Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,590
- 28,571
Siyo siri, ujenzi wa mradi wa Dar es salaam Rapid Transport(DART), una matatizo makubwa.
Mkandarasi barabarani hana vifaa kabisa vya kukidhi kazi hizi kubwa.
Kwa observation ya wazi ni kwamba mkandarasi mchina, kwanza hana uwezo.
Pili linaloigusa Serikali moja kwa moja ni kwa nini mkandarasi au hawa wakandarasi wa kichina wamefumua jiji zima la Dares salaam.
Hizi ni dalili ya poor project management kwa upande wa serikali.
Haingii akilini, kwamba kuna mtu serikalini, anaona yanayoendelea sasa Jijini na yuko kimwa utafikiri kila kitu kiko sawa.
Wananchi wameanza kulalamika kupoteza muda barabarani, magari kuharibika kwa mashimo mengi ya barabara za mchepuko.
Kiujumla miradi hii ni aibu kwa Taifa.