FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
MADEREVA wa magari ya kusafirishia abiria daladala zinazotumia barabara ya Shekilango, Morogoro, Bagamoyo na Mandela Jijini Dar es Salaam, wamelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini watu wanaojiita Polisi Jamii ambao wamekuwa wakiwakamata mara kwa mara na kuwatoza faini na kuwafanyia fujo katika maeneo hayo FikraPevu imejulishwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Juni 30, 2014 baadhi ya madereva hao akiwemo, Juma Godfrey, wamesema katika barabara hizo kumekuwepo na baadhi ya watu wanaojiita Polisi Jamii ambao wamekuwa wakiwapiga faini hata kama hawana makosa na pindi wanapokataa kutoa fedha hizo wanawazuia kuondoka katika sehemu waliyosimamishwa.
Aidha, wamesema licha ya kuwepo na Askari wa usalama barabarani wameshindwa kutatuz tatizo hilo licha ya kuwapa taarifa juu ya tatizo hilo, na hivyo kuwalazimu kukabiliana na tatizo hilo.
Katika mahojiano na FikraPevu, madereva hao wameiomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuandaautaratibu mpya ambao utawarahisishia kufanya biashara yao ya usafirishaji abiria pasipo kukutana na vikwazo visivyo vya lazima hali inayowafanya kuhofia kupata hasara katika mapato ya biashara hiyo kutokana na fedha wanazozitoa.
Wakati huo huo, madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo, wamelaani kitendo cha kuzuiwa kufika kati kati ya jiji hilo, huku wakisema kitendo hicho kimewafanya baadhi ya watu wasiohusika kutoka mamlaka husika kutumia nafasi hiyo kuwakamata kwa madai ya kwenda kinyume na sheria za usalama barabarani.
Tunapo lipa faini na kudai risiti wanatutishia kutupelekwa polisi, sasa kwasababu hapa ni mjini na ukisema ufuatilie hilo jambo litakupotezea mda wako hata kama utakuwa umepata haki yako lakini mwisho wa siku bosi wako anahitaji umpe hesabu, na hii ndio inatulazimu sisi kuwapa hela kwa huo mda ili tuendelee na shughuli zatu alisema mmoja wa madereva hao.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamanda Awadhi Haji, amesema....
Habari zaidi. soma=>Polisi Jamii walalamikiwa kuwalaghai waendesha daladala Dar