Ujasusi Sebuleni Kwetu

Ujasusi Sebuleni Kwetu

Hakuna shaka yoyote kwamba, Al-Qaeda ilikuwa inaongozwa na Osama bin Laden! Ni nani huyu Osama bin Laden? Ushahidi wa moja kwa moja unaopatikana kwenye vyanzo vinavyoaminika pamoja na uongozi wa Marekani kukiri (kama alivyofanya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekeni Bibi Hilary Clinton) kwamba al-Qaeda iliundwa na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na kupewa kiasi cha dola za Marekani bilioni tatu ($ 3bn/-) ili kundi hilo liendeshe vita dhidi ya Urusi (USSR) ya zamani iliyokuwa ikiikalia Afghanistan (rejea: http://www.theinsider.org, news.bbc.co.uk, na http://www.forbes.com).



Kiongozi wa Al-Qaeda alipata mafunzo yake ya kigaidi chini ya usiamizi wa CIA na Marekani ilikuwa inajua malengo ya kuanzishwa kwakwe. Marekani haikuwahi hata siku moja kumtafuta Osama bin Laden, hususan kwa tukio la mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Kama walikuwa wanamtafuta, kwanini waliiondoa familia yake nchini Marekani siku mbili tu baada ya kudai kuwa ndiye aliyeishambulia nchi hiyo?

Serikali ya George W. Bush ilifanya mpango ili watu wa ukoo wa Osama bin Laden waondolewe Marekani ili wasibughudhiwe. Machi 28, 2005, gazeti ‘Daily Time’s la Pakistan, likiripoti kutoka Washington DC., Marekani, lilidai kuwa FBI (Shirika la Upelelezi la Marekani) iliwasaidia Wasaudia kuondoka baada ya mashambulizi ya Septemba 11.”

FBI walishiriki kikamilifu kuandaa ndege kwa ajili ya makumi ya raia wa Saudia—wakiwamo ndugu wa Osama bin Laden—baada ya mashambulizi ya kigaidi ya 9/11.”

Taarifa hiyo ilichapishwa pia katika gazeti ‘New York Times’ ,‘The Times’ lilisema nyaraka ilizozipata kutoka serikalini zinaonesha kuwa mawakala wa FBI walizilinda na kuzisindikiza familia mbili za Kisaudia kuondoka Marekani, na Wasaudia wengine waliruhusiwa kuondoka bila hata kupekuliwa au kuhojiwa.

Ndege zilizowabeba raia hao wa Saudi Arabia ziliandaliwa baada ya tukio la Septemba 11 wakati kukiwa na madai kuwa kuna uhusiano na ushirika kati ya Rais George W. Bush na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na ile ya bin Laden. Gazeti ‘Edinburgh Evening News’ la Septemba 3, 2003, liliripoti hivi: “Serikali ya Marekani imeruhusu watu wa familia ya Osama bin Laden kupanda ndege na kuondoka Marekani mara baada ya shambulio la Septemba 11, pamoja na kwamba anga lote la Marekani lilikuwa limezuiwa kuruka ndege … hiyo ni pamoja na kuruhusiwa kwa ndugu wa bosi wa Al Qaeda.”

Tukijifunza mambo mengine kuhusu familia ya Bush na familia ya bin Laden huenda tukapata mwanga zaidi katika kujua mambo haya. Je, ni kweli kwamba Bush alimlinda sana Osama bin Laden huku akidai kuwa anamtafuta? Ni kweli kwamba Bush na familia ya Osama walikuwa wabia kibiashara?

Familia ya Bush ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa familia ya bin Laden, au angalau ndivyo ilivyokuwa. Kaka yake Osama, Salem bin Laden, ndiye aliyekuwa karibu zaidi na Bush kibiashara.

Salem ndiye alikuwa msimamizi wa makampuni makubwa zaidi nchini Saudi Arabia yaliyojulikana kama ‘Saudi Binladin Group’ (SBG). Hata baada ya kifo chake kilichotokea Jumapili ya Mei 29, 1988, Salem na George H. Bush walikuwa karibu sana kibiashara. Kampuni yake ilikuwa ikifanya kazi za ujenzi wa barabara, viwanda na nyumba katika maeneo mbalimbali duniani. EDWARD SNOWDEN alidai kwamba "Osama bin Laden" ni mshirika (operative) mtiifu na makini wa CIA kwa muda mrefu sasa. Anaendelea kudadavua kwamba Marekani ilipanga shambuluo la bandia la kumuua Osama kushirikiana na Pakistan Secret service na hili tukio limemkumbatia Osama na kumfanya awe salama zaidi, kwasababu kila mtu ameamini Osama ameuwawa, hivyo hakuna mtu atakayejishughulisha kumsaka.
Daah marekani haminiki kama. Mpemba
 
mambo ya intelijensia ni makubwa sana.. usimuamini mtu yeyote, jiamini wewe mwenyewe..
 
Jamaa analinga sana ni vyema akapigwa ban ya maisha. Anaanzisha mada huwa amalizi kwa sababu za kitoto tu na kusingizia mamlaka wakati si kweli.
Yani mtu asipomaliza mada anapewa ban ya maisha?

Kua mvumilivu mkuu. Hizi mada zinachukua muda mrefu sana kuandika, pamoja na akili nyingi.

Pia zinaweza kuhatarisha usalama wa mwandishi endapo atagusa maslahi ya watu.

As long as tunaipata makala bure, tuendelee kua wavumilivu!
 
Yani mtu asipomaliza mada anapewa ban ya maisha?

Kua mvumilivu mkuu. Hizi mada zinachukua muda mrefu sana kuandika, pamoja na akili nyingi.

Pia zinaweza kuhatarisha usalama wa mwandishi endapo atagusa maslahi ya watu.

As long as tunaipata makala bure, tuendelee kua wavumilivu!

Maslahi gani huyu jamaa kanjanja tu! Kwann km makala haijaisha asiilete humu!
 
Hii thread sijui nayo inataka kufa kibudu kama ile ya The Richest Man.....aka PK?????
 
Mchizi anavua samaki huku ha haaa.anawapa maji kiasi then anasepa nayo kimoja anajua mkipata kiu mtalia na kumfuata tu.
N mwandish mzur ila
 
Ndugu za ontario naziogopa knoma
Kwani hujui yule demu waje cheupe ndiye sekretari wa komando kipensi pale Jangid Plaza ?
Tangu aandike makala ya kumpigia debe Ontario kuhusu Forex nikaanza kumtilia mashaka......Sasa hivi ameleta tabia ya kukatisha kila thread hapa jukwaani ila wanafunika tu kombe km vjle kiachofanyika ni sawa tu
 
Wabongo wengine wavivu sana. Au tatizo kiingereza? Story zingine anazoleta the bold zimejaa tele mtandaoni, ukigoogle. Asipomaliza unaweza enda kuitafuta mwenyewe. Labda kwa zile chache chache

na the bold anajitolea, angekuwa analipwa sawa
 
Wabongo wengine wavivu sana. Au tatizo kiingereza? Story zingine anazoleta the bold zimejaa tele mtandaoni, ukigoogle. Asipomaliza unaweza enda kuitafuta mwenyewe. Labda kwa zile chache chache

na the bold anajitolea, angekuwa analipwa sawa


Mkuu kwani tuliandamana kumtaka aanzishe hii thread...Sasa kama kuna lililomsibu mpaka kashindwa kuendelea na thread si aje tu atuambie kama ile ya The Richest Man....tutamwelewa tu mkuu..
 
Back
Top Bottom