UJAMAA: Mfumo rafiki kwa maendeleo ya Tanzania. China imeendelea kwa sababu ya ujamaa uliopo mpaka sasa

Watanzania tuna kasumba ya kuuangalia ujamaa kwa jicho la ubepari na kuona ujamaa ni mfumo usio na maslahi yeyote kwa jamii. Vipi kuhusu ubepari unatengeza matabaka ndani ya jamii, una maslahi gani? Kushindwa kuutazama ujamaa kama ujamaa na badala yake ukatumia jicho la kipebari kuutazama ujamaa, hapo utaona kile usichokuwa nacho ni bora Zaidi kuliko ulichonacho( kwa sababu ulichonacho umekizoea)

Tunapozungumzia ujamaa duniani, tunazungumzia falsafa za Karl Marx na nchi mfano iliyofanikiwa kukuza na kuendeleza ujamaa kufikia mafanikio ya juu kabisa ni China. Ni wachache sana baina ya watanzania walioisoma historia halisi ya China, wengi historia ya china wanaisoma mitandaoni ambayo si historia ya China kweli ila ni ya Mmarekani(google na internet ni marekeni) hivyo Marekani inaweza kuitengeneza historia ya china kwa kadiri inavyojisikia. Si historia ya China tu bali hata ya Afrika inaweza kuitengeneza atakavyo.

Kusema Ujamaa hauna manufaa, mmeona China walichofanya ndani ya muda wa miaka 30 walipotoa azimio la maendeleo ya China miaka ya 1980? China leo imekuwa great power na sababu ni kuendeleza na kudumisha historia ya mchina hususani kuendelea na mfumo wa kijamaa.

Ni mfumo ambao china imeona unafaa kwa maendeleo na imethibitika ni kweli unafaa sana.
Leo mtanzania ukimuuliza CHINA ni mbepari au mjamaa? Karibu 80% watakuambia China ni mbepari, ni kwa sababu wanauangalia ujamaa kama ubepari na wameathiriwa na historia za mitandaoni ya ujamaa. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, mitandao na google ni mmarekani hivyo marekani itatumia kila njia kuusema vibaya ujamaa ili usienee na kuwa tishio la ubepari. Hawataki kuamini kuwa ujamaa unaweza kujenga uchumi imara na wanaogopa ujamaa unaweza kuwa tishio la ubepari.

Ili kujiridhisha ukweli wa nisemayo, kitabu cha XI JIPING- THE GOVERNANCE OF CHINA kimeeleza kila kitu na mfumo ambao china unatumia ambao ni SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS. Kama Rais wa China na Katibu mkuu wa CPC ( chama pekee kikubwa china) anasema ataiongoza CHINA katika ujamaa, inakuwaje mbepari aseme china ni mbepari? Hii ni hofu ya ubepari dhidi ya ujamaa.

Katika kitabu hicho XI JIPING anaendelea kusema kwamba wataendelea kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa lengo la kuendeleza na kukuza demokrasia. Hii kauli inathibisha uongo wa mabepari na washirika wake kuwa ujamaa hakuna demokrasia. Kama demokrasia ni vyama vingi, China ina demokrasia ya mfano lakini CPC ndio chama kikuu kama ilivyo CCM kwa Tanzania.

China hakutaka kujiingiza mzimamzima katika mfumo wa kibeberu ila alikuwa anatafuta njia yake ya kupita kwa kuuboresha mfumo wa kijamaa ambao SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS ndio mfumo wao na ni mpya kabisa. Njia ambayo wamepita ni salama kwa maendeleo yao.

Tanzania tunaweza kujifunza kitu kutokea China, mfumo wa kibeberu umekomaa sana kiasi cha kufanya nchi za Afrika kushindwa kuendana nao. Turudi kwenye historia yetu na kurekebisha falsafa za mfumo wetu wa zamani kama walivyofanya China, Nina hakika maendeleo yatakuja kwa kasi sana. Ninaamini siku moja Afrika ikisimama na kupita njia yake nje ya ubepari na ujamaa au kufuata ujamaa kwa sababu ni mchanga na hujakomaa sana, ndio siku ubepari utakufa.

Msiangalie ujamaa kwa kuiangalia Korea Kaskazini, ule ni udikteta. Uangalie ujamaa wa China ambao umeibadilisha China kwa muda mfupi sana na kuendeleza historia ya China.
Mimi pia ni muumini mkubwa wa usoshalisti ambao good practice yake iko Slovenia, Israel, Sweden... China wana ujamaa mchanganyiko.

Kwa Tanzania kuna watu Mwl. Nyerere aliwapa kuuhubiri ujamaa, wakauelekeza kwa model mbaya ndiyo maana uka-fail.
Nchi kama Israel uchumi wao mpaka miaka ya 2000 mwanzo ulikuwa umejengwa kwenye ujamaa wa aina mbili. Kubbutz na Moshav... hawa walikuwa wana-control uchumi by 60% kabla ya watoto wa kizazi cha 3 kuachana na huo mfumo na sasa kuna reforms. Ila umewaunganisha sana kiuchumi na kijamii.

Haina maana tunaishi na Indians community wachache sana, ila wana-control uchumi wetu kwa biashara, viwanda... kila fursa wana nafasi ya ku-grab simply wana akili sio nyingi sana na Cash...

Sisi wengi tuna akili ila hatuna Cash... eventually, kila fursa wamo. Indians wana-control biashara ya agro-inputs, wana-control biashara ya korosho, choroko, dengu, ufuta, mafuta ya kula, sukari...Indians wa hapa East Africa wana ka-ujamaa fulani na kuna wahindi wanakuja hapa choka mbaya, eventually wanapanda mpaka kuwa na hela.

Sisi, kuna deals unaweza kuomba hata ya ku-supply chochote kile ili ujenge uwezo... watu wa procurement wako radhi kumpa wa kuja ila wapate cha juu (aka 10%)...
Tungeishi kijamaa, na tukajenga uchumi wa kijamaa, sio kila kitu ni cash, vingine ni government legal endorsement ili kuwekeza...

Anyway, Mungu msaidie namba moja aone namna Nyerere alikuwa na TASWIRA ya ujamaa, na kwa rasimali chache sana alifanya makubwa yaliguza maisha ya watu na kukuza maendeleo ya watu.. (Human development through economic development)... hata tax base inakuwa...

Hivi mfano bajeti ya leo... Prof. Mpango... kwanini asitoe call kwa Watanzania wenye strategic buz plans waje na soluhisho la kukuza agro-processing ya Korosho...kuongeza exports za processed korosho
Kwanini asije na call ya kupunguza deficit ya samaki tani 400 annually;
Call for strategic solution ya kupunguza imports ya madawa ya hospitali... jamani hata panadol, folic acid... nazo mpaka tununue India...

Huenda ipo siku Mkulu akatafuta na watu wa kitaa including few JF thinkers tukampa sio malalamiko ya kodi ila mikakati ya kutekelezeka ya kukuza exports na kupunguza imports kama namna ya kukuza biashara ili kuongeza tax base na kuongeza capacity ya watu kuzalisha katika organized systems...
 
Ramat Yohanan is a kibbutz in northern Israel.... In 2017 it had a population of 969.In 2014, Forbes Israel ranked the Kibbutz as the 6th richest in Israel with an estimated value of 250 million Shekels... (wanakijiji wajamaa 1000 mathalani uchumi wao unakuwa sawa mapato na TZS bil160)

tatizo la hapa kwetu huenda kuna watu katika decision making organs hata hawajui dhana na falsafa ya ujamaa ambao kama tunau-custumize katika mazingira yetu tunafika wapi...

It is unfair, tuna pamba, tunaagiza uniform za wanajeshi, watoto wa shule uchina. Wajamaa wangefanya all it take processing ifanyikie ndani, uniform ushonewe ndani fedha zibaki hapa...

It is unfair hata maji ya hospitali IV fluids tuna-import wakati maji yapo, viwanda vinauzwa... wajamaa wangetoa equipment purchase kwa mkopo ili mauzo ya vifaa tiba including IV fluids vitengenezwe kwa soko la ndani...

Anyway... Mungu yupo... ipo siku watatuelewa tu...
 
Mimi pia ni muumini mkubwa wa usoshalisti ambao good practice yake iko Slovenia, Israel, Sweden... China wana ujamaa mchanganyiko.

Kwa Tanzania kuna watu Mwl. Nyerere aliwapa kuuhubiri ujamaa, wakauelekeza kwa model mbaya ndiyo maana uka-fail.
Nchi kama Israel uchumi wao mpaka miaka ya 2000 mwanzo ulikuwa umejengwa kwenye ujamaa wa aina mbili. Kubbutz na Moshav... hawa walikuwa wana-control uchumi by 60% kabla ya watoto wa kizazi cha 3 kuachana na huo mfumo na sasa kuna reforms. Ila umewaunganisha sana kiuchumi na kijamii.

Haina maana tunaishi na Indians community wachache sana, ila wana-control uchumi wetu kwa biashara, viwanda... kila fursa wana nafasi ya ku-grab simply wana akili sio nyingi sana na Cash...

Sisi wengi tuna akili ila hatuna Cash... eventually, kila fursa wamo. Indians wana-control biashara ya agro-inputs, wana-control biashara ya korosho, choroko, dengu, ufuta, mafuta ya kula, sukari...Indians wa hapa East Africa wana ka-ujamaa fulani na kuna wahindi wanakuja hapa choka mbaya, eventually wanapanda mpaka kuwa na hela.

Sisi, kuna deals unaweza kuomba hata ya ku-supply chochote kile ili ujenge uwezo... watu wa procurement wako radhi kumpa wa kuja ila wapate cha juu (aka 10%)...
Tungeishi kijamaa, na tukajenga uchumi wa kijamaa, sio kila kitu ni cash, vingine ni government legal endorsement ili kuwekeza...

Anyway, Mungu msaidie namba moja aone namna Nyerere alikuwa na TASWIRA ya ujamaa, na kwa rasimali chache sana alifanya makubwa yaliguza maisha ya watu na kukuza maendeleo ya watu.. (Human development through economic development)... hata tax base inakuwa...

Hivi mfano bajeti ya leo... Prof. Mpango... kwanini asitoe call kwa Watanzania wenye strategic buz plans waje na soluhisho la kukuza agro-processing ya Korosho...kuongeza exports za processed korosho
Kwanini asije na call ya kupunguza deficit ya samaki tani 400 annually;
Call for strategic solution ya kupunguza imports ya madawa ya hospitali... jamani hata panadol, folic acid... nazo mpaka tununue India...

Huenda ipo siku Mkulu akatafuta na watu wa kitaa including few JF thinkers tukampa sio malalamiko ya kodi ila mikakati ya kutekelezeka ya kukuza exports na kupunguza imports kama namna ya kukuza biashara ili kuongeza tax base na kuongeza capacity ya watu kuzalisha katika organized systems...
umeusema ukweli wote, ujamaa sio mfumo mbaya ila waliotakiwa kuutangaza waliutangaza vibaya labda kwa kukosa elimu au kutoujua vema. Mambo mengi yanahitaji elimu kufanikiwa na kwa kipindi hiko wasomi walikuwa wachache ambao walikuwa wanaenda kusoma nchi za kibepari na wanaporudi wanahubiri ubepari na kuachana ujamaa, hii ikazidi kuua ubepari.

kuna vitu vingi kwa nchi yetu hatuwezi kuruhusu sekta binafsi iwe na control navyo kwa wingi kama maji, umeme, elimu na huduma za afya. serikali inabidi iwe na control kubwa ya hadi 80% ya huduma hizo ili kuendelea kuleta haki, usawa katika jamii la sivyo watu maskini watakosa huduma hizo. hii ndio kanuni kuu ya ujamaa" major means of production are owned by the public"
 
Hao Wachina uchumi wao unaendeshwa kibepari kwani makampuni mengi ya Ulaya yamewekeza huko sababu ya soko kubwa ila ujamaa walionao ni kwenye siasa tu kwa chama cha kikomunisti kushika hatamu.
Nani kasema ujamaa hauruhusu makampuni binafsi kuwekeza ?
 
umeusema ukweli wote, ujamaa sio mfumo mbaya ila waliotakiwa kuutangaza waliutangaza vibaya labda kwa kukosa elimu au kutoujua vema. Mambo mengi yanahitaji elimu kufanikiwa na kwa kipindi hiko wasomi walikuwa wachache ambao walikuwa wanaenda kusoma nchi za kibepari na wanaporudi wanahubiri ubepari na kuachana ujamaa, hii ikazidi kuua ubepari.

kuna vitu vingi kwa nchi yetu hatuwezi kuruhusu sekta binafsi iwe na control navyo kwa wingi kama maji, umeme, elimu na huduma za afya. serikali inabidi iwe na control kubwa ya hadi 80% ya huduma hizo ili kuendelea kuleta haki, usawa katika jamii la sivyo watu maskini watakosa huduma hizo. hii ndio kanuni kuu ya ujamaa" major means of production are owned by the public"
Mkuu mambo mengine sio rocket sc. kabisa...
Tunasomesha watoto wetu kwa bil zaidi ya 300 kwa mwaka ambapo majority wana-drop out kwa la 7, form IV & VI
... then tunakopesha vijana wetu kwenda vyuo vikuu halafu wanatoka kazi hakuna...

Wakati huo tuna import maziwa worth 50bil to 160 bil... Bakhresa mwenyewe ana import maziwa zaidi ya lita 100 kwa siku kwa ajili ya kiwanda chake...

Good practice ya ujamaa ilikuwa kutoa soft loan ili kujenga mfumo wa kuwa na viwanda ili kuajiri hao vijana wakitoka chuo wapate ajira na kurejesha mikopo. Waziri hana majibu mikopo ya hawa watoto inarudi vip...

Good practice ningemwelewa waziri kama angetoa soft loan ili vijana wamiliki viwanda vya kutengeneza pedi za watoto wetu wa kike na pampas.... kwa namna hiyo tuna-cut down deficit ya huo mzigo hela inabaki ndani na mkopo unarejea huku vijana wameajiriwa...
Ni Watanzania wangapi wana uwezo kuanzisha viwanda kwa hela zao mfukoni very few... ila tupo Watanzania ambao tuna workable business models ambazo by more 80% zitarejesha mkopo kwa muda mfupi...

Usoshalist umejikita kwenye kutatua matatizo ya kijamii kibiashara ambapo it works in benefit of the citizens and the government...

Sipendi kuona ujamaa ni wakati wa matetemeko tunakuwa na hela au kama MV Ukara tunakuwa na hela... ujamaa unatutaka kukabili umasikini na ujinga kwa pamoja wakati wote...

Nyerere alisema, Tanzania haitakuwa huru kama jirani bado wapo colonized... inavunja moyo wapigiwa kura wetu wanaishi kwa neema na waajiri ambao ni wapiga kura wana akili ya kuja na solutions halafu baadhi ya wapigiwa kura hata hawataki kutusikiza wapiga kura... hili haliko sawa
 
Changamoto zipo ila ujamaa ni mzuri sana kama utatamalaki katika nchi
 
China ni Mabepari wanaosimamiwa na Chama cha kikomunisti. Kuwepo na mfumo wa chama kimoja cha siasa si ishara ya ujamaa. Unaweza kututofuatishia Kanuni za kibepari na zile za kijamaa na uoneshe China ya sasa inafuata kanuni zipi?
kanuni kubwa inayotofautisha kati ya ujamaa na ubepari ni " ownership" au umiliki wa rasilimali, huduma na watu na " distribution" au utolewaji wa rasilimali watu na huduma. Kanuni nyingine za kutofautisha ubepari na ujamaa zinaweza kuingiliana.

katika ubepari, huduma muhimu zinamilikiwa na kusambazwa kwa wingi na sekta binafsi" major means of production and distribution are owned by private sector". kwa maana kwamba watu binafsi ndio watoaji wa huduma muhimu kama maji, umeme , afya n.k

wakati katika ujamaa, huduma muhimu zinamilikiwa na kutolewa/kusambazwa kwa wingi na sekta ya umma( serikali)" major means of production and distribution are owned by public sector".

ila kuna ukosefu wa elimu ambao ulikwamisha malengo ya ujamaa. hakuna mfumo wowote ambao sekta binafsi au sekta ya umma unamiliki njia zote za uchumi wenyewe. Marekani yenyewe sio "pure capitalst" kwa maana ya kwamba serikali inamiliki kidogo na sekta binafsi ndio inamiliki sana.

woga wa watanzania juu ya ujamaa ulitokana na upotoshaji wa kuilinganisha " socialism" na " communism" . Katika " communism" ndio serikali inamiliki kila kitu na kunakuwa na "equal distribution of resources" ila katika socialism sio hivyo. ninachotaka kiwepo ni "ushoshalisti na sio ukomusti"
 
Twende taratibu kidogo. Mtoa kama una akili timamu ukiruhusiwa kuchagua nchi ya kwenda kuishi kati ya zile za magharibi US , Uingereza , German, Sweden n.k pamoja na China unaweza kwenda China kweli?
 
Twende taratibu kidogo. Mtoa kama una akili timamu ukiruhusiwa kuchagua nchi ya kwenda kuishi kati ya zile za magharibi US , Uingereza , German, Sweden n.k pamoja na China unaweza kwenda China kweli?
nitaishi katika nchi niipendayo kuliko zote duniani( Tanzania)
 
Unasoma ujinga halafu unauleta humu? Ujinga ni MZIGO MKUBWA SANA.
Sikutaka kusoma mambo ya china kwenye mitandao ya Marekani na ku- balance stori nikasoma kitabu kujua ukweli, sikuwa biased kushupaa na nisichokijua. Hii ndio sifa ya mjinga( according to Prof.Kabudi)
 
Back
Top Bottom