Ujamaa wa CCM Uko Wapi?

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Wakuu heshima kwenu.

Ninalazimika kuhoji kwa sauti kubwa UJAMAA wa CCM uko wapi? Hoji yangu hii imetokana na ukweli kwamba CCM wanajitambulisha kama chama cha kisiasa cha kijamaa. Lakini wakati huo huo kinatekeleza siasa za kibepari ambazo zimewafanya wanyonge wengi wakibaki masikini wa kutupwa na matajiri (mafisadi) wakiendelea kupata utajiri wa kupindukia.


Ninahoji sasa na ninaomba kusaidiwa kuhusu utata huu; kwamba kila siku rasilimali za nchi zinaporwa na wageni na wajanja wachache kutokana na siasa za CCM. Njia kuu za uchumi zimekamatwa na watu wachache tena wengi ni wageni.
Mwl. Nyerere alitaifisha miradi ya watu binafsi ili iendeshwe na serikali. Hii ilifanywa kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa siasa za Ujama. Viongozi waliomfuatia wameuza mashirika aliyoyaanzisha Mwl. Nyerere na sasa sisi tumekuwa soko la ughaibuni. Huu Ujamaa wa CCMuko wapi?


Kama huu ni uongo je kwa nini CCM na wenyewe hawaoni vibaya kujidanganya na kudanganyika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom