Mama Alfan
New Member
- Jul 4, 2023
- 1
- 2
Ujasiriamali ni stadi inayomuwezesha mtu kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kulingana na fursa zilizopo katika mazingira yake.Kuna aina nyingi za ujasiriamali kama vile kuuza mbogamboga,kutengeneza sabuni na nyinginezo nyingi.
Uzalishaji unaweza kuwa wa aina tofautitofauti pia husaidia vijana kujikwamua na shida mbalimbali pia hupelekea vijana kutokua tegemezi Kwa wengine.
ujasiriamali unapaswa kufundishwa shuleni kuanzia shule za msingi,sekondari na vyuoni ili kufanya vijana waweze kujitegemea na kupata ujuzi mbalimbali mara wanaposhindwa kuendelea na masomo yao.somo la ujasiriamali shuleni litamfanya kijana kuwa mkakamavu na hodari katika kujitafutia kipato halali.
Ujasiriamali huwaepusha vijana na makundi mbalimbali ya kiuhalifu yanayo zuka maeneo mengi,Somo hilo pia likifundishwa mashuleni linaweza kusaidia kuepukana na wingi wa watoto/vijana wasio na ajira kwasababu vijana wanaweza kujiajiri wenyewe. Wakihitimu masomo yao bila kusubiri ajira.
Somo la ujasiriamali ni Somo linaloweza kuinua uchumi wa nchi kwasababu ni Somo pana ambalo halichagui umri na halina ukomo na nisomo bunifu pia ni Somo lenye manufaa Kwa pande zote mbili na linafanya watu kujifunza zaidi kwani linaleta maendeleo yenye tija Kwa jamii husika, Mfano vijana wengi Sasa wanaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani,kama vile sabuni za maji,sabuni za miche na batiki.
Ujasiriamali ukifundishwa shuleni ni nguzo imara Kwa jamii na kizazi cha Sasa na kitasaidia vijana wengi kuepukana kutazama video mbalimbali za ngono kwenye mitandao ya kijamii na watatumia mitandao hiyo ya kijamii kutangaza fursa walizo nazo ili kujipatia wateja wa maeneo tofauti tofauti na aliyopo yeye.
Hivyo Somo la ujasiriamali ni muhimu shuleni na likifundishwa litalenga kuinua uchumi wa nchi na kuepukana na vitendo viovu vya unjaji wa amani.