SoC01 Ujasiriamali na Changamoto kwa vijana wa Kitanzania

Stories of Change - 2021 Competition
Apr 6, 2020
8
10
UJASIRIAMALI ni mchakato endelevu unao ambatana na Imani juu ya kujikomoa kiuchumi kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya juu zaidi. Nchi nyingi duniani hasa mataifa makubwa toka miaka ya 1960 zimepata kuendelea kutokana na sera tofauti tofauti zilizoanzishwa na serikali zao juu ya UJASIRIAMALI Kama nyenzo ya kuinua uchumi wa nchi na kuwekwa kipaumbele Kama sera au kaulimbiu ya nchi.

Hivyo kwa nchi yetu takribani zaidi ya miaka 50 mpaka sasa toka tupate Uhuru sera ya UJASIRIAMALI imekuwa haina kipaumbele na imekuwa Kama praystation kwasababu serikali haina njia maalumu ya kuboresha njia na fursa za UJASIRIAMALI Kama walivyofanya nchi zingine na kuwa chachu ya kuboresha uchumi wa nchi.

Changamoto kubwa ambazo sekta hii inaikumba hasa ni:

1: Ukosefu wa mitaji ambayo wajasiriamali inaweza kuwafanya wakawa committed na biashara zao bila uoga wowote katika shughuli zao.

2: Mazingira yasiyo rafiki katika ufanyaji wa biashara zao mfano mzuri maeneo ya Malimbe Mwanza wajasiriamali wengi ni WANAFUNZI lakini biashara zao sio rafiki kwa maana ya mazingira sio rafiki kuendesha shughuli zao hivyo husababisha wajasiriamali wengi kushindwa kumudu hali tofauti tofauti na kuacha shughuli zao.

3: Ukosefu wa Sera rafiki au persuasive policies ambazo zitawafanya wajasiriamali kuwa mstari wa mbele katika kujituma kwenye shughuli zao na kupiga hatua kiuchumi binafsi na hata taifa kwa ujumla.

Nini kifanyike ili kuondoa changamoto na kufanya UJASIRIAMALI kuwa first priority kwa serikali katika kuhakikisha inakuwa tegemezi la pato au ukuaji wa uchumi wa nchi?

1) Serikali inatakiwa kuunda taasisi/tume maalumu ya kiserikali itakayokua inatoa elimu, semina na ujuzi na njia sahihi za kupata mitaji kwa wajasiriamali ili kufanikisha UJASIRIAMALI kuwa njia mojawapo ya kitega uchumi katika sekta zingine.

2) Serikali kwa kushirikiana na sekta/taasisi binafsi inatakiwa kuunda SERA SHIRIKISHI kwa nchi nzima ili kuboost wajasiriamali kujiona wanathaminika na wanapewa kipaumbele Kama sekta zingine za uchumi hii itasaidia kuwapa wajasiriamali morale ya kufanya kazi na kujituma kwa Dhati katika shughuli zao.

3) Kuundwa kwa Platforms maalumu mfano inaweza Kuundwa NATIONAL ENTERPENEURSHIP PLATFORM au NATIONAL ENTERPENEURSHIP COMPETITION kwa lengo la kuinua,kukuza na kuboresha ubunifu wa wajasiriamali. Maana jamii ya watanzania wengi wanafanya UJASIRIAMALI wa kuiga yaani wajasiriamali waigaji na sio kuwa wajasiriamali wabunifu na watafiti.

Mwisho vijana ni taifa la kesho hivyo hatuwezi kuwa taifa la kesho Kama hatuna njia maalumu zitakazotufanya tuwe Bora na wakomavu
 
Asante ndugu Emanuel. Wajasiriamali waigaji ni Aina ya ujasiriamali ambao hauna tija katika jamii maana hakutakua na jipya katika mashindano au soko la kibiashara, watu au jamii ya sasa inataka vitu vipya na vya kisasa(ubunifu katika utendaji) na sio kucopy vya wengine na kufanya vyako Kwaiyo ujasiriamali wa kibunifu na utafiti ni moja ya kuleta ushindani (competitive advantage) katika misingi ya kijasiriamali na kuweza kua wa tofauti na wengine.
 
Nakubalina na wewe mletaji ndipo. Ila kutokana na maelezo ya mwandishi wa zero to one na ambaye ni mwanzilishi wa PayPal akisema kuna kitu kinaitwa 0 to 1 na 1 to n. Ambayo 0 to 1 ni ugunduzi wa vitu vipya na 1 to n ni kuiga au kuboresha ambao pia ni ujasiriamali
 
Shukurani mkuu kwa maelezo nakutakia ushindi mwema wa 5m
 
Nakubalina na wewe mletaji ndipo. Ila kutokana na maelezo ya mwandishi wa zero to one na ambaye ni mwanzilishi wa PayPal akisema kuna kitu kinaitwa 0 to 1 na 1 to n. Ambayo 0 to 1 ni ugunduzi wa vitu vipya na 1 to n ni kuiga au kuboresha ambao pia ni ujasiriamali
Shukrani Sana ndugu Batholomeo Batho kwa maelezo yako mazuri lakini siku zote huwezi fanya biashara au ujasiriamali wa kuiga na ukategemea mafanikio na ndo Mana wengi wanaoiga wanashindwa kusonga mbele sababu moja bidhaa au huduma ni ileile hakuna utofauti wowote Kati ya mjasiriamali wa mwanzo na mpya ambaye ameiga kwa wakwanza,hivyo moja atafail sababu ya customer Competition na ni vigumu kwa mteja kumuama mtoa huduma angali ashazoea na hakuna utofauti wa huduma, hivyo Bora mjasiriamali anayeiga na kuboresha naye atutamuita mjasiriamali muigaji uyu atakua wa Aina yake yani mtafiti amepata kujua mapungufu ya mjasiriamali wa awali na amekuja na wazo jipya la uboreshaji na uyu anaweza kua ana high competitive advantage kuliko wa kwanza anayeiga tuu.
Asante.
 
Kutafuta na ku-maintain wateja ni moja ya changamoto kubwa sana kwenye ujasiriamali.
Sahihi kabisa na ninakubaliana na wewe 100% asa kwa wajasiriamali waigaji yaani wanaokuja au kuingia kwenye ujasiriamali bila maboresho yoyote ya bidhaa au huduma au shughuli zao ni vigumu Sana kuliko mtu Atakaye ingia na maboresho au ubunifu.
 
Nielekeze sas
Bonyeza kwa kuandika hivi 👉 weka kibobo [] ndani ya hicho kiboma weka neno Spoiler kisha nje ya viboma andika maneno malizia kwa kufunga viboma [/] kwenye viboma vya kufunga andika tena neno Spoiler baada ya mkwaju / kisha uwe imelifungua hilo neno yaani [/Spoiler] hapo
Mafano
kisha andika neno unalo taka kuficha malizia kwa kuandika
.

Hapo kwenye kuandika maneno usiruke nafasi hakikisha maneno yanagusana na hivyo viboma.
 
Shukran
 
Back
Top Bottom