UJAMAA: Mfumo rafiki kwa maendeleo ya Tanzania. China imeendelea kwa sababu ya ujamaa uliopo mpaka sasa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,361
2,000
China ni wajamaa mabepari kama ulikua hujui ujamaa kamili government ownership inakua 100% mpaka maduka hata ya mkorogo lakini china kuna wawekezaji kutoka ulaya marekani nk...sasa labda tuseme china wana mixed economy
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669

na ubepari kamili , sekta binafsi inamiliki 100% ya njia za uchumi na usambazaji yaani sekta binafsi itamiliki mpaka mifumo ya jeshi, ulinzi wa bahari, barabara zote, madaraja yote, njia zote za mawasiliano, nishati yote na reli zote. mbona marekani wanajiita mabepari kama sekta binafsi haina umiliki wa 100%? Mixed economy ni ujinga ulianzishwa na marekani kuua ujamaa duniani,
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
111,037
2,000
Weye ni kamongo akili kushikiwa nani kakwambia ili kujua kama ujamaa bado uko China inabidi usome mitandao ya Marekani!?

Akili za wapi hizi!? 😂😂😂

Sikutaka kusoma mambo ya china kwenye mitandao ya Marekani na ku- balance stori nikasoma kitabu kujua ukweli, sikuwa biased kushupaa na nisichokijua. Hii ndio sifa ya mjinga( according to Prof.Kabudi)
 
mwanza

JF-Expert Member
May 7, 2009
761
500
Watanzania tuna kasumba ya kuuangalia ujamaa kwa jicho la ubepari na kuona ujamaa ni mfumo usio na maslahi yeyote kwa jamii. Vipi kuhusu ubepari unatengeza matabaka ndani ya jamii, una maslahi gani? Kushindwa kuutazama ujamaa kama ujamaa na badala yake ukatumia jicho la kipebari kuutazama ujamaa, hapo utaona kile usichokuwa nacho ni bora Zaidi kuliko ulichonacho( kwa sababu ulichonacho umekizoea)

Tunapozungumzia ujamaa duniani, tunazungumzia falsafa za Karl Marx na nchi mfano iliyofanikiwa kukuza na kuendeleza ujamaa kufikia mafanikio ya juu kabisa ni China. Ni wachache sana baina ya watanzania walioisoma historia halisi ya China, wengi historia ya china wanaisoma mitandaoni ambayo si historia ya China kweli ila ni ya Mmarekani(google na internet ni marekeni) hivyo Marekani inaweza kuitengeneza historia ya china kwa kadiri inavyojisikia. Si historia ya China tu bali hata ya Afrika inaweza kuitengeneza atakavyo.

Kusema Ujamaa hauna manufaa, mmeona China walichofanya ndani ya muda wa miaka 30 walipotoa azimio la maendeleo ya China miaka ya 1980? China leo imekuwa great power na sababu ni kuendeleza na kudumisha historia ya mchina hususani kuendelea na mfumo wa kijamaa.

Ni mfumo ambao china imeona unafaa kwa maendeleo na imethibitika ni kweli unafaa sana.
Leo mtanzania ukimuuliza CHINA ni mbepari au mjamaa? Karibu 80% watakuambia China ni mbepari, ni kwa sababu wanauangalia ujamaa kama ubepari na wameathiriwa na historia za mitandaoni ya ujamaa. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, mitandao na google ni mmarekani hivyo marekani itatumia kila njia kuusema vibaya ujamaa ili usienee na kuwa tishio la ubepari. Hawataki kuamini kuwa ujamaa unaweza kujenga uchumi imara na wanaogopa ujamaa unaweza kuwa tishio la ubepari.

Ili kujiridhisha ukweli wa nisemayo, kitabu cha XI JIPING- THE GOVERNANCE OF CHINA kimeeleza kila kitu na mfumo ambao china unatumia ambao ni SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS. Kama Rais wa China na Katibu mkuu wa CPC ( chama pekee kikubwa china) anasema ataiongoza CHINA katika ujamaa, inakuwaje mbepari aseme china ni mbepari? Hii ni hofu ya ubepari dhidi ya ujamaa.

Katika kitabu hicho XI JIPING anaendelea kusema kwamba wataendelea kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa lengo la kuendeleza na kukuza demokrasia. Hii kauli inathibisha uongo wa mabepari na washirika wake kuwa ujamaa hakuna demokrasia. Kama demokrasia ni vyama vingi, China ina demokrasia ya mfano lakini CPC ndio chama kikuu kama ilivyo CCM kwa Tanzania.

China hakutaka kujiingiza mzimamzima katika mfumo wa kibeberu ila alikuwa anatafuta njia yake ya kupita kwa kuuboresha mfumo wa kijamaa ambao SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS ndio mfumo wao na ni mpya kabisa. Njia ambayo wamepita ni salama kwa maendeleo yao.

Tanzania tunaweza kujifunza kitu kutokea China, mfumo wa kibeberu umekomaa sana kiasi cha kufanya nchi za Afrika kushindwa kuendana nao. Turudi kwenye historia yetu na kurekebisha falsafa za mfumo wetu wa zamani kama walivyofanya China, Nina hakika maendeleo yatakuja kwa kasi sana. Ninaamini siku moja Afrika ikisimama na kupita njia yake nje ya ubepari na ujamaa au kufuata ujamaa kwa sababu ni mchanga na hujakomaa sana, ndio siku ubepari utakufa.

Msiangalie ujamaa kwa kuiangalia Korea Kaskazini, ule ni udikteta. Uangalie ujamaa wa China ambao umeibadilisha China kwa muda mfupi sana na kuendeleza historia ya China.
Mzee ili ujamaa ufanye kazi lazima udikteta uwepo, china ina udikteta kuliko unavyofikiria, hakuna haki za binadamu, watu wanaopinga wanafungwa kila siku. Lakini china wamekuwa wajanja zaidi wameachia soko huru la kibiashara Sisi bado tunafikiria ujamaa wa kubana kila kitu ndio maana tunafeli, tukitaka tuendelee tuachie sekta binafsi ifanye kazi.
Lakini pia mazingira ya china na Sisi yako tofauti Sana, china wanasoko kubwa la ndani ambalo ni imara na ambalo kila kampuni kubwa duniani inaliangalia, Sisi soko la ndani ni dogo Sana halikaribishi wawekezaji na makampuni makubwa
 
mwanza

JF-Expert Member
May 7, 2009
761
500
na ubepari kamili , sekta binafsi inamiliki 100% ya njia za uchumi na usambazaji yaani sekta binafsi itamiliki mpaka mifumo ya jeshi, ulinzi wa bahari, barabara zote, madaraja yote, njia zote za mawasiliano, nishati yote na reli zote. mbona marekani wanajiita mabepari kama sekta binafsi haina umiliki wa 100%? Mixed economy ni ujinga ulianzishwa na marekani kuua ujamaa duniani,
Sio kweli UK ni taifa la kibepari lakini kuna mashirika mengi serikali ina mkono wake shirika la ndege, BP, treni
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
Sio kweli UK ni taifa la kibepari lakini kuna mashirika mengi serikali ina mkono wake shirika la ndege, BP, treni
I would suggest that the UK does not have capitalism because of the presence of government intervention in the economy. Clearly – unless we believe in anarcho-capitalism – there will always be some level of government intervention in the economy. However, I would argue that it is not only the great extent but also the nature of that intervention which lead to this conclusion.

source:economics blog, Adam Smith University(U.K)
 
Letibaby

Member
Aug 23, 2018
22
45

Mim nazan maendeleo yantegemeana mwamko wa watu wenyewe kam jamii siyo tegemezi sanaa hapa lazma maendeleo yawep lakin katika kutazamia mfumo nchi inaweza kuwa ya kijamaa au ya kibepari and still the problem of underdevelopment existing,, uongozi bora,mwamko kwa jamii na utendekaji bora hvi ndy utengeneza mfumo wa jamii...
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
10,831
2,000
na ubepari kamili , sekta binafsi inamiliki 100% ya njia za uchumi na usambazaji yaani sekta binafsi itamiliki mpaka mifumo ya jeshi, ulinzi wa bahari, barabara zote, madaraja yote, njia zote za mawasiliano, nishati yote na reli zote. mbona marekani wanajiita mabepari kama sekta binafsi haina umiliki wa 100%? Mixed economy ni ujinga ulianzishwa na marekani kuua ujamaa duniani,
Hao wachina unao wafagilia ndo wanao ufuata sasa.
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
Hao wachina unao wafagilia ndo wanao ufuata sasa.
China is still a socialist country, soma hapa:

First, the People’s Republic of China has some interesting characteristics that make it rather different from the average capitalist country. Most importantly, although inequality has increased over the past 40 years, the standard of living for ordinary workers and peasants has risen dramatically along with it. Wealth under capitalism generally has its counterpart in poverty and exploitation (at home and/or abroad), but in China practically everyone enjoys a far better standard of life than they used to. Extreme poverty is on the cusp of being completely eliminated – an extraordinary achievement for a country of China’s size.

Secondly, China is run by a communist party that continues to adhere to Marxism-Leninism. While it no doubt suffers from corruption, and although its ideological purity has been diluted, its history and traditions mean that it derives its legitimacy and support from the masses of workers and peasants. As such, the Chinese state operates primarily in the interests of the working classes, unlike any capitalist state.

Thirdly, as much private capital as there is in China, the economy is still very much dominated and directed by the state. So while China has introduced elements of capitalism in the 40 years since the start of ‘reform and opening up’, these do not constitute a negation of socialism, any more than they did in the New Democracy period in the 1950s, or under the New Economic Policy in the Soviet Union in the 1920s. The point of the reforms is to to lay the ground for a more advanced socialism.
 
ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
2,277
2,000
kanuni kubwa inayotofautisha kati ya ujamaa na ubepari ni " ownership" au umiliki wa rasilimali, huduma na watu na " distribution" au utolewaji wa rasilimali watu na huduma. Kanuni nyingine za kutofautisha ubepari na ujamaa zinaweza kuingiliana.

katika ubepari, huduma muhimu zinamilikiwa na kusambazwa kwa wingi na sekta binafsi" major means of production and distribution are owned by private sector". kwa maana kwamba watu binafsi ndio watoaji wa huduma muhimu kama maji, umeme , afya n.k

wakati katika ujamaa, huduma muhimu zinamilikiwa na kutolewa/kusambazwa kwa wingi na sekta ya umma( serikali)" major means of production and distribution are owned by public sector".

ila kuna ukosefu wa elimu ambao ulikwamisha malengo ya ujamaa. hakuna mfumo wowote ambao sekta binafsi au sekta ya umma unamiliki njia zote za uchumi wenyewe. Marekani yenyewe sio "pure capitalst" kwa maana ya kwamba serikali inamiliki kidogo na sekta binafsi ndio inamiliki sana.

woga wa watanzania juu ya ujamaa ulitokana na upotoshaji wa kuilinganisha " socialism" na " communism" . Katika " communism" ndio serikali inamiliki kila kitu na kunakuwa na "equal distribution of resources" ila katika socialism sio hivyo. ninachotaka kiwepo ni "ushoshalisti na sio ukomusti"
Sasa Nyerere alikuwa anahubiri nini usoshalist au ukomunist apa naona kama umechanganya mambo mzee, Nyerere alikuwa ni advocate wa ujamaa pure communist
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,669
2,000
Sasa Nyerere alikuwa anahubiri nini usoshalist au ukomunist apa naona kama umechanganya mambo mzee, Nyerere alikuwa ni advocate wa ujamaa pure communist
Nyerere alikuwa mshoshalist au mjamaa( socialist) na sio mkomunist(communist). Tanzania haijawahi kuwa taifa la kikomunisti hata maramoja na Mwl.Nyerere alihubiri ujamaa maisha yake yote
 
Bonge

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
1,070
2,000
China hakuna ujamaa.... Tena mabepari ya kichina wanawanyanyasa kweli wachina maskini wanaotokea vijijini .. Afadhali hata mlala hoi wa hapo bongo unakuta ana ardhi na kakibanda
 
Master minding

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
5,785
2,000
Unajifanya una support ujamaa
Wakati unaishi kibepari!
Acheni unafki Nyie KARLO MWILAPWA

Ova

Hao jamaa badala ya kutafuta sasa hivi wako Wapo Wapo tu wanaishi wakijifanya wameridhika huku wanachofikiria ni kupora Mali za watu kwa kisingizio cha Ujamaa baadae hizo Mali walizopora zinawashinda zinakuja kuliwa na kuchukuliwa na mafisadi
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,130

Kweli kabisa

Ova
 
Msego

JF-Expert Member
Mar 12, 2019
437
500
Kweli hapo umenena chief,Hawa wanatuona wote mazuzu
Hivi mtu anajifanya kusemea ujamaa Wakati
Usafiri tu anaotumia ni range sport

Ova
Yeye aliposoma hayo maandiko yamemkataza kufanya tafakuri. Mbona anakuwa kama sponge, anashindwa kuchuja maji na mafuta
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom