moneytalk
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 7,701
- 16,418
nawezaje kulala sasa bila kupata kiburudishoHulali my dear?
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
nawezaje kulala sasa bila kupata kiburudishoHulali my dear?
Hahahahaha lol
Sijambo mrembo uhali gani?
uwe unaniita bwana hata kama ni saa kumi usiku niamsheHahahahaha lol
unatabia mbaya unajuaSijambo mrembo uhali gani?
KAULI YA MWISHO YA RAISI KABLA YA KIFO
U-97
MTUNZI :SIMGANOJR
SEHEMU YA 21
MAWASILIANO 0687151346
ILIPOISHIA
“ luang shu ???,kama ni mtoto wa waziri itakuwa ngumu kumzuia kufanya biashara hapa nchini “.
“ ni kweli kabisa , lakini swala kubwa Zaidi ni kwamba kiwanda anachotaka kutumia na ambacho amepewa ni cha marehemu bruno lamberk kutoka kurasini na kasema ana nyaraka zte zinazomuwezesha kukichukua kiwanda hicho na kukiendeleza kihalali katika kusuka mitambo yake ya 5G.
“unataka kusema nini kiwanda hiki si kilikuwa kipo chini ya mahakama mpaka pale mwenyewe atakapo tokea inakiuwaje akawa na nyaraka hizo ?”.
“ hilo ndio swala ambalo mpaka sasa sijajua , ila kwa taarifa nilionayo nikwamba kapitia vipengele vyte vya sheria na mahakama nidio ilioidhinisha kwa bwana luang shu kutumia kiwanda hicho “.
Patrick alijikuta akitetemeka kwani swala hilo hakulitegemea kabisa , kiwanda hicho alikuwa akikitegemea mno na aliamini katika kukitumia kiwanda hicho angeweza kupata siri zote za kitechnolojia zilizokuwa zikitumiwa na bwana bruno , hivyo alimuomba baba yake amuwezeshe kutumia kiwanda hicho lakini jibu alilopewa ilikuwa ni kusubiri mchakato wa mahakama uishe, sasa leo hii anasikia kuwa kiwanda kishamilikishwa kihalali kwa mtu mwingine .
“f***ckk , ngoja niongee na baba huenda hajui swala hili “ aliongea Patrick huku akionesha kuwa na hasira sana na swala hilo kwani alikuwa ameguswa penyewe
INAENDELEA SEHEMU YA 21.
WIKI MOJA NYUMA
Ndani ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu nyerere ilitua ndege ya shirika la ATCL na moja ya abiria alietoka katika ndege hio alikuwa ni bwana mmoja hivi aliekuwa kijana kabisa kwani mwili wake haukuwa mnene wala mwembaba ila bwana huyu alionekana kuwa ni mtu anaefanya mazoezi , bwana huyu baada ya kukaguliwa na kuonyesha passport yake alitoka mpaka sehemu ya kuchukulia mizigo na alichukua begi lake na kutoka kabisa nje ya uwanja , huyu bwana alikuwa ni mchina kabisa kwani rangi yake na hata sura yake na ongea yake ilikuwa ikifanana kabisa za wachina .
Baada ya kutoka kabisa nje ya uwanja aliona mwanamama mmoja mweupe alievalia wigi mweupe, umri wake ulikuwa ni makadirio ya miaka 40 kwenda 5 hivi .
“ miss Rebecca “ alitamka bwana huyu maneno hayo kwa lafudhi yake ya kichina .
“ luang shu you are welcome in Tanzania , I think its your first time in this country “
“ karibu sana Tanzania nafikiri ni mara yako ya kwanza kufika katika taifa hili “
“its true rebbecca and just by looking I can tell Tanzania is a very beutifull nation .”
“ ni kweli Rebecca lakini kwa kuangalia tu naweza sema Tanzania ni moja ya mataifa mazuri sana “. Rebecca alimuongoza bwana huyu mpaka kufikia kwenye gari moja aina ya AUD A3 SEDANI ilioneka imetumika lakini uzuri wake haukupotea .
“ baada ya kutoka pale bwana huyu alipelekwa moja kwa moja mpaka hoteli ya golden tulip iliokuwa ikipatikana msasani pembeni ya barabara ya seokoe toure drive , basi gari ile iliingizwa kwenye moja ya maegesho yaliokuwepo ndani ya hoteli hio na Rebecca alitoa begi la bwana luang shu na kisha waliongozana kuingia ndani ya hoteli hio .
Rebecca alienda mpaka mapokezi na kisha alichukua kadi kwani tayari alikuwa ashabook chumba , na waliongozana na bwana huyo mpaka kwenye chumba chake na wote waliingia ndani .
“ thank you rebbecca “ aliongea luang shu .
“ “ I think now you have to rest , tomorrow I will come with a lawyer for the purpose of reviewing the contract and steps to take to get the factory “.
“ Nafikiri unapaswa kupumzika sasa , kesho nitakuja na mwanasheria kwa ajili ya kupitia mkataba na hatua za kuchukua kupata kiwanda “
“Okey rebbecca”
Kesho yake ilivyofika rebbecca alifika hotelini hapo akiwa ametangilizana na bwana mmoja ambae alikuwa na ndevu nyingi huku mkononi akiwa amebeba briefcase , , walipita mapokezi na moja kwa moja walifika kwenye chumba cha luang shu na kugonga na bwana huyu alionekana alikuwa tayari ashaamka kwani alikuwa amebadilisha mavazi tayari na kuwa nadhifu .
“ hellow Rebecca morning “ aliongea luang shun a kuwakaribisha .
“ luang shu as I saidi yerstarday I wiil bring lawyer , this is mr juma bakari he is lawyer , juma this is luang shu son of the chinese interior minister and he is here for investing in telecommunication business but as I mentioned , years ago they signed a contract with bruno lamberk for the purchase of an existing factory in kurasini .
“ luang shu kama nilivyokuambia jana kwamba nitamleta mwanasheria , huyu ni bwana juma bakari ni mwanasheria , juma huyu ni luang shu mtoto wa waziri wa mambo ya ndani wa china yupo nchini kwa ajili ya kuwekeza katika maswala ya biashara ya mawasiliano , na kama nilivyosema kwamba kampuni ya luang shu nchini china walisaini mkataba na bruno lamberk ili kununua kiwanda kilichopo kurasini .
Basi walisalimiana na kisha bwana juma alipewa ule mkataba na aliupitia kwa umakini kubwa kwa kila kipengele .
“ hati inayo onyesha malipo yamekwisha fanyika iko wapi ?” aliuliza juma na luang shu alitoa hati ile na kumuoesha .
“ okey kwa ushahidi huu ni sawa kabisa kusema wewe ni mmiliki halali wa kiwanda kilichopo kurasini , lakini kwakuwa mali za bwana bruno mpaka sasa zipo chini ya serikali na mahakama basi kuna hatua ambazo nitapitia ili kuhakikisha unapata haki yako “ aliongea juma na kisha waliagana
Siku mbili mbele bwana luang shu alikabidhiwa rasmi kiwanda kilichopo kurasini , kiwanda ambacho kilikuwa kikihusika na utengenezaji wa vifaa vya electronics , na baada ya kupewa kiwanda hichi bwana luang sh alifata taratibu zote za kiwizara pamoja na kubadilisha jina la kiwanda hicho na kuweka wazi anataka kufanya biashara gani .
Mwana mama aziza kibwetere waziri wa viwanda alitia saini karatasi zilizowasilishwa ofisini hapo na luang shu , pamoja na Rebecca .
*****
Mara baada ya suzzane kutoka kituo cha magogoni moja kwa moja alienda mpaka ikulu na kuomba kuonana na muheshimiwa na aliruhusiwa na kuingia .
“vipi suzzane ??.
“ mheshimiwa ridhiwani kwa maelezo yake inaonekana hahusiki kabisa na kile kilichotokea pale serena ,lakini kwa maeneo aliokuwepo yananipa shaka “
“ unamaanisha nini suzzane kusema maeneo aliokuewepo , kwani ni maeneo gani aliokuwepo ?”
“ kwa maelezo ni kwamba muda wa saa moja alikuwa ndani ya U-97 cassino “ aliongea .
“ ndio kama alikuwa kwenye U 97 ulikuwa wataka kumaanisha nini hapo mpaka upatwe na shaka? “.
“ mkuu jambo ninaloliwaza, nataka kwanza kulifanyia uchunguzi nione kama ni kweli hisia zangu zipo sahihi na ndipo nitakuja kuekueleza kwa undani , lakini kama unavyo jua kuwa hatuna mamlaka ya kufanya upekuzi ndani ya U-97 swala hili linakuwa gumu kwangu , hivyo kwa ruhusa yako nataka nipate kibali cha kuingia ndani ya U- 97 CASSINO “ aliongea suzzane
“una uhakika jambo unalotaka kufanya, je litatupeleka mpaka kujua ni nani muhusika ?”
“ ndio muheshmiwa I m positive about it “
“ okey unaweza kwenda nitawasiliana na meneja wa casino na akuruhusu lakini hakikisha hakuna kibaya kinacho tokea kwenye ile casino kwani its beyond my reach “.
“ sawa mheshimiwa “ aliongea suzzane na kisha aliingia kwenye gari yake aina ya brevis na kisha alitoweka ikulu na kuelekea upanga ambako U-97 cassino ilikuwa ikipatikana , muda huo ilikuwa ni saa nane mchaana wakati akiingia eneo la casino hio , alienda mpaka mlangoni na kujitambulisha kisha aliruhusiwa kuingia .
Ebwana eeh kuna watu walikuwa wanafanya dhambi , kilichokuwa kinafanyika ndani ya casino hio ilikuwa sio mchezo , kulikuwa na kila aina ya ufuska , wadada mbali mbali walikuwa wakitembea uchi wengine walikuwa wakinyonya ‘rungu’ , kuna waliokuwa wakicheza Kamari , lakini ndani pia ya casino hilii kulikuwa na ofisi na zilionesha hizo ofisi zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kazi za kutia mikataba , kwa wale waliokuwa wakicheza Kamari mezani kulikuwa na pakti za madawa ya kulevya , mwanga uliokuwa humo ndani haukuwa tofauti na usiku , kwani ulikuwa na giza na mwanga wa taa za kuvutia za rangi , suzzane hakuwa mgeni sana ndani ya casino hii
“ nahitaji kuonana na muongoza camera wa hapa ndani “ aliongea suzzane akimwambia meneja wa casino bwana mmoja alivalia kipensi huku akiwa ameshhikilai sigara yake kubwa aina vasobranie black russians, ilikuwa ni moja ya sigara ghali sana .
Meneja yule kwa ishara alimruhusu suzzane na kwenda upande wa camera .
“ nahitaji matukio ya jumapili kwanzia muda wa saa kumi na moja jioni “ aliongea suzzane na kuonyeswa na vijana hao wa IT , alianza kuangalia watu waliokuwa wakiingia ndani ya casino hilo , alijikuta akitabasamu baad aya kuona sura aliokuwa akiitafuta , sura hii ilikuwa ni ya ridhiwani na hata miondoko yake ilikuwa ni ya kijana ridhiwani na alionekana aliingia hapo casino saa kumi na mbili kama na nusu hivi , suzzane aliendelea kuangalia baadhi ya picha na hapo kuna sura ilimvutia Zaidi aliomba waikuze , hii ilikuwa ni ya mwanaume aligongana nae ndani ya hoteli ya serena usiku wa jana yake jumapili na hata kumjibu vibaya na mtu huyu alionekana aliingia ndani ya casino hilo kwenye muda wa saa kumi na moja za jioni .
“ rudisha , peleka mbele kidogo , kuza hio picha “ aliongea suzzane na alifanyiwa kama alivyo elekezwa na hapo ndipo alipo tabasamu kwani aliona kuna mwanga., alikuwa ni ridhiwani akitoka , lakini ridhiwani huyu alikuwa akitofautiana na ridhiwani alieingia , alimuona bwana huyu akiingia kwenye gari aina ya crown yenye namba XXX za gari na ikaondoka eneo hilo .
“ alingalia watu waliotoka saa nne kamili usiku , hapo ndipo alipomshuhudia ridhiwani akitoka na mwanadada na kuondoka eneo hilo na huyu alikuwa ni ridhiwani mwenyewe “.
Aliendelea kutafuta karibia camera zote lakini kuna sura aliona mara moja tu ikiingia lakini sura hio haikutoka kabisa , huyu alikuwa ni mwanaume aliekutana nae serena hoteli .
“ okey asanteni nilichokuwa nikikitafuta nimekipata “ aliongea na kisha kuondoka .
“ yule mwanume mweusi aliekuwa akinisemesha ndio kahusika lazima , lakini nawezekanaje akawa na sura ya ridhiwani , nitajua baada ya kumtia mikononi yule “ aliongea suzzane na kisha akawasha gari lake na kwenda mpaka serena , alisimamisha gari na kisha alienda hadi mapokezi na kutaja shida yake
“ kama aliingia ndani ya ile casino na hakuonekana kutoka basi anaweza akawa ni huyo alietoka na sura ya ridhiwani , japo sijui kama jambo hili linawezekana lakini hsia zangu zinaniambia hivyo “ aliwaza muda huo akifika mapokezi .
“ nataka taarifa za mgeni chumba namba 85 aliongea suzzane na kisha bwana mmnoja wa kiume aliekuwa hapo mapokezi alitaka agome , lakini baada ya kuoneshwa kitambulisho alifanya kazi hio .
“ jina lake ni DAMIANI RABANI “.
“ DAMIANI RABANI “ aliongea suzzane na kumfanya apatwe na mshangao ,
“ nataka kwenda kwenye chumba chake, ashaondoka au yupo??”
“ taarifa hapa zinaonesha hajarudisha chumba “ aliongea kijana yule na suzzane aliomba kadi ya ziada na akapewa na kisha alielekea mpaka kwenye kile chumba , baada ya kufika kwenye mlango wa kile chumba alitoa siraha yake na akagonga mlango , lakini hakukua na majibu , alichokifanya ni kuweka ile kadi na kisha akafungua mlango na kwa tahadhari ya hali ya juu alijirusha ndani , alkini alikutana na chumba kikimchekea , kwani hakukuwa na mtu , lakini kwenye kijimeza kulikuwa na box lililotengenezwa na karatasi , aliliangalia , lakini hisia zilimwambia kulikuwa na mtu bafuni , alienda kwa tahadhari ya hali ya juu na kufungua mlango , lakini holla .
Chumba hakikuwa na mtu kabisa . alienda mpaka kwenye meza na kuchukua lile box na kulifungua
GOOD TRY SUZZANE by mzalendo
KESHOOOOOOO........
Ahsantekeshoo jioni
Kulikoni?