Ujangili wa kutisha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

JUMANNE, OCTOBA 30, 2012 04:52 NA RUTH MNKENI, DAR ES SALAAM

pg%208.jpg


Watuhumiwa waliokamatwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 2.1 wakiwa kwenye Kituo cha Kati cha Polisi Dar es Salaam jana. Nyuma yao ni baadhi ya meno hayo. Picha na Deus Mhagale.


*Meno ya tembo yakutwa yakiandaliwa kuwekwa kwenye jeneza
*Baadaye yangefunikwa kwa bendera ya taifa, polisi wakataa hongo

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia raia watatu kutoka nchini Kenya na Mtanzania mmoja, baada ya kuwakamata wakiwa na meno ya tembo 214, yenye thamani ya Sh bilioni 2.1.

Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la polisi nchini, kukamata shehena kubwa ya meno ya tembo, kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa ni majangili.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, alisema watuhumiwa hao walikamatawa juzi katika eneo la Kimara Stop-Over.

Aliwataja watuhumiwa hao, kuwa ni Polisi Simon (42), ambaye ni dereva wa daladala aina ya Costa, Charles Wainaine (41), mkazi wa Tarakea Wilaya ya Rombo na Peter Kabi, ambao wote ni Wakikuyu kutoka nchini Kenya.

"Uchunguzi wa awali, ulibaini wahalifu hawa, ni wazoefu katika matukio ya mtandao wa ujambazi, usafirishaji na umiliki wa nyara za Serikali.

"Mpango wa siri, walioutumia watuhumiwa ni kutumia gari aina ya Costa, inayoendeshwa na Polisi Simon, kwa kusafirisha... waliweka jeneza lililofunikwa bendera ya Taifa, kama wanasafirisha maiti ya mtu mashuhuri wa Serikalini.

"Lengo ni kutaka kuzubaisha vyombo vya dola au mamlaka zinazohusika...nyara hizi zingevushwa kwenda nje ya nchi, kupitia mpaka wa Tarakea Wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro," alisema Kova.

Alisema katika tukio hilo, mwanamke mmoja Leornad Kabi, alikamatwa kwa kosa la kuwashawishi askari polisi waliokamata mali hizo, ili wapokea rushwa ya Sh milioni 15 na kuahidi kuwapatia fedha nyingine siku inayofuata, kama wangewaachia.

"Tunashirikiana na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, ili kupata uzito wa thamani na uchunguzi wa kina utafanyika, ili kubaini mitandao ya wizi wa nyara za Serikali," alisema.

Alisema polisi walifanya msako, baada ya kupata taarifa kuwa, kuna nyumba inahifadhi mali za wizi, ambazo zinasadikiwa kuwa nyara za Serikali.

Alisema polisi walifika katika nyumba hiyo, ambayo alipanga Peter Kami, anayeishi na Leornad Kabi na kukuta idadi ya meno 214, ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya salpheti 12, ikiwa imefunikwa na bendera ya Taifa, pembe za ndovu 10 na na mifupa ya tembo 500.

 
Yaani ni kama Mimi na Wewe hawaonekani kama MAJANGILI wa sura za kutisha...
 
Hii ni tanzania
Meno 214 gawanya kwa mbili ni tembo 107 wameuwawa kama ni zile pembe tuu
Duh na bado walikouwa hao tembo kuna walinzi wa hifadhi na mbuga za wanyama wanaolipwa na serikali na bado idadi hiyo kubwa ya tembo wameuwawa na bado tunasema tuna askari wa wanyamapori
Hii nchi hii bana kila kiru kinawezekana mkuu nngu007
 
Last edited by a moderator:
hii ni tanzania
meno 214 gawanya kwa mbili ni tembo 107 wameuwawa kama ni zile pembe tuu
duh na bado walikouwa hao tembo kuna walinzi wa hifadhi na mbuga za wanyama wanaolipwa na serikali na bado idadi hiyo kubwa ya tembo wameuwawa na bado tunasema tuna askari wa wanyamapori
hii nchi hii bana kila kiru kinawezekana mkuu nngu007

si bora hao tembo/wanyama wanaouwawa_wanauwawa binadamu kina mwangosi,mwabulambo,..kina ulimboka,mwakyembe,mwandosya chup chup...bila kulindwa ndio itakuwa hao....hii nchi fujo kila kona.
 
Hapo badooAfrika ya Mashariki haijaja,Mtakoma ubishi-Vichwa vya watu vitapelekwa Burundi,Meno ya faru Kenya,Ngozi ya binadamu Uganda,Sasa sijui nyara za albino zitapelekwa wapi.Duuu kina Kova wa enzi hizo zijui watakuwa wa Kanda maalum ya wapi.......:pop2:Jana alinichekesha kweli qakishindwa kutumia ipad mpaka mwenzake amsaidie kuscroll down ndipo asome ahaa haaa haaa haaa KOVA OYEEEE BBC tupuuu.
 
Hii ni tanzania
Meno 214 gawanya kwa mbili ni tembo 107 wameuwawa kama ni zile pembe tuu
Duh na bado walikouwa hao tembo kuna walinzi wa hifadhi na mbuga za wanyama wanaolipwa na serikali na bado idadi hiyo kubwa ya tembo wameuwawa na bado tunasema tuna askari wa wanyamapori
Hii nchi hii bana kila kiru kinawezekana mkuu nngu007

Kumbuka pia Venance Tossi ndiye kamanda wa hao jamaa yaani askari wa wanyapori. Nina wasiwasi Tossi yuko pale kuhakikisha watu wanaua tembo bila kukamatwa na si kuwalinda kwa manufaa ya waTZ. Tossi alikuwa anawatumikia mafisadi kabla ya kustaafu nani adanganyike kuwa kule wanyamapori atawapinga the same mafisadi badala ya kuwa mlinzi wa mali zao?
 
siamini kama polisi walikataa kupewa hongo au hawakukubaliana price nini?

Usishangae Mzazi huo mzigo unaweza pigwa biashara ukiwa hapo kituoni na mtu auchukua baada ya mwaka mtakuwa msha sahau kabisa .................twiga waliopanda ndege imeishia wapi
 
Hawa wanawezaje kuziuza hizo pembe wakati Tanzania kama nchi tulishindwa kuziuza zilizopo kwenye stock yetu?
 
Duh Naona Tembo watakwisha Kabisa!! Tembo zaidi ya mia Hapo!! Au walichomoa pembe na Tembo Kubaki Hai?
 
Back
Top Bottom