Ujenzi barabara: Wabunge wamkumbuka Hayati Magufuli

Sawa, tumshukuru mama kwa lipi hapo? Amezindua Tanzanite, atazindua Busisi, yale majengo ya magomeni, n.k

Je, ni nani anahusika moja kwa moja na yote hayo? JK, JPM au SH?

SGR imeanza lini? Meli za kwenye maziwa makuu? Zahanati 400, ukarabati wa shule ngapi za serikali? Si ajabu zikazinduliwa na mama pia!
Ametoa pesa za kukamilisha na anaendelea kulipa madeni..

Aliyezindua ndio mhusika, mipango sio matumizi bali mtoa pesa..
 
Sure mkuu. kuna miradi kibao alizindua afu hakujenga yeye. Na akawa anajipa maujiko kuwa nimeweza hiki sijui nini. Binafsi jiwe sijawahi mkubali na siwezi mkubali kwa maana aliharibu hili taifa mno
Aliharibu eneo gani wengi mnaompinga J.P.M ni mabwabwa hongereni kwa kupata uhuru sasa
 
KWA hilo povu ujue awezi kufutika maana bado yupo hai kiroboto unachanganyikiwa hata hakitajwa kwa ulivyo hata pepo hulipuka likisikia jina la yesu na mtatukana sana
Hata Hitler na Idd Amin wako hai ila hakuna legacy zao na kama zipo zinatumika kama mifano mibaya
 
Madharavya kuwa na vyeti feki. Haya mmerudishwa tena kazini nenda kajiendeleze.
Tunakula maisha yakiwemo mafao,si unajua tena kichaa anaoza huko 👇

Screenshot_20220520-081529.png
 
Magufui alikuwa na mikoa yake ya kujenga barabara.
Kuna mikoa aligoma kabisa.
Mbeya ni mfano mzuri.
Barabara ya Igawa-Tunduma , yenye kilometa karibu 200, na kuby-pass Jiji a Mbeya imeimbwa wakati wa ilani za Uchaguzi toka miaka ya Mkapa na Mwinyi.

Magufuli amekuwa waziri wa ujenzi mpaka rais miaka zaidi ya 20, na hakuna ilichofanyika.
Kule kwetu milimani barabara ya Tukuyu-Mbambo -Busokelo-Mwakaleli-Katumba, ya karibia kiometa 90, imeimbwa weee...... miaka yote ya uchaguzi.
Makandarasi yupo lakini kazi iliyofanyika ni kidogo sana.

Ujenzi wa barabara mwendazake alichagua za kujenga.
Hahaha unataka ajenge maremu mbona mnachuki hadi mnatia kinyaa
 
Ndio nimeumia mnoo maana mtu aliyevuruga mpango wa Ujenzi barabara alikuwa Magufuli..

Alihamisha bajeti ya barabara ikahamia kwenye reli na sgr,miaka 6 ya Magufuli kajenga chini ya km2,000 za lami wakati Tulikuwa tunajenga wastani WA km 2500-3000 kwa miaka 5..

Hao hata walie au wapige sarakasi hakuna kitakachobadilika kwa sababu pesa hazitoshi..

Hayo ndio matokeo ya kuwa na mtu asiye na akili.Binafsi ninakereka Sana na Mwendazake kwa sababu aliharibu mambo mengi mno..

Mfano mkoa wa Songwe alijenga km 50 tuu kwa miaka yote 6,Rukwa hata km 1 hakuna,Katavi ndio alijenga km 390 kwa sababu Waziri wa Ujenzi alikuwa wa huko ndio hiyo barabara Rais alizindua juzi..

Kigoma hakuna, barabara zimeanza kujengwa mwaka juzi baada ya mkopo wa

Yaani kiufupi hakuna Mkoa ambao barabara zilijengwa zaidi ya km 100 kwa miaka 6..Mwaka wa kwanza wa Samia karibu pesa yote ya Wizara ya ujenzi imelipa madeni ya wakandarasi..

Mwaka huu ndio pengine barabara zitaanza kujengwa kwa angalau Kwa speed ya awali.
Dogo Rukwa barabara ya Kutoka Matai kwenda Kasanga KM 60 na zaidi, barabara za Dar kwasasa mnazurura zimejengwa Kwa wingi wakati wa JPM, barabara ya Mpanda Tabora, kamalizia Barabara ya Itigi-Tabora, Chunya Makongorosi, Songea-Mbinga-Mbambay, Biharamulo-Muleba, Mwigumbi-Bariadi-Lamadi, Bunda-Kisorya (najua haijaisha kipande Fulani), Kujenga upya Barabara ya Mafinga-Makambako-Igawa, Dodoma-Babati kamalizia yeye, nk wakati mwingine tusiongee kuona hakuna kilichofanyika,
 
Hivi magufuli alijenga kilomita ngapi za lami? Maana hata hii lami iliyozinduliwa juzi Tabora ni kazi ya Kikwete.
Acha uongo, hicho kipande alichozindua mama kajenga magufuli akiwa rais, kikwete alijenga tabora to kigwa na manyoni to chaya, chaya kigwa kajenga JPM
 
Wabunge waliochangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi wamelia na kusuasua kwa ujenzi wa barabara za majimboni mwao.

Wengine wamefikia hatua ya kumkumbuka Mwamba hayati Magufuli

Chanzo: Bungeni
Hivi nyie mnaomuita mwamba ni utani tu au mna maaanisha. Yule hakustahiri hata kuwa mkuu wa wilaya Mana ni zero brain.
 
Makubwa 10 yaliyotendeka wakati wa JK, miaka 5 ya kwanza, kisha tufananishe 10 makubwa yaliyotendeka miaka 5 ya JPM, yawekeni hapa, sio kupiga ngonjera na kutetea matumbo yenye njaa tu!
Ok. Twende kazi
1. Jk watoto walisoma vyuo na kupata mikopo na ajira nje nje.
2. Wafanyakazi walipandishwa madaraja na kulipwa stahili zao na nyongeza za mishahara kwa wakati.
3. mazingira kwa wafanya biashara yalikua wezeshi.
4. Alijenga barabara za lami kwa kilomita nyingi zaidi ya raisi mwinginw yeyote tz.
5. Aliruhusu bunge, na watu wakosoane kwa hoja. Hatukuona mambo ya kutekana au kumiminiana risasi km alivyomiminiwa lisu.
6. Alisaidia watoto wa maskn kupata elimu angalau mpaka kidato cha 4 kwa wingi. Hili kwa kujenga shule za kata na kuendeleza zilizopo kwa wingi. Haijawahi kutokea.
7. Wawekezaji waliongezeka nchini.
8. Hakuwa mtu wa ukabila na ukanda alihudumia nchi yetu kwa usawa. Hakuweka kwao mbele kama huyo mtu wenu.
9. Aliweka mipango mizuri ila jiwe akaja kuiharibu.
10. Uwanja wa ndege wa JKN alianza kuupanua na kuuboresha yeye, daraja la kigamboni nk alitekeleza bila kupiga kelele wala kujimwambafai.

Nyongeza.
11. Aliendeleza yaliyoachwa mezani na mtangulizi wake kwa weledi hadi tukafikia uchumi wa kati kwa maono ya mkapa ambayo kikwete nayeye aliyaendeleza.
12. Vyuo vilijengwa vingi watanzania wakasoma.
13. Alianza kusambaza umeme vijijini.
14. Aliboresha mahusiano na nchi zinazotuzunguka kwa faida ya kibiashara.
15. Hakuwa mshamba wa madaraka.
16. Hakutaka chalinze iwe mkoa.
17. Uongozi wake uliplan fly over ya ubungo, madaraja, na reli ya kisasa.
18. Aliboresha afya mfano ujenzi wa hospital ya mloganzila nk.
19. Aliheshimu taaluma za watu katika utendaji wake.
20. Haja wahi kuwa na mashaka katika utendaji wake. Sio yule wa mm nilosukumiwa tu, nilijaribu nikasukumiwa.

Haya lete legacy zako hapo chini
 
Dogo Rukwa barabara ya Kutoka Matai kwenda Kasanga KM 60 na zaidi, barabara za Dar kwasasa mnazurura zimejengwa Kwa wingi wakati wa JPM, barabara ya Mpanda Tabora, kamalizia Barabara ya Itigi-Tabora, Chunya Makongorosi, Songea-Mbinga-Mbambay, Biharamulo-Muleba, Mwigumbi-Bariadi-Lamadi, Bunda-Kisorya (najua haijaisha kipande Fulani), Kujenga upya Barabara ya Mafinga-Makambako-Igawa, Dodoma-Babati kamalizia yeye, nk wakati mwingine tusiongee kuona hakuna kilichofanyika,
Wewe ni mpumbavu hakuna unachojua..

Barabara zote ukiingia website ya Tanroads utaona mwaka ambao zilianza kujengwa..

Barabara ya Sumbawanga Kasanga imeanza kujengwa mwaka 2012 na imemalizika 2020 na bado serikali inadaiwa..

Nataka barabara mpya uniambie kwa mkoa wa Rukwa iliyojengwa na Magufuli maana SSH ameanza ujenzi wa barabara mpya ya Matai-Kasesya border,Ntendo-Muze-Kilyamatundu na barabara ya Laela-Kizombwe achana na za Tarura..

Chunya-Makongolosi bado haijakamilika, barabara zote ulizozitaja kaja kuzimalizia alikuta zinaendelea na ujenzi..

Nataka barabara mpya ambazo zilianzishwa 2015 na zimemalizika,ukiacha barabara iliyozinduliwa juzi na Rais Samia
 
Ndio nimeumia mnoo maana mtu aliyevuruga mpango wa Ujenzi barabara alikuwa Magufuli..

Alihamisha bajeti ya barabara ikahamia kwenye reli na sgr,miaka 6 ya Magufuli kajenga chini ya km2,000 za lami wakati Tulikuwa tunajenga wastani WA km 2500-3000 kwa miaka 5..

Hao hata walie au wapige sarakasi hakuna kitakachobadilika kwa sababu pesa hazitoshi..

Hayo ndio matokeo ya kuwa na mtu asiye na akili.Binafsi ninakereka Sana na Mwendazake kwa sababu aliharibu mambo mengi mno..

Mfano mkoa wa Songwe alijenga km 50 tuu kwa miaka yote 6,Rukwa hata km 1 hakuna,Katavi ndio alijenga km 390 kwa sababu Waziri wa Ujenzi alikuwa wa huko ndio hiyo barabara Rais alizindua juzi..

Kigoma hakuna, barabara zimeanza kujengwa mwaka juzi baada ya mkopo wa

Yaani kiufupi hakuna Mkoa ambao barabara zilijengwa zaidi ya km 100 kwa miaka 6..Mwaka wa kwanza wa Samia karibu pesa yote ya Wizara ya ujenzi imelipa madeni ya wakandarasi..

Mwaka huu ndio pengine barabara zitaanza kujengwa kwa angalau Kwa speed ya awali.
Acha uongo ewe Nyumbu org. Barabara ya Tunduma Sumbawanga na Sumbawanga kibaoni ilijengwa Wakati baba yako akiwa Rais?
 
Acha uongo ewe Nyumbu org. Barabara ya Tunduma Sumbawanga na Sumbawanga kibaoni ilijengwa Wakati baba yako akiwa Rais?
Baba yangu gani? Uongo upi wewe fala? Hakuna unachoweza niambia kuanzia Iringa,Mbeya,Songwe,Rukwa na Katavi huku ni maeneo yangu ya kujidai na ni nyumbani..

Nakwambia hivi barabara ya Tunduma Sumbawanga hadi mpanda imejengwa kwa ufadhili wa USAid chini ya MCC enzi za JK na ilikamlika 2014/15 ..

Ropoka jambo jingine
 
Legacy ya mpumbavu yule itafutika automatically..

Nilikuuliza hapa nipe km za barabara alizojenga Mwendazake huna,kama hujui kachukue bajeti ya mwisho ya mwaka 2020 ina summary ya hizo uone uozo alioufanya..

Yule mtu wenu alikuwa hovyo Sana ,alikuwa anazindua barabara zilizokamilika toka 2014 mfano barabara ya Iringa -Dodoma, Sumbawanga-Tunduma nk..

Nchi hii Barabara alijenga Kikwete.
Huna akili kabisa. Unatukana wafu upate nini?
 
Back
Top Bottom