UJENZI na shilingi 252 bilioni

UJENZI na shilingi 252 bilioni

Mkuu Pasco , niseme nilitambua hili litaku provoke kidogo pengine kukukihiri. Tumekuwa tunajadiliana kuhusu hili si mara moja au mbili sometime tunakuwa page moja na wakati mwingine tofauti, jambo zuri ni kuwa huwa tuna hoja za kujenga.

Mwaka 2011 niliandika kuwa si lazima kuwa na mwandishi wa habari wa taaluma, kinachotakiwa ni mwandishi wa habari mwenye kuelewa(weledi) wa mambo. Huyu ataweza kujua habari gani ifafanuliwe na nani. Kilichopo ni maripota ambao hawajui right source za info. Journalist waliopo nao wameingia katika mkumbo wa sensational news badala ya kufanya 'analysis' kutafuta habari zaidi na kuziandika katika lugha nyepesi.
Ni kwasababu hizo wao hawaonekani, tunaona maripota

Kuna uwezekano kabisa wa vyombo kuajiri wataalam kama part time, kwamba kila anapohitajika analipwa.
Tatizo siyo kupata wenye taaluma, tatizo hao waliopo wanajiendeleza na kupanua wigo wao wa ufahamu?

Watanzania hasa vijana wana tatizo. Wao wanategemea kusoma ajira za magazetini.
Wanashindwa kuwa aggressive na wanadhani taaluma zao zinazungumza zenyewe.

Miaka ya 70 na 80 watu walikuwa wanatumiwa barua za scholarship kama wanataka.
Form 6 akimaliza tu ajira kabla ya kwenda chuo. Siku hizi mambo sivyo, competition ni kubwa sana tena yenye ''technical know who na si know how''

Unaweza kuwa na digriii zako za nguvu zenye GPA ya haja. Digrii hazizungumzi wala hazielezi wewe ni nani katika free market. Soko linatawali na wewe nina, una nini na unaleta nini mezani.
Soko la ajira ni biashara kwamba inabidi utangaze kama wanavyotangaza wafanyabiashara.

Katika upande wa journalism soko lipo huru na wazi kabisa. Wewe kama Engineer, Lawyer, Mchumi n.k. kwanini usijitolee muda wako kufanya kazi za kufafanua, kuandika kuhusu taaluma yako ukiomba msaada wa mwandishi mkongwe kuweka habari zako katika hali inayokubalika?

Katika soko overcrowded kama hili la leo nani atakuona kama hutafanya jitihada za kuonekana?

Atakayeona kitu ni PM.
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nalia na wewe, yaani hujaona hata mmoja mmoja wa kutafuta?.
Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe, ila pia kwa bongo, uandishi ni noble professional, inafanywa kwa mapenzi na wito and not kwa ajili ya take home!.

Wako waandishi nawafahamu, waliospecialize, hawakurudi tena newsroom.
Hivi unajua Dr. Mlimka, Dr. Harison Mwakyembe, Dr. Sengodo Mvungi, Prof. Palamagamba Kabudi, Benjamin William Mkapa, Sammy Mdee etc, etc, wote hawa ni waandishi wa habari?. Waliondoka newsroom na kwenda ku specialize, hawakurudi tena newsroom kwa sababu hicho walicho specialize, paid them more!.

Kiukweli the going kwa waandishi wa habari, is very tough, and the tough is not going!. Watu wanaandika kwa mapenzi tuu no for returns, ukiondoa wale waliofika newsroom na kugota kwa sababu they have no where else to go, iko kada yetu ambao tunaandika au kuripoti just for the love of it!. Sisi ndio tunaopaswa kuspecialize but them for what?!.

Wakati wa cold war, nchi za East zimetrain Watanzania wengi sana katika fani ya media to masters level, wamerudi bongo wanafanya mambo mengine better paying jobs!. Sasa kama waliosomeshwa ndio hao wamekimbia, watakao specialize na kubaki ni kina nani?!.

We are doomed kwenye uchumi, we are doomed kwenye siasa, and we are doomed kwenye jamii media ikiwa among, doomed bongo media! Dam! ila hii ndio yetu!.

Msisitizo wa kutotutendea haki bado upo, appreciate hata hao wachache waliopo ili tuwapate wengi, ila we have few good ones, very good analysts na wengine ni pro, need not mention names!.
 
Back
Top Bottom