Ujambazi Unaofanywa Na Polisi Tarime !

Ujambazi Unaofanywa Na Polisi Tarime !

Baada ya kuvuka sehemu moja inayoitwa Nyancha Bukenye mida hii kuna polisi wanasimamisha kila gari linalopita barabarani na kuwalazimisha madereva kutoa hela wakidai wana speed na makosa mengine ya kulazimisha. Mmoja wao anatoa kauli chafu sana kwa madereva, anawaambia asiyetaka kutumia barabara anunue ndege apae usitumie barabara

Hawa watu wanataka hela yoyote siyo chini ya 20,000. Mimi wamenilazimishia makosa sita na kutaka 180,000 baada ya mabishani wakasema watanipunguzia iwe laki moja. Ukiwaambie wakupe risiti wanasema wanakupeleka kituoni huko utapata evidence ya speed yako huko. Ukikomaa sana, wanakupa risiti feki, lakini lazima uwape hela kwanza. Nimefanikiwa kumpata mdada anayekusanya hela ni WP 9555 PC Grace. Kamanda Siro imulike ofisi ya OCD Tarime. Watasababisha vurugu maana huu unyanganyi siyo wa kawaida. Huyo Grace aisaidie polisi kufanya uchunguzi. Wana Land rover Defender Pick up nyeupe iliyofichwa kwenye Kichaka
Hata mimi mkuu wmenitesa sana hao jamaa tena wanasema tochi haifutwi hata kwa rais.
Hawa jamaa waliniumiza sana moyo. Wamenichanja pesa wakati naenda tarime na wakati narudi dar.
 
Huyo WP Grace ana shida ila waliambiwa wachukue za brush viatu!! Ndio hizo wanachangisha hapo!!!
 
Kwanini usiende takukuru kama unauhakika wanatoa risiti feki,acha kulalama onana na taasisi husika badala ya kuja kulia mitandaoni

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
Usimlazimishe, inategemea muda wake uko vipi!
 
Hakuna watumishi wanyang'anyi nchi hii kama hapo Polisi
 
Polisi Wa kanda maalum Tarime ndo tabia yao,cha msingi tafuta virekodi sauti ili wakati wanataka rushwa uwarekodi,Mimi huwa natembea nacho ila bahati yao sijawapata.ila day IPO watauingia mkenge.
 
Baada ya kuvuka sehemu moja inayoitwa Nyancha Bukenye mida hii kuna polisi wanasimamisha kila gari linalopita barabarani na kuwalazimisha madereva kutoa hela wakidai wana speed na makosa mengine ya kulazimisha. Mmoja wao anatoa kauli chafu sana kwa madereva, anawaambia asiyetaka kutumia barabara anunue ndege apae usitumie barabara

Hawa watu wanataka hela yoyote siyo chini ya 20,000. Mimi wamenilazimishia makosa sita na kutaka 180,000 baada ya mabishani wakasema watanipunguzia iwe laki moja. Ukiwaambie wakupe risiti wanasema wanakupeleka kituoni huko utapata evidence ya speed yako huko. Ukikomaa sana, wanakupa risiti feki, lakini lazima uwape hela kwanza. Nimefanikiwa kumpata mdada anayekusanya hela ni WP 9555 PC Grace. Kamanda Siro imulike ofisi ya OCD Tarime. Watasababisha vurugu maana huu unyanganyi siyo wa kawaida. Huyo Grace aisaidie polisi kufanya uchunguzi. Wana Land rover Defender Pick up nyeupe iliyofichwa kwenye Kichaka

UPDATE. Huyo Grace hakuwa na sauti. Kazi yake ilikuwa ni kukusanya Hela. Steringi alikuwa ni Mzee mmoja aliyevaa Uniform pamoja na Kijana aliyevaa nguo ZA Kiraia. Alivaa T-shirt ya rangi ya damu ya Mzee, yenye mistari mieusi
Nimetupia uzi related na huu jana, ujue siku hizi wana tochi za kwao wenyewe na si za serikali.
Pia nawe uwe muelewa hata ukamatwe na makosa mia saba unalipia kosa moja tu.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mm huwa najiuliza kwanini wanajificha machakani??? Kukaa chakani mwishowe uumwe na nyoka bura kisa unalenga matochi....waelimishe watu watajua na watatii...sasa haya mambo kila sehemu ni shida...unakuta askari anakusimamisha anakuomba leseni ukimpa tu anaanza kutembea kwenda kwenye kazi nyingine sasa unaanza kumfafata kama vile huna akili...wanafanya mambo mabaya sana hawa jamaa...wabadilike tujenge nchi..waelemishe watu sio kila siku lazima fine..elimisha kwanza elekeza hela sio kila kitu.
 
Hivi ukiishitaki polisi utasikilizwa????

Zaidi wewe toa laana tu... me nilitoa laana kwa Trafiki mmoja ovyo sana nilipata ajari mbezi gari yangu imetoka police naipeleka parking ya bima ipigwe picha kisha iende garage akanikamata ati gari imegongwa alihakikisha gari inalala police maana alichukua key tokea mchana hadi jioni ati yupo kazini hatuwezi kwenda central nikamind mno.. akazuia leseni yangu kinguvu tulikururushana maana aliingangania kwa nguvu na nikona hawana nguvu kwani kijasho kilimtoka hahaha Trafiki fanyeni mazoezi.... huyo Askari nilikuja muona kavaa nguo za ffu na bunduki kabebeshwa nilicheka sana... laana imempata pesa za kukomoa watu kwishnei
 
Nimeendesha gari kwa miaka 12, sijawahi ambiwa fine zaidi ya 30 au mara 2 tsh 60, huko hapatakuwa Tanzania!
Kuna madereva wa daladala mkoa wa Songwe washawahi kugoma kwasababu walikua wanaandikiwa fine hadi nne kwa wakati mmoja na huo mkoa upo Tanzania
 
Aisee polisi ni watu wa ajabu sana
 
Hivi ukiishitaki polisi utasikilizwa????

Zaidi wewe toa laana tu... me nilitoa laana kwa Trafiki mmoja ovyo sana nilipata ajari mbezi gari yangu imetoka police naipeleka parking ya bima ipigwe picha kisha iende garage akanikamata ati gari imegongwa alihakikisha gari inalala police maana alichukua key tokea mchana hadi jioni ati yupo kazini hatuwezi kwenda central nikamind mno.. akazuia leseni yangu kinguvu tulikururushana maana aliingangania kwa nguvu na nikona hawana nguvu kwani kijasho kilimtoka hahaha Trafiki fanyeni mazoezi.... huyo Askari nilikuja muona kavaa nguo za ffu na bunduki kabebeshwa nilicheka sana... laana imempata pesa za kukomoa watu kwishnei

Utawashtaki wapi? Ila laanainatosha na pia kuwashtaki katika maakama ya Mungu inayotoa laana kwaona vijukuu vyao
 
Aisee!!!!

Sasa hapa ulimlaani au ulimbariki akafanye mazoezi kama ulivyosema.
 
Ungechukua video mbona wangetumbuliwa leo asubuhi
 
Utawashtaki wapi? Ila laanainatosha na pia kuwashtaki katika maakama ya Mungu inayotoa laana kwaona vijukuu vyao
Nadhani ifike muda kama taifa tujitafakari tunakokwenda. Kwa nini Polisi wanaolinda amani kila siku walalamikiwe kwa uonevu. Hili swala siyo la mzaa. Mimi mwenyewe hawa watu walishachukua kwangu 50,000 kipindi cha nyuma njia ya Tanga, Asubuhi na mapema baada ya kulazimisha nilikuwa mwendo mkali.

IGP awamulike hawa walalamikiwa. Kila siku ni jeshi la polisi, too much
 
Afadhali umeyasema wewe kaka. Wengine tungeitwa wachochezi
 
Back
Top Bottom