA KUZITUMIA VIBAYA - YouTube

MICHUZI BLOG: CAG AKANUSHA MADAI YA KUWEPO UFISADI KATIKA MRADI MAALUM WIZARA YA UJENZI

4. MBOWE ALIPOMSIFU JK (SOURCE: YOUTUBE & JF)

Mbowe Clip - YouTube

5. CHEYO ALIPOISIFU WIZARA YA UJENZI (SOURCE: YOUTUBE & JF)

JOHN CHEYO AKIMSIFU DR.MAGUFULI - MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI - YouTube

6. MKOSAMALI AUNGA MKONO HOJA YA SERIKALI (SOURCE: YOUTUBE & JF)

MKOSAMALI AIPONGEZA BAJETI YA UJENZI NA KUUNGA MKONO HOJA - YouTube

Hizi clips zinasdambazwa sana humu JF????!!

Nawalkilisha
 
Tatizo hili si la kwanza wala la pili, kuna viporo vingi kama hivi vimefichwa kwa jina la 'tume' n.k.
Wanoafanya hivi wanatujua vema Watanzania na wala hawana wasi wasi.
Matatizo yapo wapi?

1. MTAZAMO , kwa bahati mbaya taifa hili halina watu wa taaluma ya uandishi. Kila mmoja anaweza kuwa mwandishi.Habari hizi zilitakiwa ziandikwe kwa lugha rahisi na inayoeleweka kwa mwananchi.
Hakuna wa kufanya hilo, tuna reporters hatuna journalists. Pasco prove me right or wrong

2. Ujinga wa Wananchi.
a) Wananchi hasa wanachama wa CCM ni kikwazo katika kupata suluhu. Suala la linalogusa maisha yao watalifanya la kisiasa. Utawasikia wakiimba nyimbo za kubariki uozo huu, kwa bahati mbaya wao si sehemu ya mgao.Mwisho wa siku watalala kama nguruwe pale muhimbili, wakiamka na afadhali wanatudi kuisaga lami


Kweli kabisa mkuu,

CAG kapiga siasa pia.Anasema hakuna ufisadi kwenye hili simply ameamua kutumia vizuri maana halisi ya neno ufisadi kupindisha ukweli wa makosa ya msingi kabisa juu ya jinsi fedha hizi zilivyoombwa na kuja kutumika (Misappropriation).

Ilipaswa waziri akubali haya makosa na watuambie kwanini watumie mbinu hiyo kuomba fedha Bungeni bila kusema wazi makusudi halisi ili wabunge wahoji vizuri.

CAG kanishangaza zaidi anasema ni makosa ya kiuhasibu tu!!!! Siasa hizi hadi kwa watu professional!! Waandishi wetu kama kawaida habari zao ni CAG awasafisha akina magufuli blah blah!!! Hakuna aliandika kwa kuchambua udhaifu wa wazi juu ya hili wanasubiri akina Zitto waandike makala kufafanua basi!!!

Swali la msingi madeni yametoka wapi while fedha za ujenzi wa barabara zote zilitengewa bajeti? Kama kulikuwa na madeni kwanini hakuomba fedha za hayo madeni ili bunge lihoji vizuri?
 
Kumbe kiwango cha ujinga wa wananchi wa Tanzania kinaweza kuwa kikubwa kuliko inavyodhaniwa!
 
Ungesoma hadi mwisho na kuelewa, sidhani kama ungeibuka na post ya hivi. Kuna tatizo.

Kwa fungu lenye kiasi kikubwa kama hicho cha Shs. 252 bilioni kwamba limepitishwa na Bunge makini bila ya kujua miradi husika iliyomo ndani ya fungu hilo ni jambo la kujiuliza.
 

1. MTAZAMO , kwa bahati mbaya taifa hili halina watu wa taaluma ya uandishi. Kila mmoja anaweza kuwa mwandishi.Habari hizi zilitakiwa ziandikwe kwa lugha rahisi na inayoeleweka kwa mwananchi.
Hakuna wa kufanya hilo, tuna reporters hatuna journalists. Pasco prove me right or wrong
Mkuu Nguruvi3, kusema Tanzania hatuna waandishi, sio kututendea haki, kwa sababu waandishi tupo, maripota pia wapo na maanalist pia wapo, ila tatizo ni level tuu!.

I can't prove you right or wrong kutokana na views zako kwa sababu huo ni mtazamo na its relative!.Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Tanzania waandishi tupo ila level yetu na uwezo wa kuchanganua mambo mazito ni limited kwa sababu hatuna kada ya waandishi waliospecialize kwenye technical issues kama hizi.

Kwa miaka 4 mfulilizo, nimekuwa nikiwaletea humu ripoti za CAG ile siku zinatoka tuu!, lakini sii wengi wenye uwezo wa kuzisoma kuzielewa na kuzichambua ipasavyo, ndio itakuwa sisi waandishi?!. Angalia CNN, kukiwa na technical issues, wanamuita pro. Wakati wa vita vya Gulf, CNN walimuajiri retired joint chief of staff kuwa war commentator!.
Media yetu ipi ina jeuri ya kumuajiri Mboma, Sarakikya au Sayore?!.

Siku ya bajeti ambayo ni moja kwa Tanzania, Kenya na Uganda, soma magazeti ya Kenya na Uganda wanavyoripoti bajeti zao!. Hata Bajet yetu, inachambuliwa vizuri zaidi kwenye gazeti la The East Africa kuliko gazeti la Daily News!.

Ili tuwe na specialization, inabidi mtu aliyesoma uchumi to degree level, then akasoma journalism, then anakuwa na uwezo wa kuandika uchambuzi wa kina!.

Hili la kusema Tanzania hatuna hiki au kile sii haki, unamaanisha waandishi wote hawa humu Tanzania huwaoni?!. Hivi ni kweli wote tunaoandika hata humu tuu, wote ni maripota tuu?!, hakuna waandishi?!, au angalau hata wachambuzi?!.

Pasco



 
Mkuu @Nguruvi3, kusema Tanzania hatuna waandishi, sio kututendea haki, kwa sababu waandishi tupo, maripota pia wapo na maanalist pia wapo, ila tatizo ni level tuu!.

I can't prove you right or wrong kutokana na views zako kwa sababu huo ni mtazamo na its relative!.Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Tanzania waandishi tupo ila level yetu na uwezo wa kuchanganua mambo mazito ni limited kwa sababu hatuna kada ya waandishi waliospecialize kwenye technical issues kama hizi.

Kwa miaka 4 mfulilizo, nimekuwa nikiwaletea humu ripoti za CAG ile siku zinatoka tuu!, lakini sii wengi wenye uwezo wa kuzisoma kuzielewa na kuzichambua ipasavyo, ndio itakuwa sisi waandishi?!. Angalia CNN, kukiwa na technical issues, wanamuita pro. Wakati wa vita vya Gulf, CNN walimuajiri retired joint chief of staff kuwa war commentator!.
Media yetu ipi ina jeuri ya kumuajiri Mboma, Sarakikya au Sayore?!.

Siku ya bajeti ambayo ni moja kwa Tanzania, Kenya na Uganda, soma magazeti ya Kenya na Uganda wanavyoripoti bajeti zao!. Hata Bajet yetu, inachambuliwa vizuri zaidi kwenye gazeti la The East Africa kuliko gazeti la Daily News!.

Ili tuwe na specialization, inabidi mtu aliyesoma uchumi to degree level, then akasoma journalism, then anakuwa na uwezo wa kuandika uchambuzi wa kina!.

Hili la kusema Tanzania hatuna hiki au kile sii haki, unamaanisha waandishi wote hawa humu Tanzania huwaoni?!. Hivi ni kweli wote tunaoandika hata humu tuu, wote ni maripota tuu?!, hakuna waandishi?!, au angalau hata wachambuzi?!.Pasco
Mkuu Pasco , niseme nilitambua hili litaku provoke kidogo pengine kukukihiri. Tumekuwa tunajadiliana kuhusu hili si mara moja au mbili sometime tunakuwa page moja na wakati mwingine tofauti, jambo zuri ni kuwa huwa tuna hoja za kujenga.

Mwaka 2011 niliandika kuwa si lazima kuwa na mwandishi wa habari wa taaluma, kinachotakiwa ni mwandishi wa habari mwenye kuelewa(weledi) wa mambo. Huyu ataweza kujua habari gani ifafanuliwe na nani. Kilichopo ni maripota ambao hawajui right source za info. Journalist waliopo nao wameingia katika mkumbo wa sensational news badala ya kufanya 'analysis' kutafuta habari zaidi na kuziandika katika lugha nyepesi.
Ni kwasababu hizo wao hawaonekani, tunaona maripota

Kuna uwezekano kabisa wa vyombo kuajiri wataalam kama part time, kwamba kila anapohitajika analipwa.
Tatizo siyo kupata wenye taaluma, tatizo hao waliopo wanajiendeleza na kupanua wigo wao wa ufahamu?

Watanzania hasa vijana wana tatizo. Wao wanategemea kusoma ajira za magazetini.
Wanashindwa kuwa aggressive na wanadhani taaluma zao zinazungumza zenyewe.

Miaka ya 70 na 80 watu walikuwa wanatumiwa barua za scholarship kama wanataka.
Form 6 akimaliza tu ajira kabla ya kwenda chuo. Siku hizi mambo sivyo, competition ni kubwa sana tena yenye ''technical know who na si know how''

Unaweza kuwa na digriii zako za nguvu zenye GPA ya haja. Digrii hazizungumzi wala hazielezi wewe ni nani katika free market. Soko linatawali na wewe nina, una nini na unaleta nini mezani.
Soko la ajira ni biashara kwamba inabidi utangaze kama wanavyotangaza wafanyabiashara.

Katika upande wa journalism soko lipo huru na wazi kabisa. Wewe kama Engineer, Lawyer, Mchumi n.k. kwanini usijitolee muda wako kufanya kazi za kufafanua, kuandika kuhusu taaluma yako ukiomba msaada wa mwandishi mkongwe kuweka habari zako katika hali inayokubalika?

Katika soko overcrowded kama hili la leo nani atakuona kama hutafanya jitihada za kuonekana?



Atakayeona kitu ni PM.
 
Back
Top Bottom