Ujanja wa Rais Samia kwa Museveni

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
Rais wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, leo wameshiriki uzinduzi wa Shule ya awali na msingi Museveni iliyojengwa katika kijiji cha Nyabilezi, Chato mkoani Geita.

Shule hiyo imejengwa kwa gharama ya takribani Dola za Kimarekani Milioni 1.67 zilizotolewa na Rais wa Uganda kama alama ya urafiki baina ya mataifa haya mawili.

Rais Samia akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano amemuomba Rais Museveni, kuwa endapo itampendeza basi Shule hii ipate Shule Dada/Kaka huko Uganda.

UJANJA HUU.
Tunafundishwa kwamba wema hauozi, wema hulipwa kwa wema na wema ni deni.

Utekelezaji wa aliyochokiomba Rais Samia utamaanisha kurudisha fadhila, utamaanisha kulipa deni, utamaanisha Rais Samia kutenda wema kama alioutenda Museveni kwa Tanzania.

Ujanja wa deni bhana ni kulipa😂😂, Rais Samia kalipa deni.

Samia m7.jpeg
 
View attachment 2027543
Uganda wamfunge shule tangia covid
Hawana shida ya shule
 
Inapaswa hapo juu jf heading kuwe na taadhali, kuwa usitukane, usikejeli wala kumdhalilisha mtu, wengi tunajisahau kuwa watu wa rika, jinsia, na dhamana na mamlaka mbalimbali upeluzi jf, hivyo hawapendi lugha za kuudhi!
 
Unaongelea jf Tu, mbna kuna wengine wameambiwa "non sense" hadi kwenye TV ya Taifa kuliko hapa mkuu

Sent from my 5033X_EEA using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom