Ujasiri wa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasiri wa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Apr 12, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kufuatia vikao vya CC na NEC ya CCM, nimeonelea nimpongeze JK kwa vitendo kadhaa vya kijasiri.
  1. Kumpatia nafasi ya uenezi Nape Nnauye ni kitendo cha kijasiri kwa maana Nape haivi na Ridhiwani. Ni Ridhiwani aliyemshawishi baba yake kumtosa Masauni aliyekuwa akielewana na Nape. Vile vile, Nape alimshambulia hadharani Lowassa kuhusu ujenzi wa makao makuu ya UVCCM na Lowassa akiwa mdhamini wa UVCCM akamlima kwa JK. Hivyo JK amefanya 'u-turn' kinyume na mapenzi ya mwanae.
  2. Kutamka wazi kuwa kuna mafisadi katika CCM ni ujasiri, ikizingatiwa kuwa CCM walikataa kabisa msamiati wa ufisadi hadi wakafikia hatua ya kudai fisadi ni mtu anayekwea wake za watu wakimlenga Dr. Slaa aliyeachana na Kamili na kuhusiana na Mshumbusi. Huenda lilikuwa ni fukuto moyoni mwake rais lakini hakuwa na namna ya kulitoa hadi wakati huu ulipofika.
  3. Maamuzi aliyochukua Kikwete si mawazo yake binafsi bali ni ushauri wa 'wazee'. Huyu rais wetu ana sifa ya kutoshaurika. Kitendo cha kukubali ushauri na kuutekeleza kinaonesha sasa rais amekua, na anashaurika. Huu ni ujasiri maana kinyume cha haya angeweza kuendeleza udikteta.
  4. Vile vile inaelekea Kikwete sasa hataki kuwategemea vijana kama Ridhiwani na Malisa, ambao wamekuwa wakimpelekea umbeya na badala yake anataka kutegemea vijana wenye mtazamo chanya kama January na Nape. Ikumbukwe kuwa January ni mtoto wa Yusufu Makamba hivyo kumteua bila kujali mtazamo wa waompinga baba yake ni ujasiri na alama kuwa mwana harithi dhambi za baba yake.
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  AA wapi . Anatapatapa tu. Ngoja tuone
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Some truth in here!
  iLA HIYO no 2 imenifurahisha zaidi!
  Hofu ya kupoteza utawala 2015 ni kubwa, na wanajua wazi kuwa hii si ndoto!
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  yeye msafi?
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mbona unamsifia Nape tu, na wengine Je.

  yaani unataka tukubaliane na uongo wako kuwa ni wazee akina mzee Kisumo ndiyo wamependekeza jina la Wilson Mkama, January Makamba na zakia Meghji?
   
 6. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni rahisi zaidi kwa mtu msafi kusema wengine ni wachafu hivyo kama unadhani JK sio msafi, then ametumia ujasiri mkubwa kusema wenzake kuwa wana mikono michafu maana ingekuwa rahisi zaidi kwake kuwanyamazia kimya.
   
 7. U

  Uswe JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hahahahaaaaaa
   
 8. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  angewany'ang'anya kadi za chama hao anaowaita mafisadi ndani ya chama ndo tungesema ni jasiri. Kutamka kwamba kuna mafisadi ndani ya chama sio ujasiri wowote kwa sababu alijua siku nyingi kwamba mafisadi wapo na ndio wafadhili wa chama.
   
 9. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kama mafisadi wamo ndani ya chama! Na mhe. Rais amethibitisha hilo sasa anasubiri nini dawa ni kuwatoa chamani haraka iwezekanavyo. Hii itasaidi kuwadhoofisha kabisa.
   
 10. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wasiwasi wangu ni kuwa haya tunayoyaona isiwe ni kiini macho!! ili kupisha mhemuko uliopo nchini upoe na baadaye mambo yaende km yalivyo......CCM inaubavu gani wa kutotegemea matajiri mafisadi...kwani hata ule utaratibu wa kuhamasisha wanachama kulipia kadi zao ili kutunisha mapato ya chama ulishasahauliwa....sasa chanzo cha mapato kitakuwa nini zaidi ya ruzuku?
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  wamewakorofisha wafadhili wa chama sasa tusubiri kodi kupandishwa ovyo kukifinance chama..
   
Loading...