Ujenzi Bandari ya Bagamoyo: Aliyemshauri vibaya Rais Magufuli ni nani?

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
14,190
21,324
Habari wakuu

Leo spika wa bunge Ndugai kasema Hayati Magufuli alishauriwa vibaya kuhusu kujengwa kwa bandari ya Bagamoyo na bunge linataka kupendekeza ikiwezekana bandali ijengwe tu.

Sasa hapa napata kigugumizi hao washauri wa Magufuli waliompotosha Magufuli ni akina nani?

Mimi binafsi nina wasiwasi na mkalimani aliyekuwa anamtafsiria huo mkataba Hatati Magufuli, huenda ndie alimshauri na kumtafsiria vibaya mlolongo mzima wa mkataba huo.

Naamini huo mkataba haukuwekwa hadharani kujadiliana sasa aliyemtafasiria akampoteza ...

Kwani kuna mtu aliyeuona huo mkataba? Wabunge je?

Uzi tayari
 
ikijengwa na ika kamilika hii bandari ya bagamoyo ipo siku Tuta mkumbuka JPM....
JPM alikataa yale masharti yaliyo kuwepo baada ya kuona ni unyonyaji ulio kidhiri....
Ndungai toka mwanzo alitaka hii bandari ijengwe....
Lazima uangalia kuwa hapa kuna kitu..

Ila sawa Wa afrika Ku uzwa tumesha zoea
 
Wekeni hadharani mktaba huo ujadiliwe na tanuru la fikra kisha majibu watayapata kwa uamuzi ulio sahihi.
 
Baada ya mwaka tu tutamkumbuka sana JPM, mafisadi wanaanza kurudi kwa kasi ya ajabu, JK is behind huu upuuzi wote, waweke mkataba wazi kama kweli una manufaa kwetu. SSH ni loudspeaker tu, nyaya zinatoka hukoooo, huyu ndio atakuwa Rais dhaifu na wa hovyo kuwahi kutokea Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…