Ujamaa wa Tanzania na Dini (Hotuba ya J. K. Nyerere - 1970)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,475
19,508
HOTUBA YA NYERERE NA VIONGOZI WA DINI TABORA 27/7/70​
Key Take Away:
  • NCHI ya Tanzania / TANU hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...
  • Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani); Tunaulizana Habari za Maji, Maharagwe na Mabarabara..... Lakini hatuulizi Kabisa kama ipo Pepo; kama kwenda Mbinguni ziko ngazi ngapi ? Tunaulizana ya kwetu yanataka Kura, sasa la Mungu mtalipigiaje kura ! Kwamba wengi wamekubali Mungu yupo kwahio yupo au hayupo ?
  • Dini; Mimi nina yangu Karume ana yake Kawawa na Waheshimiwa wengine, Waheshimiwa mbalimbali kila mtu ana yake....., tunapokutana kwenye mikutano hatumuulizi leo Umesali ? Aa! Hiyo ni Hiari yake, kasali hakusali anajiuliza Mwenyewe
  • SIASA ya UJAMAA kwa mtu anayejua Socialism ya Ulaya mtu wa Dini Inabidi Aelezewe vizuri sana sivyo atakupinga (atakuona hatari)
  • Ulaya ilifika wakati watu wakasema "Kama Dini yenyewe ipo hivi Hatukubali"; Dini inatetea Mali zaidi ya mtu
  • CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.
 
Attachments

  • Ujamaa na Dini.pdf
    14.2 MB · Views: 6
HOTUBA YA NYERERE NA VIONGOZI WA DINI TABORA 27/7/70​
Key Take Aways:
  • NCHI ya Tanzania hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...
  • Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani); Tunaulizana Habari za Maji, Maharagwe na Mabarabara..... Lakini hatuulizi Kabisa kama ipo Pepo; kama kwenda Mbinguni ziko ngazi ngapi ? Tunaulizana ya kwetu yanataka Kura, sasa la Mungu mtalipigiaje kura ! Kwamba wengi wamekubali Mungu yupo kwahio yupo au hayupo ?
  • Dini; Mimi nina yangu Karume ana yake Kawawa na Waheshimiwa wengine, Waheshimiwa mbalimbali kila mtu ana yake....., tunapokutana kwenye mikutano hatumuulizi leo Umesali ? Aa! Hiyo ni Hiari yake, kasali hakusali anajiuliza Mwenyewe
  • SIASA ya UJAMAA kwa mtu anayejua Socialism ya Ulaya mtu wa Dini Inabidi Aelezewe vizuri sana sivyo atakupinga (atakuona hatari)
  • Ulaya ilifika wakati watu wakasema "Kama Dini yenyewe ipo hivi Hatukubali"; Dini inatetea Mali zaidi ya mtu
  • CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.
Log...
Hebu soma hayo hapo chini:

HOTUBA YA NYERERE NA VIONGOZI WA DINI TABORA 27/7/70

Key Take Aways:

NCHI ya Tanzania hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...

  1. Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani); Tunaulizana Habari za Maji, Maharagwe na Mabarabara... Lakini hatuulizi Kabisa kama ipo Pepo; kama kwenda Mbinguni ziko ngazi ngapi? Tunaulizana ya kwetu yanataka Kura, sasa la Mungu mtalipigiaje kura ! Kwamba wengi wamekubali Mungu yupo kwahio yupo au hayupo?
  2. Dini; Mimi nina yangu Karume ana yake Kawawa na Waheshimiwa wengine, Waheshimiwa mbalimbali kila mtu ana yake... tunapokutana kwenye mikutano hatumuulizi leo Umesali ? Aa! Hiyo ni Hiari yake, kasali hakusali anajiuliza Mwenyewe.
Hapakuwa na mwanachama katika harakati za kuwaunganisha wananchi wa Tanganyika katika African Association ambae alikuwa na fikra ya kuwa hajui kuwa ‘’Mungu yupo au hayupo.’’

Sababu ya mimi kusema hivi ni kutokana na waasisi wa African Association wenyewe ambao wengi wao walikuwa Waislam.

Kusema maneno hayo hiyo ni kufru kubwa.

Wanachama walioasisi African Association mwaka wa 1929 ni hawa: Abdallah Kleist Sykes, Secretary, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu na Zibe Kidasi jumla yao watu sita.

Waliobakia watatu: Cecil Matola, President, Rawkesi Kusi na Rawson Watts hawa ni Wakristo.

Waislam ndiyo waliokuwa wanatawala siasa miaka hiyo na walikuwa wakianza mikutano yao yote kwa dua.

Huwezi kusoma dua ikiwa huamini kuwa yupo Mungu, muumba wa ardhi na mbingu na kila kitu kilichoma katika ya viwili hivi.

Kuonyesha nafasi ya Uislam katika siasa za Tanganyika ni kuwa baada ya kuunda African Association mwaka wa 1929 ili kuiweka African Association nje ya Uislam Kleist Sykes na Mzee bin Sudi wakaunda mwaka wa 1933 Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) Mzee bin Sudi akiwa President na Abdallah Kleist Sykes, Secretary.

Mkutano wa kwanza wa TANU ulihudhuriwa na hawa wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Sioni vipi watu hawa kama ninavyowafahamu wangekubali kusikia mtu katika chama chao anamkashifu Allah kuwa hana uhakika kama yupo au hayupo.

TANU isingekuwapo kama hii ndiyo ingekuwa sera yake.

Ningeweza kuweka mifano mingi ya kuwa TANU na waasisi wake pamoja na waliokiunga mkono waliamini Mungu.

TANU ilikuwa na dini na si tabu kutambua hili.
Angalia picha ya wanachama wa TANU wa miaka hiyo:

1706702090913.png

Mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 angalia kofia na kanzu.
1706702208906.png

Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja angalia kushoto wanawake wamevaa mabaibui na wametengewa sehemu yao maalum ya kukaa​
 
Wanachama walioasisi African Association mwaka wa 1929 ni Waislam ni hawa: Abdallah Kleist Sykes, Secretary, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu na Zibe Kidasi jumla yao watu sita.

View attachment 2889767
Mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 angalia kofia na kanzu.
View attachment 2889769
Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja angalia kushoto wanawake wamevaa mabaibui na waketengewa sehmu yao maalum ya kukaa​

Kwahiyo we mzee ulitaka kusemaje labda,mana hunaga jipya zaidi ya udini hofu yako kubwa ni ipi?
 
Huenda wote walikuwa waumini katika uanzilishi, Je inamaanisha waliendelea wote kuwa waumini ? Je inamaanisha angekuja mpagani katika Chama hicho cha ukombozi asingepewa uanachama sababu tu sio muumini ?

Sidhani kama JKN alisema haya kwa kumaanisha kwamba Dini ni mbaya La Hasha..., Bali Dini ni an individual thing ni vigumu sana kuwaweka watu kwenye imani tofauti katika same blanket (ingawa matatizo ya njaa, umasikini na unyonyanyaji hayo hayachagui Imani) kwahio maana yake ilikuwa ni kuwaachia injili na mafundisho ya Kiimani viongozi wa Dini na Imani yao (Ingawa hakuwakataza watu kukemea maovu kwa vijimaneno vya eti ya Kaisari kumuachia Kaisari)
Wanachama walioasisi African Association mwaka wa 1929 ni Waislam ni hawa: Abdallah Kleist Sykes, Secretary, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu na Zibe Kidasi jumla yao watu sita.

Waliobakia watatu: Cecil Matola, President, Rawkesi Kusi na Rawson Watts hawa ni Wakristo.

Waislam ndiyo waliokuwa wanatawala siasa miaka hiyo na walikuwa wakianza mikutano yao yote kwa dua.

Huwezi kusoma dua ikiwa huamini kuwa yupo Mungu, muumba wa ardhi na mbingu na kila kitu kilichoma katika ya viwili hivi.

Kuonyesha nafasi ya Uislam katika siasa za Tanganyika ni kuwa baada ya kuunda African Association mwaka wa 1929 ili kuiweka African Association nje ya Uislam Kleist Sykes na Mzee bin Sudi wakaunda mwaka wa 1933 Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) Mzee bin Sudi akiwa President na Abdallah Kleist Sykes, Secretary.

Mkutano wa kwanza wa TANU ulihudhuriwa na hawa wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Sioni vipi watu hawa kama ninavyowafahamu wangekubali kusikia mtu katika chama chao anamkashifu Allah kuwa hana uhakika kama yupo au hayupo.

TANU isingekuwapo kama hii ndiyo ingekuwa sera yake.

Ningeweza kuweka mifano mingi ya kuwa TANU na waasisi wake pamoja na waliokiunga mkono waliamini Mungu.

TANU ilikuwa na dini na si tabu kutambua hili.
Angalia picha ya wanachama wa TANU wa miaka hiyo:
Nadhani hapo hatumtedei haki Mwalimu yeye mwenyewe alikuwa Mkristo na aliyasema hayo akiwa amezungukwa na watu wa Dini ila maana yake ni kwamba angewa yeye na hao wengine wanaamini je akija mwingine asiyeamini basi afukuzwe au asisikilizwe ? Je kujiunga / kuwa mtanzania lazima uwe Mkristo au Muislamu ? Nadhani hapo unaona tukienda kwenye such a rabbit hole tutajikuta tumeacha kuongelea Maji, Maharage na Mabarabara na tunajadili ni vipi tutafika peponi (wakati tunaweza kuvifanya vyote hivyo kwa wakati wake wala bila kuwatenga wasioamini kama sisi)

View attachment 2889767
Mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 angalia kofia na kanzu.
View attachment 2889769
Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja angalia kushoto wanawake wamevaa mabaibui na waketengewa sehmu yao maalum ya kukaa​

Ni vema na Haki je wangekuja machifu na mafuvu na Mizimu yao mgewafukuza ?
 
Mohamed Said Nadhani ni vema badala ya kukujibu kama mimi nikujibu kama Hotuba inavyosema kama haujaisoma alafu uniambie ni wapi JKN amepotoka kuhusiana na Dini ya TANU

Chama chetu hakina dini. Kama Chama cha TANU, hakini dini. Ni Chama cha Siasa tu. Na hakina dini wala hakina Uhusiano na dini. Nitaeleza maana yake.

Vipo Vyama duniani vya Siasa lakini vina uhusiano na dini. Kwa mfano, sasa hivi katika nchi mbali mbali za Ulaya viko vyama si vidogo, vikubwa vinatawala, vinahusiana na dini. Ujerumani Magharibi kipo chama kinaitwa Christian Democratic Union. Ni Chama cha Siasa; lakini cha dini. Kinaitwa "Chama cha Demokrasi cha Kikristo". Italia wana cha namna pengine kama ningependa kutaja ningeweza nikavitaja. Chama umsingi wake wa Siasa yake ni dini — dini fulani. Kwa hiyo, ndiyo kusema nadhani, ndiyo kusema, kwa mfano, Ujerumani au Italia kama kungekuwa na Waislamu, na wao wangeweza wakaanzisha Chama chao — labda "Moslem Democratic Union"! Kwa msingi huo na wao vile vile wangeweza wakaanzisha chama chao cha Siasa lakini msingi wake dini. Chetu hakina. Hatuna msingi wa dini.

Kadhalika nchi yetu. Nchi yetu Tanzania haina dini. Hilo nalo naweza kuwasitusheni, lakini nitalieleza. Hatuna dini maana yake nini? Kwamba nchi yenyewe Tanzania haina dini. Kwamba tuulizwe "Dini ya Tanzania, dini rasmi ya Tanzania ni dini gani, tuitamke" — Aa hakuna, hatuna; nchi yetu haina dini. Uingereza ina dini rasmi; ina dini Dini ya nchi, inayokubaliwa na Katiba ya Nchi. Waingereza kwa Katiba ya Nchi ni Anglikani. Na kweli Mfalme wa Nchi sharti awe Anglikani. Na Wakubwa kubwa wa nchi vile vile wanaojulikana sharti wawe Anglikani. Lazima wawe wa madhehebu hayo. Wawe ni Wakristo lakini Wakristo wa aina fulani. Ni Waprotestant lakini Waprotestant wa aina -fulani. Hiyo ndiyo dini rasmi ya nchi. Wengine wanakubaliwa. Hawaharamishwi.' Kwa hiyo Mkatoliki anakubaliwa vile vile awepo na aabudu. Na Mprotestant\ wa madhehebu mengine mengine anakubaliwa awepo na aabudu. Lakini Ki-Katiba wanazuiwa wa madhehebu hayo kushika vyeo fulani fulani kwa sababu dini zao, madhehebu yao, madhehebu rasmi ya nchi. Hiyo ni ya testant.

Zipo za Kikatoliki. Nadhani Italia ni ya Kikatoliki rasmi. Dini ya Italia ni Ukatoliki- Ndiyo dini rasmi ya nchi. Wengine wanakubaliwa; kama wapo Wàprotestant wanakubaliwa; kama wapo Waislamu hawafukuzwi. Wanakubalika lakini hawakubaliki rasmi: kuna kazi fulani fulani za nchi hawawezi wakazifanya kwa sababu ya dini yaol Nadhani Pakistan ni nchi ya Kiislamu kwa Katiba — kwa katiba. Ni nchi ya Kiislamu kwa katiba. Kwa hiyo dini zingine zinaruhusiwa. Ukiwa Mkristo unaruhusiwa. Lakini Ki-Katiba ni Dini ya Kiislamu. Hivyo ndivyo ailivyo nchi nyingine.

Sisi hapana. Sisi hatuna. Sisi hatuna dini. Sisi nchi yetu haina dini. Sisi si nchi ya Kikristo; wala si nchi ya Kiislamu; wala si nchi Kiyahudi; sisi ni Tanzania tu. Ndiyo hivyo. Watanzania wenyewe wana dini. Watanzania wenyewe wana dini; nchi haina. Watanzania: Sheikh pale Mwislamu; Mama pale Mkatoliki; wengine huko wanajua wenyewe. Kila Mtanzania kila mmoja ana dini yake — yake. Mimi nina yangu. Sheikh ana yake hapa; hawa hapa, oh, mbalimbali hawa; mbalimbali, wakati wengine wala hatuwaulizi juu ya dini zao. Hatujui dini zao; kila mmoja anajua yake. Watanzania kila mtu ana dini yake. Na hazikatazwi, hazikatazwi na sheria ya nchi; madhali si dini zinazoleta ukorofi — ukorofi. Yapo madhehebu ya ukorofi ukorofi. Kuna madhehebu yanakataa serikali; yanasema kitu serikali ni haramu kinakatazwa na Mungu. Sasa hao wakorofi sana. Tunawakataza. Nadhani moja tumeiharamisha: tumeipiga marufuku kwa sababu ya ukorofi ukorofi wake. Kuna. madhehebu mengine wanasema Mungu aliumba•mtu hana nguo; kwa hiyo kwa nini kuvaa, na tutembee hivi hivi hatuna nguo. Hayo nayo tunaona wakorofi; aa dini za namna hiyo zinaweza zikatuletea taabu bure bure. Hizo tunaizuia kwa sababu huenda zikaleta fujo baina ya raia: zikaleta vurugu baina ya raia. Lakini kama dini haileti vurugu baina ya raia tunaikubáli. Tunaikubali lakini ni ya mtu, si ya nchi. Si ya nchi yetu ya Tanzania iwe ikiulizwa: Dini ya Tanzania ni nini? Inatamkwa! Au kwamba iko katika katiba! Hatuna. Hiyo hatuna,

Na hivyo hivyo kabisa kwa Chama chetu. Nataka kurudia tena Hatuna dini; hatuna kabisa Uhusiano na dini. lakini wenyewe mmoja mmoja tuna dini: Mimi nina yangu; Kawawa ana yake; Karume ana yake; Waheshimiwa mbali mbali kila mtu na yake. Lakini tunapokutana katika mkutano hatumwulizi: "Leo umesali?" Aa! Hiyo ni hiari yake kabisa. Kama kasali au hakusali anajiuliza mwenyewe; hatumwulizi sisi. Hatumwulizi dini yake; hatumwulizi kama ana dini au hana dini. Kabisa hatumwulizi. Kwa hiyo katika Chama chetu hatumwombi mtu awe Mkristo wala hatumwombi mtu awe Mwislamu.

Viko Vyama vinafanya hivyo. Vinasema: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — hiki ni chama cha Wakristo, wewe Mkristo?" Ukisema hapana, wewe huwezi kuingia! Au: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — chama hiki ni cha Waislamu; wewe ni Mwislamu?" Ukisema hapana, wewe huwezi kuingia, Au vingine vinasema: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — chama chetu hakikubali dini; wewe nawe unakataa dini?" Ukijibu: "Mimi naamini dini"; basi wewe huwezi kuingia. Viko vyama vya namna hii ambavyo ili uingie katika chama sharti useme: hakuna Mungu!"

Sisi hatuulizani habari hizo. Katika Chama chetu cha TANU hatuulizi habari za Mungu. Kichama hatujui kama Mungu yupo au hayupo. Si jambo tunalolizungumza katika Katiba: "jamani Mungu yupo?" Hatuulizani kabisa. Tunauliza habari za maji, na maharagwe, na mabarabara... Lakini hatuulizi kabisa kama iko pepo; kama kwenda mbinguni ziko ngazi ngapi? Hatuulizani hilo. Maana mambo tunayoulizana ya kwetu ndiyo yanataka kura. Tunapiga kura. Sasa la Mungu mtalipigiaje kura! Kwamba wengi wamekubali kwamba Mungu yupo kwa hiyo Mungu yupo. Au wengi wamekataa kwamba Mungu hayupo...! Hilo hatujui sisi. .Vyama vingine vinajiingiza katika mambo haya ya kuamua: waamue kichama kama Mungu yupo; au waamue kichama kwamba hakuna Mungu. Sisi hatufanyi hivyo. Halituhusu kabisa kabisa. Hatumwulizi kabisa mwanachama wetu. Akiwa Mwislamu tutamkubali; kama ni Mkristo tunamkubali; kama unaabudu mizimu, Mzanaki wa hivi hivi tu — "non-aligned" tunamkubali. Hata kama ni "atheist" anayekana Mungu, tunamkubali. Anayesema: "hakuna Mungu", kwa sababu hilo si jambo linalozungumzwa katika Chama hiki.

Madhali hatumwulizi dini; madhali hatumwulizi Uislamu wake; hatuulizi imani yake kwa namna yoyote. Kwa hiyo wakuu wa dini wasishangae kuona Sisi tumechanganyika katika Chama. Waislamu humo humo — tena Waislamu wote basi: WaSunni, Wa-shia, Wa-Kadiani — wote, Wakristo wa Madhehebu yote. Na, hao wasiokuwa Wakristo nao wa madhehebu yote: wanaoabudu vibuyu, wanaoabudu mwezi, wanao... wote tunawakubali,

Hilo, nasema lilikuwa jambo la kwanza kulieleza. Na tunafanyå hivyo kwa kuamini kwamba hivyo ndivyo sawa. Tunafanya hivyo kwa kuamini kwamba hivyo ndivyo sawa. Haifai Nchi iwe na dini inaitwa rasmi. Tunasema nchi inapokuwa inachagua dini, inaifanya rasmi, inadhalilisha dini zingine. Na si kazi nchi kufanya hivyo. Inawatia raia wa dini zingine unyonge wa bure. Kwa hiyo raia lazima wote wawe sawa. Na nchi ikija kuchagua dini imewafanya raia wake hawatakuwa sawa Raia wa dini fulani watakuwa ni bora kuliko. raia Ya dini zile ambazo hazikuchaguliwa.

Kadhalika Chama chetu tunaona ni sawa kwamba iwe hivyo, kwamba chama chetu hakina: dini, hatutaki kukiingiza katika mambo. ya dini, Lakini• Chama. chetu kinatetea haki ya kila mtu kuabudu. kwa kadiri ya Imani yake. 'Hilo tunalikubali na kuona kwamba ni la maana.
 
Sisi wa Africa ni majuha,badala kujadili jinsi ya tufanye mambo ya maendeleo ,tunawaza uislamu na ukristo tulioletewa na waarabu na wanzungu.mbaya zaidi waarabu waliwaua babu zetu.ndiomaana hakuna mwarabu mweusi.🤬🤬🤬🤬🤬😇😇
 
Hana hofu yoyote ila anarekebisha au anasahihisha historia iliopindishwa. Uzuri vithibitisho viko wazi kwa hiyo jibu hoja usishambulie udini.
Katika kujadili hii Hutoba au faida na hasara yaliyosemwa unadhani ni wapi JKN alikosea ? TANU ilikuwa DINI gani na TANZANIA ni DINI gani ? Pili hata kama Chama na Nchi vina DINI ni nini Faida ya kuwa hivyo kwenye nchi ambayo ni diversify kama hii?
 
Kwa hiyo ni kwamba Udini uliingia baadae katika TANU? na kisha CCM? Kwa sasa Maaskofu na Mapadre wamekua na nguvu sana kiasi cha kupeleka Kanisani mambo ya Nchi wanapata wapi mamlaka haya!?
 
MOJA; KUKEMEA SIO KWAMBA KULIKATAZWA -TENA JKN AMESEMA KABISA KAMA TUNAKOSEA KATIKA KUTETEA WANAONYONYWA MTWAMBIE - MSIKAE KIMYA

Hata katika hii Hotuba anasema sababu ya Makanisa kupoteza Sifa yake nzuri huko Ulaya ni sababu ya Makanisa Ku-side na Wanyonyaji na kuwa Wanyonyaji hivyo watu kuona kwamba Hawafai...... NANUKUU KUTOKA KWENYE NUKUUU

Kuna Mataifa mawili Sasa". Katika nchi ile ile ? moja kuna mataifa mawili — kuna kataifa kadôgo ka mabwana kanashiba, kanatakata, kana jeuri, na taifa kubwa la wafanyakazi hawana kitu maskini, hali yao inazidi kuwa dhalili.

Manung'uniko lazima yaanze. Yakaanza. Yakaanza. Dhahiri katika nchi zile, imegawanyika sehemu moja inaonea, dhahiri inaonea, na sehemu moja inaonewa. Wafanyakazi lakini jasho lao linapotea hivi hivi. Manung'uniko yalikuwaya ? Lazima. Lazima. Mtu hakubali akae ananyonywa hivi hivi. Halafu anyamaze tu asiseme. Kwa hiyo, dhahiri watu walianza kunung'unika? Watu walianzaz kunungunika kwa sababu wafanyakazi dhahiri wanadhulumiwa na matajiri wao. Nasema kelele hizi Ulaya zikawa nyingi sana katika karne mwisho wa karne iliyopita. Nyingi sana!

Sasa, watu wanazungumza juu ya . dhuluma; watu wanazungumza juu ya dhuluma. Watu wengi wananung'unika wanasema wanadhulumiwa na wachache. Dhuluma jambo baya.

Waelezaji wa mema na mabaya duniani, waliotumwa waeleze mema na mabaya duniani angalao wenyewe ndivyo wanavyotuambia — ni wakubwa wa dini. Wasimamizi: "Msifanye hivi — hivi ni vibaya; msifanye hivi hivi -ni vibaya. Fanyeni hivi hivi ndivyo vizuri.. Inafika wakati ambapo taifa limegawanyika katika sehemu mbili: watu fulani wananungunika - tena wengi wananung'unika kwamba wanaonewa, na wachache wanawaonea. Kilio kikubwa si kidogo hicho.

Inapofika hapo Watu wa dini — nyinyi mnatazamiwa sauti yenu iwe ya wazi wazi. Si ya mashaka mashaka, Kama ni mazungumzo kati ya haki na dhuluma, wakubwa wa dini hawatazamiwi kunongona; au kuwa na mashaka mashaka; lazima waseme dhahiri: "Mnaonea nyinyi; mnawadhulumu hawa" Lakini jamaa wanaojua historia hii ya Ujamaa Ulaya wanajua kwamba kauli ya Makanisa haikuwa ya wazi wazi, Makanisa yalibabaika. Makanisa. ya Kikristo yalibabaika babaika katika jambo hili. Makanisa ya Ulaya yalibabaika kidogo katika jambo hili la dhuluma Kwa nini yalibabaika, wanajua wenyewe.

Lakini wengine tunadhani kwamba ingawa dini ni ya Mungu; anawapa Mitume wake: "Kawafundisheni binadamu kadha kadha". Lakini' hao Mitume wanaotumwa, hao ni binadamu hao. Kwahiyo pamoja na kueleza dini yenyewe kama walivyotumwa na ubinadamu hupitapita hümo! Na wakati mwingine vitamaa tamaa vya kibinadamu hupita pita humo vikawapata watu. Wakati mwingine dini, Uislamu na Ukristo, hupakwa matope na ubinadamu — ubinadamu! Dini zilizotazamiwa zisimamie haki tu hujikuta zimeambatana kidogo — kidogo, kidogo ----- kidogo, kidogo — kidogo; Zimepakwa pakwa matope; na matope yale yanafifisha sauti yake!

Katika hili: Ardhi ni ya Mungu. Ardhi anatoa Mungu anawapa binadamu wote— Sisi wapangaji tu. Tunakuja tunapanga tunakwenda; tunakwenda; hakuna mtu aliyetengeneza ardhi. Tunapanga tunakwenda. Tunakuja hivi hivi — tunakuja hivi hivi. Ardhi ipo kwa binadamu wote; Sio kwa baadhi ya binadamu; kwa binadamu wote. Leo Julius na Mheshimiwa hapa wanasema, "Hii yetu", yaani tunachukua haki katika ardhi ya kumnyima huyu, kumnyima huyu, kumnyima huyu! haki hii tunaipata wapi? Wanyamwezi — tuseme — sasa Wanyamwezi mkitaka ardhi niombeni mimi na "Area Commissioner", ni mali yetu; na "Regional Commissioner" ni mali yetu. Maana yake ninil Hii haki tuliipata wapi? Kwa sababu ardhi anatoa Mungu; kulima nalima mimi; kufyeka nafyeka mimi. Naweza kusema, "Hapa nimefyeka jama, nimefyeka mimi; usiniingilie nimefyeka mwenyewe hapa; Aa Aa". Lakini ardhi yenyewe ni ya Mungu.

Sasa tunaanza kugawana; mimi nachukua. huyu anachukua, na Kanisa nalo linachukua! Mimi nimepata pande langu, Mheshimiwa amepata pande lake, Kanisa nalo limepata pande lake, na Maimamu nao wamechukua mapande yao ya ardhi; wanasema wakfu! Vema. Watu wanaanza kunung'unika sasa: ''Jamani hatuna pa kulima!" Tunawatoza. Mimi nawatoza; bwana anawatoza; na Mheshimiwa wa Wakfu na wewe unawatoza. Wote tunawatoza. Wanapiga kelele: "Jamani ardhi ni ya wote imekwenda kwendaje ardhi imekuwa ya mtu" Mimi nasema: ''Nani anasema watu wote sawa'?" Mimi nasema, "Nani kasema watu wote sawa. Watu wanaweza kuwa sawa bwana. Watu tuko tofauti; wengine wanawatumikia wengine. Wote mnawezaje kuwa sawa; mbona hata vidole haviwi sawa?" Mimi nasema hivyo. Na Imamu naye anaanza kusema hivyo hivyo; anachukua na Msahafu. Anapata aya fulani inayosema hayo anayoyataka yeye anakwenda Msikitini anasema:" Nani anasema watu wote ni sawa?" Na Padri anaanza kutetea jambo la kumiliki ardhi binafsi!

Tuonyeshe katika Msahafu: Ardhi tunavyojua. Mungu kawaumbia wote hakuigawanya. Wewe Padri. binadamu wamegawana-gawana na wewe umetumbukia ndani!? Sasa Padri akishatumbukia ndani akagawana, na yeye ana-pande Iake Ia ardhi, hawezi kuwatetea maskini.; Hawezi kuwatetea maskini. Anatetea wenzake wenye ardhi. Kadhalika Misikiti na Makanisa mkianza kuwa na nyinyi mña viwanda.- Badala ya kuhubiri Neno Ia Mungu, mnahubiri viwanda vycnu. Mnategemea mali ya kutokana na viwanda. Sasa nyinyi. wafanyakazi na matajiri wanapozungumza juu ya dhuluma, nyinyi lazima mtakuwa huku pamoja na matajiri. Na wafanyakazi wako upande mwingine — wanawanung'unikia matajiri wao pamoja na nyinyi vile Vile.

Kwa hiyo kelele ya dhuluma itakapoanza: "Jama tunadhulumiwa na Matajiri Misikiti kimya; haisemi kitu; Makanisa kimya; hayasemi kitu. Yanasema: "Wana fujo hao". Na hasa- kama wanaodhulumu ni Serikali: haya makubwa, haya yenye mali ndiyo vile vile huwa matawala ya Serikali vile Vile. Basi Mapadri mara wanasimama katika Makanisa wanasema: "Mpeni Kaisari kilicho chake!" "Chake! hata ardhi ya Mungu vile vile yake! Hata ardhi ya Mungu nimpe Kaisari, mali yake ile? Ardhi — Kaisari na mimi kwa Ardhi wote sisi ni sawasawa. Kaisari anakula na mimi nakula. Kwa nini Kaisari yeye awe na ardhi mimi sina Ardhi' Padri kusema: Mpeni Kaisari chake"; ”Chake nini "Chake, Ardhi?" ”Chake, Ardhi? Kaisari ana matumbo mangapi. huyu mnamtetea yeye awe na ardhi? Na sisi wote sawa ! Kaisari anânionea mimi nyinyi mnasema Mpe Kaisari chake ” ' 'Chake", ni kipi cha Kaisari hasa?”

Kaisari kwamba awe na viwanda. Anasema: Hawa wafanyakazi wangu! Kaisari amepata — ana viwanda chungu mzima amevipata wapi viwanda hivyo Kaisari? Kaisari naye si alikuja duniani hivi hivi, naye mtupu hivi kama Sisi? Leo ana viwanda, ana watu wake wanamfanyia kazi, ana mamali ya ajabu!”' Mashekhe tunapiga kelele Sisi: ”Huyu Kaisari anatuumiza jamani tazameni ana mali huyu; kaambatana na matajiri venzake, tunabanwa- tu; sasa Polisi na majeshi ya kutuonea Sisi?' ' Badala ya kuja na kututetea Sisi, Mapadri na Mashekhe mnatwambia: 'Lazima mtii wakubwa”. ''Tuwatii wakubwa, hawa wanyonyaji!” Mnatujibu "Unyonyaji si kitu”.

Mahubiri mengine kwa sababu Sheikh, na lmamu, na Padri na Askofu mmekwisha ambatana mna ma Ardhi, mna viwanda, mna ma mali', kwa sabâbu mmekwisha fitia huku azima mtumie Kuruani na Injili kutetea mali yenu. Hamwezi kuitumia Kuruani na Injili kutetea maskini, hata! Na, inadhaniwa, Ulaya ilifika kiasi hicho. Wanadhani watu Ulaya ilifika kiasi hiëho. Ilifika kiasi hicho! Dhuluma ni ya dhahiri kabisa kabisa, lakini Makanisa kimya! Wanababaika katika jambo la haki kana kwamba Kanisa nalo linababaikal Kanisa kama halijui kama hii ni dhuluma au si dhuluma! Kanisa haliwezi kuwa na mashaka juu ya dhuluma! Kanisa haliwezi kuwa na mashaka liseme: "Hatujui kama hii ni dhuluma au si dhuluma!"

Kanisa wakati wote linajua: Hii ni dhuluma na hii ni haki. Haliwezi kuwa na mashaka mashaka. Haiwezi kuwa imegawanyika kabisa kabisa, kundi kubwa linasema. "Hii dhuluma", halafu Kanisa lasema "Sisi hatujui". Kanisa hamjui! kwamba hii ni dhuluma au si dhuluma?•

Sasa likinyamaza Kanisa, sio kwamba mambo yenyewe basi watu wanyamaze. Kanisa laweza likababaika: inaweza ikababaika; lakini Watu hawawezi kunyamaza Wataendelea. Wataendelea kupigania haki yao. Na Ulaya ilifika kiasi hicho. Ulaya ilifika kiasi hicho; jamaa wakaendelea, Nadhani walifika wakati 'wakasema Ala, kumbe Makanisa yenyewe ndiyo hivyo — lo! potelea mbali"! Wakajikatalia. Wakajikatalia wengine wakakataa dini. "Kumbe dini- zenyewe ndiyo hivyo bwana: dini inaona watu wanaonewa wengine hivi hivi dini haisemi....
 
Log...
Hebu soma hayo hapo chini:

HOTUBA YA NYERERE NA VIONGOZI WA DINI TABORA 27/7/70

Key Take Aways:

NCHI ya Tanzania hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...

  1. Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani); Tunaulizana Habari za Maji, Maharagwe na Mabarabara... Lakini hatuulizi Kabisa kama ipo Pepo; kama kwenda Mbinguni ziko ngazi ngapi? Tunaulizana ya kwetu yanataka Kura, sasa la Mungu mtalipigiaje kura ! Kwamba wengi wamekubali Mungu yupo kwahio yupo au hayupo?
  2. Dini; Mimi nina yangu Karume ana yake Kawawa na Waheshimiwa wengine, Waheshimiwa mbalimbali kila mtu ana yake... tunapokutana kwenye mikutano hatumuulizi leo Umesali ? Aa! Hiyo ni Hiari yake, kasali hakusali anajiuliza Mwenyewe.
Hapakuwa na mwanachama katika harakati za kuwaunganisha wananchi wa Tanganyika katika African Association ambae alikuwa na fikra ya kuwa hajui kuwa ‘’Mungu yupo au hayupo.’’

Sababu ya mimi kusema hivi ni kutokana na waasisi wa African Association wenyewe ambao wengi wao walikuwa Waislam.

Kusema maneno hayo hiyo ni kufru kubwa.

Wanachama walioasisi African Association mwaka wa 1929 ni hawa: Abdallah Kleist Sykes, Secretary, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu na Zibe Kidasi jumla yao watu sita.

Waliobakia watatu: Cecil Matola, President, Rawkesi Kusi na Rawson Watts hawa ni Wakristo.

Waislam ndiyo waliokuwa wanatawala siasa miaka hiyo na walikuwa wakianza mikutano yao yote kwa dua.

Huwezi kusoma dua ikiwa huamini kuwa yupo Mungu, muumba wa ardhi na mbingu na kila kitu kilichoma katika ya viwili hivi.

Kuonyesha nafasi ya Uislam katika siasa za Tanganyika ni kuwa baada ya kuunda African Association mwaka wa 1929 ili kuiweka African Association nje ya Uislam Kleist Sykes na Mzee bin Sudi wakaunda mwaka wa 1933 Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) Mzee bin Sudi akiwa President na Abdallah Kleist Sykes, Secretary.

Mkutano wa kwanza wa TANU ulihudhuriwa na hawa wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Sioni vipi watu hawa kama ninavyowafahamu wangekubali kusikia mtu katika chama chao anamkashifu Allah kuwa hana uhakika kama yupo au hayupo.

TANU isingekuwapo kama hii ndiyo ingekuwa sera yake.

Ningeweza kuweka mifano mingi ya kuwa TANU na waasisi wake pamoja na waliokiunga mkono waliamini Mungu.

TANU ilikuwa na dini na si tabu kutambua hili.
Angalia picha ya wanachama wa TANU wa miaka hiyo:

View attachment 2889767
Mkutano wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955 angalia kofia na kanzu.
View attachment 2889769
Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja angalia kushoto wanawake wamevaa mabaibui na wametengewa sehemu yao maalum ya kukaa​
We nae lijinga fulani alitumia akilia kutoa nchi kweny mikono ya kidini hasa hiyo dini uliyo itaja tungekuwa wajinga wa mwisho pia nchi ina mchanganyiko wa dini mbalimbali so ilikuwa jambo nzuri kuwa non secularism state ...uache ulofa mkuuu
 
Log...
Tatizo kubwa ninaloliona hapa JF ni kuwa wengi mnakuja hapa kupinganz na mimi mkitarajia kunishinda.

Hamkubali kuwa mimi ni kizazi cha hawa wazalendo na nimeishi ndani ya historia hii kwa hiyo naijua vizuri.

Lakini kubwa juu ya hayo nikaitafiti historia hii kuipa ithibati.
Mathalan hili la machifu na mafuvu limetoka wapi?

Nakuwekeeni hapo chini historia ya machifu na uhusiano wao na TAA Act. President na Secretary Abdul Sykes ili mtambue vipi siasa zilivyokuwa zinaendeshwa.

Aisha ''Daisy'' Sykes mtoto wa Abdul Syjes anaeleza aliyoyaona nyumbanin kwao utotoni kwake:

''Lakini kile ambacho kimeathiri fikra zangu na kubakia na mimi katika kumbukumbu zangu ni kufika pale nyumbani kwa uongozi wa juu wa Waafrika kabla ya uhuru, machifu kutoka makabila mbalimbali ya Tanganyika na viongozi wa vyama vya wazalendo vilivyokuwa ndiyo vinainukia, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi Waafrika katika wa serikali ya kikoloni.

Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani.

Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.

Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.

Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo.

Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.''

Kuna muabudu mzimu katika hawa watu walitajwa hapa kuanzia Abdul Sykes mwenyewe hadi Chief John Maruma?

TANU iliundwa na Waislam hapakuwa na nafasi ya imani yoyote ya ushirikina katika siasa zake.

Ikutoshe tu kuwa ndani ya TAA Political Subcommitee kulikuwa na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo.
1706873222850.png

1706873303121.png

Mbele kulia Chief Abdallah Said Fundikira, nyuma kushoto ni Abdulwahid Sykes, Tewa Said Tewa Hijja mwaka 1964​
 
Katika hawa machifu kuna yeyote muabudu mizimu?
Nadhani umeniqoute picha hazikuingia ila si neno tuseme wote waanzilishi na viongozi ni Dini moja..., Je Chama ni cha Viongozi na Waanzilishi Pekee ?

Je mtu akija muabudu mizimu akaomba kujiunga katika kujenga nchi yake asikubaliwe ? Kama Asikubaliwe kwa ajili ya Imani yake ya Kidini tukubali kina nani na tuache kina Nani ?

Je kujadili kwetu Imani zetu binafsi ambazo ni tofauti katika mustakabali wa Taifa badala ya kujadili mambo yanayotusumbua wote (Haki, Kuondoa Umasikini, Ujinga n.k.) huoni kwamba wangekuwa wanatumia muda kwa kufanya mambo ambayo yanaweza kufanyika kwa kila mmoja kwa wakati wake ?
 
Mimi sikukatazi kuwa na fikra ulizonazo wala sina sababu ya kuingia katika ubishi na wewe.

Mimi niko hapa kueleza historia ya wazee wangu na vipi walipigania uhuru wa Tanganyika.

Hapakuwa na Wapagani si katika uongozi au wanachama.
 
Log...
Logi...
Tatizo kubwa ninaloliona hapa JF ni kuwa wengi mnakuja hapa kupinganz na mimi mkitarajia kunishinda.
Duh Mkuu mimi kutoa Hii Hutoba sehemu kuleta hapa ni kutaka kupingana na wewe ? Mimi nimeweka andiko tena wapingaji wakija ndio vema sababu tutaongea kwa hoja na kuweka mambo kutokana na mitizamo tufauti na mwisho wa siku kuona Pro and Cons za yaliyosemwa...

Tena mkuu una bahati sana kama kuna watu wanakuja kabisa hapa ili wakupinge ningefurahia sana kama ningepata bahati hio ili wanipinge na mimi niweke Hoja zangu ambazo ni mitizamo tofauti huenda hata hao wanaonipinga wakaona mambo through my perspective au mimi nikaona through theirs hence kuelimika zaidi...
Hamkubali kuwa mimi ni kizazi cha hawa wazalendo na nimeishi ndani ya historia hii kwa hiyo naijua vizuri.
Moja mkuu assumption yako ni kwamba wote wanaokujibu unawafahamu sasa mkuu unajuaje hao wanaokujibu nao sio kizazi hicho ? Zaidi kabisa ni kwamba hata huyu aliyetoa hii Hotuba na yeye ni Kizazi hicho tena ni mmoja kati ya wahusika wakubwa (sasa na yeye haijui historia vizuri) Namzumgumzia JKN..., lakini mbali zaidi tuongelee validity ya alichosema na sio aliyesema....
Lakini kubwa juu ya hayo nikaitafiti historia hii kuipa ithibati.
Mathalan hili la machifu na mafuvu limetoka wapi?
Mkuu haukunielewa mimi ndio nimekuuliza wangekuja Machifu na Mafuzu kwenye huo Mkutano mgewafukuza ? Sababu kuamini kwao Mafuvu kunawaondelea kuwa Watanzania ?
Nakuwekeeni hapo chini historia ya machifu na uhusiano wao na TAA Act. President na Secretary Abdul Sykes ili mtambue vipi siasa zilivyokuwa zinaendeshwa.

Aisha ''Daisy'' Sykes mtoto wa Abdul Syjes anaeleza aliyoyaona nyumbanin kwao utotoni kwake:

''Lakini kile ambacho kimeathiri fikra zangu na kubakia na mimi katika kumbukumbu zangu ni kufika pale nyumbani kwa uongozi wa juu wa Waafrika kabla ya uhuru, machifu kutoka makabila mbalimbali ya Tanganyika na viongozi wa vyama vya wazalendo vilivyokuwa ndiyo vinainukia, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi Waafrika katika wa serikali ya kikoloni.

Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani.

Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.

Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.

Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo.

Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.''

Kuna muabudu mzimu katika hawa watu walitajwa hapa kuanzia Abdul Sykes mwenyewe hadi Chief John Maruma?
View attachment 2891778
View attachment 2891780
Mbele kulia Chief Abdallah Said Fundikira, nyuma kushoto ni Abdulwahid Sykes, Tewa Said Tewa Hijja mwaka 1964​
Sasa mkuu narudia tena kwa mara nyingine tena wangekuja waabudu mizimu wangefukuzwa ? Au niulize hivi kila aliyekuwa anafika mlangoni kwenu mlikuwa mnamuuliza Imani yake ?
 
Log...
Mimi sikukatazi kuwa na fikra ulizonazo wala sina sababu ya kuingia katika ubishi na wewe.

Mimi niko hapa kueleza historia ya wazee wangu na vipi walipigania uhuru wa Tanganyika.

Hapakuwa na Wapagani si katika uongozi au wanachama.
Kwamba TANU ilikuwa na DINI ? Ofcourse watu walikuwa na Imani zao kila mmoja kivyake lakini nakuuliza angekuja Mpagani asingepewa Kadi ? Kabla ya kupewa uanachama ulikuwa unaulizwa kama unamuamini Mungu au Hapana ?
 
Mohamed Said Nadhani ni vema badala ya kukujibu kama mimi nikujibu kama Hotuba inavyosema kama haujaisoma alafu uniambie ni wapi JKN amepotoka kuhusiana na Dini ya TANU

Chama chetu hakina dini. Kama Chama cha TANU, hakini dini. Ni Chama cha Siasa tu. Na hakina dini wala hakina Uhusiano na dini. Nitaeleza maana yake.

Vipo Vyama duniani vya Siasa lakini vina uhusiano na dini. Kwa mfano, sasa hivi katika nchi mbali mbali za Ulaya viko vyama si vidogo, vikubwa vinatawala, vinahusiana na dini. Ujerumani Magharibi kipo chama kinaitwa Christian Democratic Union. Ni Chama cha Siasa; lakini cha dini. Kinaitwa "Chama cha Demokrasi cha Kikristo". Italia wana cha namna pengine kama ningependa kutaja ningeweza nikavitaja. Chama umsingi wake wa Siasa yake ni dini — dini fulani. Kwa hiyo, ndiyo kusema nadhani, ndiyo kusema, kwa mfano, Ujerumani au Italia kama kungekuwa na Waislamu, na wao wangeweza wakaanzisha Chama chao — labda "Moslem Democratic Union"! Kwa msingi huo na wao vile vile wangeweza wakaanzisha chama chao cha Siasa lakini msingi wake dini. Chetu hakina. Hatuna msingi wa dini.

Kadhalika nchi yetu. Nchi yetu Tanzania haina dini. Hilo nalo naweza kuwasitusheni, lakini nitalieleza. Hatuna dini maana yake nini? Kwamba nchi yenyewe Tanzania haina dini. Kwamba tuulizwe "Dini ya Tanzania, dini rasmi ya Tanzania ni dini gani, tuitamke" — Aa hakuna, hatuna; nchi yetu haina dini. Uingereza ina dini rasmi; ina dini Dini ya nchi, inayokubaliwa na Katiba ya Nchi. Waingereza kwa Katiba ya Nchi ni Anglikani. Na kweli Mfalme wa Nchi sharti awe Anglikani. Na Wakubwa kubwa wa nchi vile vile wanaojulikana sharti wawe Anglikani. Lazima wawe wa madhehebu hayo. Wawe ni Wakristo lakini Wakristo wa aina fulani. Ni Waprotestant lakini Waprotestant wa aina -fulani. Hiyo ndiyo dini rasmi ya nchi. Wengine wanakubaliwa. Hawaharamishwi.' Kwa hiyo Mkatoliki anakubaliwa vile vile awepo na aabudu. Na Mprotestant\ wa madhehebu mengine mengine anakubaliwa awepo na aabudu. Lakini Ki-Katiba wanazuiwa wa madhehebu hayo kushika vyeo fulani fulani kwa sababu dini zao, madhehebu yao, madhehebu rasmi ya nchi. Hiyo ni ya testant.

Zipo za Kikatoliki. Nadhani Italia ni ya Kikatoliki rasmi. Dini ya Italia ni Ukatoliki- Ndiyo dini rasmi ya nchi. Wengine wanakubaliwa; kama wapo Wàprotestant wanakubaliwa; kama wapo Waislamu hawafukuzwi. Wanakubalika lakini hawakubaliki rasmi: kuna kazi fulani fulani za nchi hawawezi wakazifanya kwa sababu ya dini yaol Nadhani Pakistan ni nchi ya Kiislamu kwa Katiba — kwa katiba. Ni nchi ya Kiislamu kwa katiba. Kwa hiyo dini zingine zinaruhusiwa. Ukiwa Mkristo unaruhusiwa. Lakini Ki-Katiba ni Dini ya Kiislamu. Hivyo ndivyo ailivyo nchi nyingine.

Sisi hapana. Sisi hatuna. Sisi hatuna dini. Sisi nchi yetu haina dini. Sisi si nchi ya Kikristo; wala si nchi ya Kiislamu; wala si nchi Kiyahudi; sisi ni Tanzania tu. Ndiyo hivyo. Watanzania wenyewe wana dini. Watanzania wenyewe wana dini; nchi haina. Watanzania: Sheikh pale Mwislamu; Mama pale Mkatoliki; wengine huko wanajua wenyewe. Kila Mtanzania kila mmoja ana dini yake — yake. Mimi nina yangu. Sheikh ana yake hapa; hawa hapa, oh, mbalimbali hawa; mbalimbali, wakati wengine wala hatuwaulizi juu ya dini zao. Hatujui dini zao; kila mmoja anajua yake. Watanzania kila mtu ana dini yake. Na hazikatazwi, hazikatazwi na sheria ya nchi; madhali si dini zinazoleta ukorofi — ukorofi. Yapo madhehebu ya ukorofi ukorofi. Kuna madhehebu yanakataa serikali; yanasema kitu serikali ni haramu kinakatazwa na Mungu. Sasa hao wakorofi sana. Tunawakataza. Nadhani moja tumeiharamisha: tumeipiga marufuku kwa sababu ya ukorofi ukorofi wake. Kuna. madhehebu mengine wanasema Mungu aliumba•mtu hana nguo; kwa hiyo kwa nini kuvaa, na tutembee hivi hivi hatuna nguo. Hayo nayo tunaona wakorofi; aa dini za namna hiyo zinaweza zikatuletea taabu bure bure. Hizo tunaizuia kwa sababu huenda zikaleta fujo baina ya raia: zikaleta vurugu baina ya raia. Lakini kama dini haileti vurugu baina ya raia tunaikubáli. Tunaikubali lakini ni ya mtu, si ya nchi. Si ya nchi yetu ya Tanzania iwe ikiulizwa: Dini ya Tanzania ni nini? Inatamkwa! Au kwamba iko katika katiba! Hatuna. Hiyo hatuna,

Na hivyo hivyo kabisa kwa Chama chetu. Nataka kurudia tena Hatuna dini; hatuna kabisa Uhusiano na dini. lakini wenyewe mmoja mmoja tuna dini: Mimi nina yangu; Kawawa ana yake; Karume ana yake; Waheshimiwa mbali mbali kila mtu na yake. Lakini tunapokutana katika mkutano hatumwulizi: "Leo umesali?" Aa! Hiyo ni hiari yake kabisa. Kama kasali au hakusali anajiuliza mwenyewe; hatumwulizi sisi. Hatumwulizi dini yake; hatumwulizi kama ana dini au hana dini. Kabisa hatumwulizi. Kwa hiyo katika Chama chetu hatumwombi mtu awe Mkristo wala hatumwombi mtu awe Mwislamu.

Viko Vyama vinafanya hivyo. Vinasema: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — hiki ni chama cha Wakristo, wewe Mkristo?" Ukisema hapana, wewe huwezi kuingia! Au: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — chama hiki ni cha Waislamu; wewe ni Mwislamu?" Ukisema hapana, wewe huwezi kuingia, Au vingine vinasema: "Wewe unataka kuingia katika Chama chetu — chama chetu hakikubali dini; wewe nawe unakataa dini?" Ukijibu: "Mimi naamini dini"; basi wewe huwezi kuingia. Viko vyama vya namna hii ambavyo ili uingie katika chama sharti useme: hakuna Mungu!"

Sisi hatuulizani habari hizo. Katika Chama chetu cha TANU hatuulizi habari za Mungu. Kichama hatujui kama Mungu yupo au hayupo. Si jambo tunalolizungumza katika Katiba: "jamani Mungu yupo?" Hatuulizani kabisa. Tunauliza habari za maji, na maharagwe, na mabarabara... Lakini hatuulizi kabisa kama iko pepo; kama kwenda mbinguni ziko ngazi ngapi? Hatuulizani hilo. Maana mambo tunayoulizana ya kwetu ndiyo yanataka kura. Tunapiga kura. Sasa la Mungu mtalipigiaje kura! Kwamba wengi wamekubali kwamba Mungu yupo kwa hiyo Mungu yupo. Au wengi wamekataa kwamba Mungu hayupo...! Hilo hatujui sisi. .Vyama vingine vinajiingiza katika mambo haya ya kuamua: waamue kichama kama Mungu yupo; au waamue kichama kwamba hakuna Mungu. Sisi hatufanyi hivyo. Halituhusu kabisa kabisa. Hatumwulizi kabisa mwanachama wetu. Akiwa Mwislamu tutamkubali; kama ni Mkristo tunamkubali; kama unaabudu mizimu, Mzanaki wa hivi hivi tu — "non-aligned" tunamkubali. Hata kama ni "atheist" anayekana Mungu, tunamkubali. Anayesema: "hakuna Mungu", kwa sababu hilo si jambo linalozungumzwa katika Chama hiki.

Madhali hatumwulizi dini; madhali hatumwulizi Uislamu wake; hatuulizi imani yake kwa namna yoyote. Kwa hiyo wakuu wa dini wasishangae kuona Sisi tumechanganyika katika Chama. Waislamu humo humo — tena Waislamu wote basi: WaSunni, Wa-shia, Wa-Kadiani — wote, Wakristo wa Madhehebu yote. Na, hao wasiokuwa Wakristo nao wa madhehebu yote: wanaoabudu vibuyu, wanaoabudu mwezi, wanao... wote tunawakubali,

Hilo, nasema lilikuwa jambo la kwanza kulieleza. Na tunafanyå hivyo kwa kuamini kwamba hivyo ndivyo sawa. Tunafanya hivyo kwa kuamini kwamba hivyo ndivyo sawa. Haifai Nchi iwe na dini inaitwa rasmi. Tunasema nchi inapokuwa inachagua dini, inaifanya rasmi, inadhalilisha dini zingine. Na si kazi nchi kufanya hivyo. Inawatia raia wa dini zingine unyonge wa bure. Kwa hiyo raia lazima wote wawe sawa. Na nchi ikija kuchagua dini imewafanya raia wake hawatakuwa sawa Raia wa dini fulani watakuwa ni bora kuliko. raia Ya dini zile ambazo hazikuchaguliwa.

Kadhalika Chama chetu tunaona ni sawa kwamba iwe hivyo, kwamba chama chetu hakina: dini, hatutaki kukiingiza katika mambo. ya dini, Lakini• Chama. chetu kinatetea haki ya kila mtu kuabudu. kwa kadiri ya Imani yake. 'Hilo tunalikubali na kuona kwamba ni la maana.

Ndugu yangu, pamoja ya kwamba sijamaliza kusoma maoni yako lkn kwakuwa mwanzoni tu nimeona makosa yako.... kinadharia wanasema ukikosea mwanzoni utapata majibu yenye makosa mwishoni.

Napenda usome kwa majini maneno haya ya nyerere.

NCHI ya Tanzania / TANU hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani);

Kwa ufupi hapa Nyerere alikuwa unazungumzia kuhusu dhana na asili ya itikadi ya Usekyula.

Ktk theologia ya Secularism wanasema; waanzilushi na waumini wa imani ya Usekyula.

1. Hawana uhakika kwa uwepo wa Mungu. Hii ni imani moja wapo wa Atheism wenye msimamo wa kati.

Lkn kuna Atheism wenye msimamo mkali wao wanasema Secularism ni kuwa na yakini kuwa Mungu hayupo, mungu kauwawa.

Kwa hiyo.

Itikadi ya kusekyula aliyoisimika Nyerere ilikuwa na lengo la kuwafanya watz waislam wasiwe waislam na wakristo wasiwe wakristo.

Lkn kubwa jiulize.

Kwanini atheism (Secularism) walazimishe imani yao iwe ya watz.

Na kulazimisha UTAMADUNI wao uwe juu ya SHERIA za watz.
 
Kwamba nimekosea Ku-attach hio PDF sio ya Hotuba au ya sio ya JKN ? au niliochoqoute kwa ufupi kwa ambao hawajasoma PDF nimepotosha ? Nadhani cha maaba ni kuonglea ujumbe aliotaka kuuweka katika hili suala la Kwamba CHAMA / NCHI hakina DINI rasmi kwahio hapa tukiongelea tija au mapungufu ya kwenda njia hio nadhani ndio jamba la maana na sio semantics za Usekyula au lack of thereof... kwa kwenda huko hata kina JKN wangejikita huko na sio kuzungumzia Maharage, Maji na Mabarabara.....
Napenda usome kwa majini maneno haya ya nyerere.

NCHI ya Tanzania / TANU hazina Dini; Wananchi ndio Wana Dini...Kichama / TANU Hatujui kama Mungu yupo au hayupo (Hatuulizani);

Kwa ufupi hapa Nyerere alikuwa unazungumzia kuhusu dhana na asili ya itikadi ya Usekyula.

Ktk theologia ya Secularism wanasema; waanzilushi na waumini wa imani ya Usekyula.

1. Hawana uhakika kwa uwepo wa Mungu. Hii ni imani moja wapo wa Atheism wenye msimamo wa kati.

Lkn kuna Atheism wenye msimamo mkali wao wanasema Secularism ni kuwa na yakini kuwa Mungu hayupo, mungu kauwawa.
What has this got to do with anything ? Kwamba anayeabudu Mungu Nusu, Robo au anayeabudu Mizimu inaingiaje kwenye Mjadala wa watu ambao hawajadili suala hilo ? ni Kwamba uamuzi ni either kuweka Imani kwenye Menu au Imani kuwa kigezo cha wanaokutana au kutokuwa Kigezo hivyo kila ajaye na aje sababu kinachowaunganisha sio Imani yao.......
Kwa hiyo.

Itikadi ya kusekyula aliyoisimika Nyerere ilikuwa na lengo la kuwafanya watz waislam wasiwe waislam na wakristo wasiwe wakristo.
Kwamba wakijunga TANU au wakiwa wa-TANZANIA under Nyerere wasiende kwenye Ibada zao ?
Lkn kubwa jiulize.

Kwanini atheism (Secularism) walazimishe imani yao iwe ya watz.

Na kulazimisha UTAMADUNI wao uwe juu ya SHERIA za watz.
Kwamba!!! wamelazimisha wapi ? Sheria Ipi ya Watanzania aliyoivunja Nyerere kwa kusema alichosema ? Utamaduni wao kina nani na Utamaduni wao Upi ?!!!!;
 
Tanzania udini upo toka kipindi cha Nyerere Uislam na Ukristo.

Nyerere alikuwa tapeli
 
Back
Top Bottom