kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,378
- 17,000
Tangu tupate uhuru tumesema sisi tunajenga nchi ya ujamaa na kujitegemea, na hatukuwahi kusema kuwa sasa tumeachana na ujamaa na kujitegemea tunageukia ubepari. Tunataka kila Rais wetu ajue hivyo. Ujamaa una misingi yake na ubepari una sura na misingi yake. Mfano, kuchukua ardhi iliyoko kwenye kabila moja na kuwapa kabila lingine bure ni sura ya ujamaa.
Kama Rais Samia hatasisima imara dhidi ya wahuni historia inaweza kumkumbuka kama Gorbachev wa Tanzania.
Urusi chini ya Soviet ilikuwa imara kwa kila kitu kuliko China lakini China sasa ni imara kuliko Urusi kiuchumi hata kiulinzi kutokana na makosa ya Mikail Gorbachev. Urusi ya sasa inamlaani Gorbachev kwa kuandika Katiba iliyosababisha muungano wa Kisoviet kuanguka na sasa Urusi ni dhaifu, na wahuni wanatishia kuichukua kabisa yote. Kama sio akili za Putin sasa hivi wahuni wa magharibi wangeshazigawana rasilimali zote za Urusi na kuwa zao. China imejifunza kutokana na makosa ya Soviet ndiyo maana hawataki majimbo kama ya Tibet na Taiwan yajitenge na kuyafanya majimbo mengine yaige mfano wao. India ndiyo maana hawataki tena Kashimir ijitenge kama yalivyofanya majimbo mengine kama bangaladesh na mengine.
Wachina na Warusi na Nyerere sio wajinga kiasi hicho kuukumbatia ujamaa. Nchi yetu bado ina wajinga na maskini wengi sana, hebu twendeni taratibu. Uchumi wetu bado ni mdogo sana kumudu kugharamia demokrasia kama ya Marekani; tutadumaa kwelikweli kama tutapanua demokrasia ikawa pana sana kama ya magharibi. Marais wetu waliotangulia sio kwamba walishindwa kuandika katiba mpya, lakini walihofia kuwa Gorbachev wa tanzania, chama na nchi vikawafia mikononi mwao.
Pale Kenya kila wiki wanagoma na kuandamana kisa wanayo katiba inayoruhusu kufanya hivyo. Katiba ambayo haiongezi value yao kimaisha na uchumi wa nchi. Ukabila na kutekana kumebaki kulekule mpaka sasa ingawa wanayo katiba ambayo inaweza kuufutilia mbali uchaguzi na kuanza upya.
Tanzania hatuna uchumi unaoruhusu kuufuta uchaguzi woote na kurudia tena upya huku wanafunzi wakiwa hawana fedha ya mikopo na madarasa hayana madawati.
RAIS SAMIA anaweza kuwa Gorbachev wetu kama atakubali kuandika Katiba pana yenye Tanganyika, mgombea huru, tume huruuuuu, na madaraka ya rais yaliyopunguzwa sana. Nchi itasambaratika kwenye awamu yake. Tunamuomba aiche nchi kama alivyoiacha Magufuli, Nyerere na marais wengine kwakuwa muda wa watanzania kuwa huru kama raia wa Marekani na Ufaransa bado, bado kuna wanaojisaidia vichakani mpaka leo wanohitaji kulelewa na mfumo wetu huu wa kijamaajamaa. Bado kuna makabila hayana ardhi ambayo wanahitaji mfumo huu wa kupewa ardhi na Rais hata kama iko kwenye makabila mengine.
Sisi ni wajamaa tangu tupate uhuru ndiyo maana hata wachagga na waarusha wenye shida ya ardhi kwao wanaweza kuhamia popote nchini bila usumbufu, huko Kenya huwezi kufanya jambo kama hilo kwakuwa wao ni mabepari tangu awali na wanashinikizwa na mabepari kufuata mfumo huo kwa lazima hata kama hawataki. Hatuwezi kuwaiga wao kwa lolote lile maana hawana kizuri cha kujifunza kutoka kwao. Bila kuwa na nguvu alizokuwanazo Magufuli Kikatiba asingeweza kujenga bwawa lile la umeme na SGR, na wazigua wangepinga ardhi yao kupewa Wamasai wa Ngorongoro. Wapinzani wangempinga na mahakama ingemkwamisha Magufuli kujenga bwawa, reli au kuhamia Dodoma kwa nguvu kama alivyofanya Magufuli. Tutadumaa kwelikweli.
Vurugu za Oct29 kiukweli hazikutokana na madai ya Katiba mpya, ila waliopanga vurugu zile waliwajumuisha tu pamoja watu wanaodai Tanganyika (G55) na wale wanaodai tume huru ya uchaguzi (wapinzani). Chanzo halisi cha vurugu zile ni wale wale waliotaka Rais Samia asiwe Rais baada ya kifo cha Rais JPM kwa sababu zao. Na ni haohao ambao hawakutaka agombee uchaguzi wa 2025. Kundi hili kwasasa halina nguvu na pengine limeshaachana na madai yao kwakuwa lilishindwa mara mbili kumzuia mama asiwe Rais na asigombee 2025. Kundi hili sasa labda linajipanga kuandaa mgombea wao kwenye uchaguzi wa 2030 ndani ya CCM kwa kutumia Katiba hiihii na tume hiihii.
Kelele za sasa za Katiba mpya ni za wale wanaodai Tanganyika na wanaodai Tume huru ya uchaguzi ambao walikuwa wamejibanza kwenye kundi la wanaCCM ambao walikuwa hawapendi Rais samia awe Rais. Wanatumia sasa vurugu zile ambazo hazikuwa za kwao peke yao kumchomekea Mama na CCM agenda zao za Katiba mpya yenye Tanganyika na Tume huru ya Uchaguzi. Makundi haya mawili moja linataka Tanganyia zaidi na la pili linataka tume huru zaidi. Kundi la tanganyika liko tayari kulisaidia kundi la tume huru hata kwa kubadilisha kifungu hicho tu cha tume kwanza kabla ya uchaguzi wa 2029 na 2030 kuonyesha kuwa katiba hii hata wao wanaitamani sana ispokuwa kwenye kipengele cha tume huru ya uchaguzi na tanganyika. Maana yake hata wao kama wataingia madarakani hawatakuwa na haraka ya kuandika katiba mpya maana katiba hii ni tamu sana kwa watawala.
CCM ni replica ya chama cha ki communist cha China, hivyo lazima ki behave kama chama cha ki communist la sivyo nchi hii itasambaratika kama ilivyosabaratika Soviet union. Na hii ndio sababu ya Mwl. Nyerere kusema bila CCM imara nchi itayumba. Masalia ya G55 ya akina Jenerali Ulimwingu na Warioba yameibuka kudai tanganyika kwa kutishia eti bila katiba mpya hali itakuwa mbaya zaidi 2030; uongo;
CCM bado inao wajibu wa kuilea nchi hii hadi pale kila mtanzania amepata elimu, afya, chakula, mahali pa kulala, umeme, maji safi, barabara, kumiliki kipaande cha ardhi yake na umbali mfupi wa kupata huduma. Katiba hii ndiyo yenye uwezo wa kufikia haraka mambo haya yote kama rasilimali zetu zitavunwa, kusindikwa, kusimamiwa na kusambazwa kwa wananchi kwa usawa (equitably). Kazi yetu kuu ni kuwa makini na uteuzi wa viongozi makini na wazalendo kwa nchi yao.