Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi

UTENGENEZAJI WA YOGHURT Part2

Kabla sijaenda moja kwa moja kwenye utengenezaji wa Product hii pendwa toka kwenye maziwa, nataka niwape hints ambazo ni muhimu kuzingatia ili uweze pata Yoghurt nzuri na bora.

1. Ukaguzi wa ubora wa maziwa
Ni muhimu kukagua kama maziwa uliyonunua yanakidhi ubora.
Baadhi ya ukaguzi unaohitajika kwa level ya kawaida ni kama zifuatazo.

i. Kukagua kama Maziwa uliyonunua yame chakachuliwa(Yameongezwa maji).
Tambua kwamba maziwa yakiongezwa maji huaribu ubora wake na kuathiri upatikanaji wa Yoghurt bora.

Maji hufanya maziwa kuwa mepesi na pia kusababisha yogurt kuwa nyepesi au yenye maji. Pia maji yanaweza kuwa na bacteria wengi hivyo kusababisha kutoganda kwa maziwa na kufanya yoghurt iliyo jitenga maji.

Hivyo nilazima ufanye ukaguzi ili kujua kama maziwa yako yameongezwa maji au la.

ii. Kujua kama maziwa yamesha chacha.
Maziwa yakisha anza kujichachisha yenyewe basi huwezi pata yoghurt nzuri.
Hapa unaweza kugundua kwa njia ya kawaida ya nyumbani. Chukua Kijiko cha chai chota maziwa kidogo, kama robo kijiko, then weka kijiko juu ya mshumaa unao waka. Ukiona maziwa yamejitengeneza vibonge vibonge vidogo kama vya mtindi basi maziwa yako yameharibika, hivyo hayafai kutengeneza Yoghurt.

Ukiona maziwa yako yanachemka kawaida bika kutengeneza vibonge basi maziwa yako yapo safi.

iii. Ukaguzi wa harufu na ladha.
Ni vizuri ukatumia Milango ya fahamu/sense organs kutambua ubora waaziwa. Hapa tuna angalia harufu na ladha. Kumbuka kuna maziwa mengine hukamuliwa katika hali ya uchafu au kuhifadhiwa kwenye chombo kichafu. Unakuta maziwa yana shombo ya kinyesi cha Ng'ombe. Pia maziwa wengine huweka madawa ya kienyeji ili yasiharibike.
Hivyo kwa kutumia macho, ulimi na pua unaweza kugundua utofauti huo.

TUTENGENEZE YOGHURT SASA.
Hakikisha kabla hujaanza una vitu vifuatavyo.
*Maziwa, Moto(jiko), Sufuria ya kuchemshia, mwiko wa kukorogea

*Thermometer kupimia jotoridi

*Sukari kwa ajili ya kuongeza utamu/ ingawa sio lazima

*Flavour kama vanilla, Strawbarries nk zinapatikana supermarket kwa bei nafuu, vichupa vidogo ni kama Tsh 600-1500.

*STARTER CULTURE- (Yoghurt culture contain these two symbolic bacteria Lactobacillus bulgaricus na Streptococcus Thermophillus) Hii ndio itatusaidia kugandisha maziwa yetu. Ni bacteria maalumu ambao wapo kwa wingi, kwa ajili ya kugandisha maziwa.
Hapa unaweza nunua ya kisasa. Zinapatikana ofisi ya PROMACO pale Kamata Opposite na Nakumati Supermarket , Nyerere Rd. Inauzwa 20,000 ipo kwenye Pakti, na unaweza kutumia kugandishia mpaka Lita 500 za maziwa. Kiasi utakacho tumia inategemea na kiasi cha maziwa. Ipo kama chengachenga.

Pia unaweza tumia Starter Culture ya kienyeji, nayo inatoa Yoghurt safi kabisa. Hii ni Yoghut ambayo ipo tayari. Yani unaweza nunua Yoghurt ya dukani au mtu ambae ameitengeneza.

HATUA ZA UTENGENEZAJI.
i. Chemsha maziwa kwa joto la 85-90 centigrade. Wakati unachemsha hakikisha unakoroga kila wakati ili kupata Yoghurt nzuri, na pia kuepusha kuungua chini.

Tunachemsha ili kuua Bactetia, enzymes, na virus. Pia kuongeza uzito na ladha ya yoghurt.

ii. Pooza maziwa kwa joto la 42-43 centigrade. Weka kwenye Ndoo safi iliyo safishwa kwa maji ya moto sana, ili kuuwa bacteria waliopo. Hapa ndipo unapaswa kuhakikisha maziwa yapo kwenye joto hilo la 42 au 43, ukikosea basi Hutopata Yoghurt, au yoghurt yako itachukua muda mrefu. Unaweza yapooza kwenye Dishi kubwa lenye maji baridi kushusha ile Temperature 90 centigrade hadi 42-43centigrade. Yakisha fikia joto hili 42 au 43 centigrade unayaondoa.

Tunapooza kwa hiyo temperature ili kuwezesha culture tutakayo iweka waweze kugandisha vizuri . Kumbuka Starter culture ina bacteria maalumu kwa kugandisha maziwa, na joto hilo ndio hufanya kazi vizuri kwa kuitafuna ile sukari ya maziwa na kufanya maziwa kuganda (Rejea maelezo ya nyuma).

iii. Weka Starter Culture 2% ya maziwa. Hapa nazungumzia Starter culture ya kienyeji, yani yoghut iliyotayari ndio unachanganya na haya maziwa kwa 2%. Yani kama
maziwa yako ni lita 10 (10,000 ml) (ndoo ndogo) basi unapaswa kuweka Culrture kile kikombe kidogo cha chai ambacho ni 200ml (0.2L), hala ndio 2%inapatikana. Culture ndio hutumika kugandisha maziwa kwa haraka (3hrs).
Funika maziwa kwa saa 3 yangande.

iv. Koroga na yavundike kwa joto la 42 au 43 centigrade

v. Baada ya masaa matatu(3hrs) yataganda, hivyo haraka sana yaweke kwenye freezer au Friji lenye ubaridi mkali. Lengo ni kuwapooza wale bacteria ili wasifanye kazi. Kwa joto la 0 hadi 4 centigrade bacteria hawa hupooza na kushindwa kuendelwa kuchachusha maziwa. Hapa tunafanya hivi ili Yoghurt yetu isiwe na uchachu mkali. Hii Process ndo tunaita Rippening/ kuiva kwa Yoghutt. Iweke kwenye Friza kwa muda wa masaaa nane (8hrs).

vii. Baada ya masaa 8, Ondoa Yoghut yako kwenye friza. Hapa unaweza kuondoa kiasi kingine cha Cultute kwa matumizi ya kugandisha maziwa wengine baadae. Hakikisha chombo cha kuhifadhia culture ni sterile au kisafi.

vi. Unaweza weka sukari na flavour. Sukari ni 4% ya maziwa. na Flavour ni kijiko kidogo tu.

Vii. YOGHURT YAKO IPO TAYARI.
Hapa unaweza kuiuza unavyotaka, kama ni kwa kupak kwenye nylon plastic au cup ni sawa tu. Au ukiamua kuuza kwa glass ni sawa pia.

NOTE MUHIMU.
Yogurt ni Cold chain Product, ni bidhaa inayo hitaji ubaridi muda wote. Hivyo unapaswa kuiweka kwenye Friji, ila isigande kuwa barafu. Usipo iweka kwenye ubaridi basi kumbuka wale culture wataendelea kuchachusha na kuifanya mtindi kuwa mchachu zaidi.

VITU VINAVYOSABABISHA YOGHURT ISIGANDE.
1. Starter Culture imechoka/ yani hapa culture imetumika kwenye chain ndefu sana. Pia culture kuvamiwa na virus (Bacteriophage)

2. Maziwa yametoka kwenye Ng'ombe mgonjwa au ambae yupo kwenye dozi za dawa. Dawa zile huingia kwenye maziwa yake hivyo huja kuua culture.

3. Vyombo vimesafishwa ka sabuni ya Unga. Sabuni ya Unga huwa haiondoki kwa haraka, hivyo huuwa Culture. Hivyo ni vizuri ukatumia sabuni ya kipande kwenyenuoshaji.

4. Joto la kughandisha halipo sahihi

FAIDA ZA YOGHURT.
i. Yoghurt ina Calcium nyingi hivyo husaidia mifupa kuwa imara

ii. Umeng'enywaji wake ni rahisi mwilini. Pia husababisha chakula kumeng'enywa kwa haraka. Kama umeshiba sana kunywa Yoghurt isiyo na sukari

iii. Ni nzuri kwa watu ambao wanatatizo la LACTOSE INTOLERANCE. Watu ambao hawanywi maziwa fresh

iv. Inapambana na bacteria kibao mwilini hivyo kuepusha magonjwa ya kuharisha na kuumwa tumbo

v. Inapunguza vitambi, kuondoa kichefuchefu.

vi. Protein iliyopo kwenye yoghurt inasaidia kuongeza kuvu za kiumee


TUNYWE YOGHURY KWA FAIDA YA AFYA ZETU.

Nakaribishwa maswali.

Somo litakalo fuata ni Utengenezajinwa Mtindi(Cultured milk au maziwa Mala.)

Karibuni
Asante sana kiongozi kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya watu.
 
Back
Top Bottom