Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi

Habari Wana Jukwaa.
Karibu katika Andiko hili ambalo nitaeleza biashara hii kinaga ubaga.

Tutaanza na topic hizi:-
1. Jinsi ya kuanzisha kiwanda kidogo cha Maziwa

2. Jinsi ya Kutengeneza Yoghurt

3. Jisni ya kutengeneza Mtindi

4. Changamoto ya biashara hii

5. Vya kuzingatia kukidhi mamlaka hiziTBS, TFDA, TRA, Kwa uwekezaji mkubwa kidogo.

************************************
Nimerudi wakuu.
Kwanza niwaombe radhi kwa kuwakalisha kwa mda mrefu kusubiri mada hii. Kuna mambo ya kisafari yaliingiliana hapa kati hivyo kushindwa kuwaletea mada hii.

Kama nilivyo ainisha mada yangu, ambayo nimeifanyia editing ili iwe rahisi kueleweka hata kwa watu wa kawaida. Hivyo nitaanza kwa mtiririko wa namba kama ilivyo kwenye mada yangu.

N.B Naomba mnivumilie katika matumizi ya lugha, kwani kuna baadhi ya maneno nalazimika kutumia kingereza ili kueleweka zaidi.

1. JINSI YA KUANZISHA KIWANDA KIDOGO CHA MAZIWA (DAIRY IINDUSTRY)

i. Utangulizi.
Maziwa ni kimiminika kinacho zalishwa na wanyama wanaonyonyesha kwa ajili ya watoto wao. Mara nyingi maziwa ya Ng'ombe ndio hutumika kwa matumizi kwa binadamu.

Hata hivyo maziwa ya Mbuzi, Buffalo, Ngamia pia hutumika kama chakula kwa binadamu katika sehemu nyingine.

Maziwa yana virutubisho vingi sana katika afya zetu. Maziwa ni moja ya vyakula vichache ambavyo hujulikana kama. complete food yaani chakula kilicho kamilika.

Chakula kilicho kamilika ni chakula chenye virutubisho vyote sita ambavyo tunavijua.
Maziwa yana Carbonhydrate ambayo hujulikana kama lactose(sukari ya maziwa) na hupatikana kwenye maziwa pekee.
Maziwa yana protein, mafuta, vitamini, madini, maji n.k

Maziwa yanaweza kutengeneza Products(mazao) mengi yakisindikwa kama maziwa fresh, yoghurt, mtindi, samli, jibini, siagi, ice cream, maziwa ya unga (dried milk). n.k

ii. Composition ya maziwa.
Asilimia kubwa ya maziwa ni maji (88%), lactose 4%, protin 4%, mafuta 3.8%, madini 0.6%, na zilizobakia ni vitamin n.k


iii. Mambo ya Muhimu ya kuzingatia kabla hujaanza kiwanda kidogo.

a)Utafiti juu ya hali ya soko
b)Upatikanaji wa malighafi (maziwa)
c)Mpango fedha (Mtaji)
d) Vifaa vinavyo hitajika
e)Changamoto ya biashara hii (hii nitaeleza mwishoni mwa mada hii).

a) UTAFITI JUU YA MASOKO
i. Bidhaa zipi zinahitajika katika eleo husika
Ni vema ukafahamu bidhaa zipi zinapendwa na wateja, je ni mtindi? yogurt? siagi? cheese?

ii. Nani watakuwa wateja wako
Je hapa umewalenga kundi gani? wanafunzi? watu wa maofisini? watu wa majumbani? supermarkets? madukanii?

iii. Kiasi gani kinahitajika
Je kiasi gani kinahitajika sokoni?

iv. Bei zitakazo kubalika
Je bei gani ni ya wastani kwa wateja wako? Utakuwa na bei tofauti kutokana na ainabya wateja na soko? bei yako inaendana na washindani wako?

v. Aina ya vifungashio
Umelenga kutumia vifungashio vipi, vya nylon? vikombe vya plastic? chupa? Je zitakuwa labelled?

vi. Kuelewa bidhaa zilizopo madukani na washindani wako
Unawashindani wangapi sokoni? Nguvy zao ninini? unanini kipya kuingia sokoni?


b) UPATIKANAJI WA MALIGHAFI (MAZIWA)
i. Upatikanaji wa maziwa katika eneo husika.
Je wewe ndio utakua mfugaji? Utanunua maziwa? Kama utanunua, bei ni rafiki ukiingia sokoni?

d) VIFAA VINAVYO HITAJIKA
i. Vifaa vya kuhakiki ubora wa maziwa
Msindikaji mdogo wa maziwa lazima awe na vifaa hivi ili kuhakiki ubora wa maziwa

*Lactometer- Hiki kifaa hutumika kwa ajili ya kupimia uzito(density) au Specific gravity. Hii inatuonesha kama maziwa yamechakachuliwa, yaani kama yamewekwa maji. Hapa nawazungumzia wale ambao hununua kwa wafugaji. Zipo Maduka ya vifaa vya maabara
112a4c231e14f41ceae3549dd1dcb072.jpg
Huuzwa Tsh 10,000-15,000/=

* Alcohol gun- Kwa ajili ya kupimia kama maziwa yameharibika. Hapa test tube kama mbili zinatosha. Alcohol ya 70%,.

*Kipima joto(Thermometer) yenye uwezo wa kupima nyuzi joto 0-100 Centigrade. Hakikisha kipimia ni Centigrade na sio Fahrenheit. InauzwaTsh 6000--10,000/= Zipo Maduka ya vifaa vya maabara

*Acidity kit-kifaa hiki kwa ajili ya kupimia ongezeko la asidi

*Mshumaa- Njia ya kienyeji kutambua kama maziwa yameharibika

iii. Vifaa vya Kusindikia maziwa

*Heat Source- Chanzo za moto ambao utatumia kuchemshia maziwa. Je ni Gesi, mkaa, Umeme, kuni?

*Cooling vat-Kipoozeo cha maziwa baada ya kuchemka. Linaweza kuwa ni beseni kubwa au pipa lililokatwa.

*Incubator- hapa sizungumzii incubator kama zile za kutotolea mayai. Bali ni chemba yenye kuweza kuhakikisha nyuzi joto(Temperature) haishuki wala kupanda wakati wa kusindika maziwa. Kwa wasindikaji wadogo wanaweza tumia maji ya vuguvugu kwenye baseni kubwa ambayo maziwa yatawekwa hapo kwa muda maalumu hadi yagande. Nitaeleza huko mbeleni, kwani hii hutegemea na aina gani ya product unataka kutengeneza.

*Vifaa vya kubebea maziwa toka kwa mfugaji hadi kiwandani. Kuna zile aluminiam Can ambazo zina ujazo wa kuanzia lita 20,30,40,50,70,100. Unaweza pia kutumia madumu ila inabidi uwe msafi na ujue jinsi ya kuyasafisha mara kwa mara.

* Freezer- Hii ni lazima uwe nayo, ukubwa wake itategemea unataka kuzalisha kiasi gani. Freezer hutumika kupoozea maziwa baada ya kuganda. Naomba utofautishe Freezer na friji la kawaida, freezer ni lile linalo gandisha maji kwa ubaridi mkali kwa muda mfupi. Pia hutumika kuhifadhi maziwa ambayo yametoka kwa Ng'ombe yasiharibike.

*Vifungashio-kwa wanao anza wanaweza anza na mifuko ya plasti ambayo ipo labelled kama ile ya Tanga Fresh. Nitawaeleza zinapo patikana

* Plastic sealer- Hii nimashine ya kuvungia vifungashio vya nylon, kuna ya mkono ambayo kuna ya 45,000/, 50,000 , 75,000= Hutumia umeme.Hutofautiana kutokana na ukubwa na aina ya kampuni. Zipo soko kuu la k.koo

*Cool boxes- Kwa ajili ya usambazaji wa maziwa

* Cream separator- Kwa ajili ya kutenganisha cream(fat/mafuta) kwenye maziwa. Cream itakusaidia kutengeneza siagi, samli, ice cream

* Sufuria aina mbali mbali kwa ajili ya kuchemsha

*Mwiko/Plunger/ kipekecho kwa kukorogea

*Chujio na kitambaa vya kuchujia maziwa

*Detergents/Sabuni za kufanyia usafi vifaa na eneo la usindikaji

*Visu

*cold room

*Butter churn- kifaa kwa ajili ya utengenezaji wa siagi

*Butter mold-kinachofyatulia butter(siagi)

*Chombo cha kusafiria/kusambaza products zako, gari? Pikipiki za tairi tatu(guta), pikipiki, baiskeli?


c) MPANGO FEDHA/MTAJI.
i. Mtaji wa kuanzia.
Kwa kiwanda kidogo ambacho kitakuwa na uwezo wa kusindika lita 500 kwa siku inakuhitaji kama Tsh 5,000,000 hapa namanisha pamoja na pikipiki.

Ila kama unataka uanze kibishi, basi hata milion tatu inatosha.

ii. Utunzaji kumbukumbu za mauzo, matumizi na mapato

Note. Kiwanda hiki kinauwezo wa kuendeshwa na mtu yeyote wa kawaida ambae anajua kusoma na kuandika.

Kinacho hitajika ni kufuatilia maelekezo kwa umakini.

Nitarudi kuendelea na somo

Karibu kwa maswali

2.JINSI YA KUTENGENEZA YOGURT/ YOGHURT Part 1

JINSI YA KUTENGENEZA YOGHURT Part 2

Bandiko la Mtindi hilo hapa

Ujasiriamali 2: Usindikaji wa Mtindi (Sour Milk) - JamiiForums

Mawasiliano: 0737212132
Naweza pata namba yako Mkuu pm me Tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahitaji hizi package za uht
Hizi sijajua upatikanaji wake lakini nahisi aliExpress inaweza kuwa suruhu ya hili tatizo lako.

Kwani hicho utakachoweka unakuwa umekizalisha under UHT parameters au unataka uzibadilishie matumizi.
 
Swali zuri kaka, na unaonekana upo makini.

Kwanza kabisa katika maeneo ya joto kama Dar, Tanga mjini, Moro mjini kwa muda wa masaa 3 kwa joto hilo maziwa hayawezi shuka kwaraka sana, labda iwe ni kipindi cha baridi. Hivyo unaweza changanya Culture na maziwa yako kwa hilo joto na yakaganda ndani ya masaa 3 bila hilo joto kushuka.

Kwa zile sehemu zenye ubaridi kama Lushoto, Iringa, Makambako, Mbeyya Part 1 ya somo la yoghurt nilosema unapaswa kuwa na incubator. Hiki ni chombo ambacho kina maintain temperature constant ukisha iseti. Zinatofautiana ukubwa. Kwa matumizi ya kibiashara unapaswa unjengewe chamber au ununue zile kubwa ambazo utaweka culture, maziwa, sukari, flavour kwenye package una seal then unaweka kwenye incubator, baada ya masaa 3 unapunguza temperature mpk 0-4.

Lkn kwa mtaji midogo najua ni ngumu kuimudu hiyo incubator, hivyo unapaswa kufanya kama ifuatavyo kwa sehem zenye baridi

1. Chemsha maji mpaka temperature 43
.2. Weka maji hayo kwenye chombo kikubwa ambacho kitaweza beba chombo ulichoweka maziwa na culture.
3. kazi yako itakuwa kuhakikisha maji ya nje temperature yake haishuki chini ya hapo kwa kuongeza ya moto pale inalotokea temperature inashuka.

N.B Pia niwakumbushe kufunika maziwa hayo baada ya kuweka culture, kwani hewa haipaswi kuingia ndani, na pia joto lisitoke nje.

Karibu
Safi,sasa ikitokea joto limeshuka halafu nikaongeza maji ili kufanya joto liendelee kuwa 42 na bahati mbaya joto likazidi 42, hao bacteria humo ndani si watatafutana mkuu? (wataipata pata fresh ya shamba na zoezi lote likaishia hapo)
 
Back
Top Bottom