KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Watanzania tuna kasumba ya kuuangalia ujamaa kwa jicho la ubepari na kuona ujamaa ni mfumo usio na maslahi yeyote kwa jamii. Vipi kuhusu ubepari unatengeza matabaka ndani ya jamii, una maslahi gani? Kushindwa kuutazama ujamaa kama ujamaa na badala yake ukatumia jicho la kipebari kuutazama ujamaa, hapo utaona kile usichokuwa nacho ni bora Zaidi kuliko ulichonacho( kwa sababu ulichonacho umekizoea)
Tunapozungumzia ujamaa duniani, tunazungumzia falsafa za Karl Marx na nchi mfano iliyofanikiwa kukuza na kuendeleza ujamaa kufikia mafanikio ya juu kabisa ni China. Ni wachache sana baina ya watanzania walioisoma historia halisi ya China, wengi historia ya china wanaisoma mitandaoni ambayo si historia ya China kweli ila ni ya Mmarekani(google na internet ni marekeni) hivyo Marekani inaweza kuitengeneza historia ya china kwa kadiri inavyojisikia. Si historia ya China tu bali hata ya Afrika inaweza kuitengeneza atakavyo.
Kusema Ujamaa hauna manufaa, mmeona China walichofanya ndani ya muda wa miaka 30 walipotoa azimio la maendeleo ya China miaka ya 1980? China leo imekuwa great power na sababu ni kuendeleza na kudumisha historia ya mchina hususani kuendelea na mfumo wa kijamaa.
Ni mfumo ambao china imeona unafaa kwa maendeleo na imethibitika ni kweli unafaa sana.
Leo mtanzania ukimuuliza CHINA ni mbepari au mjamaa? Karibu 80% watakuambia China ni mbepari, ni kwa sababu wanauangalia ujamaa kama ubepari na wameathiriwa na historia za mitandaoni ya ujamaa. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, mitandao na google ni mmarekani hivyo marekani itatumia kila njia kuusema vibaya ujamaa ili usienee na kuwa tishio la ubepari. Hawataki kuamini kuwa ujamaa unaweza kujenga uchumi imara na wanaogopa ujamaa unaweza kuwa tishio la ubepari.
Ili kujiridhisha ukweli wa nisemayo, kitabu cha XI JIPING- THE GOVERNANCE OF CHINA kimeeleza kila kitu na mfumo ambao china unatumia ambao ni SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS. Kama Rais wa China na Katibu mkuu wa CPC ( chama pekee kikubwa china) anasema ataiongoza CHINA katika ujamaa, inakuwaje mbepari aseme china ni mbepari? Hii ni hofu ya ubepari dhidi ya ujamaa.
Katika kitabu hicho XI JIPING anaendelea kusema kwamba wataendelea kuwa na mfumo wa vyama vingi kwa lengo la kuendeleza na kukuza demokrasia. Hii kauli inathibisha uongo wa mabepari na washirika wake kuwa ujamaa hakuna demokrasia. Kama demokrasia ni vyama vingi, China ina demokrasia ya mfano lakini CPC ndio chama kikuu kama ilivyo CCM kwa Tanzania.
China hakutaka kujiingiza mzimamzima katika mfumo wa kibeberu ila alikuwa anatafuta njia yake ya kupita kwa kuuboresha mfumo wa kijamaa ambao SOCIALISM WITH CHINESE CHARACTERISTICS ndio mfumo wao na ni mpya kabisa. Njia ambayo wamepita ni salama kwa maendeleo yao.
Tanzania tunaweza kujifunza kitu kutokea China, mfumo wa kibeberu umekomaa sana kiasi cha kufanya nchi za Afrika kushindwa kuendana nao. Turudi kwenye historia yetu na kurekebisha falsafa za mfumo wetu wa zamani kama walivyofanya China, Nina hakika maendeleo yatakuja kwa kasi sana. Ninaamini siku moja Afrika ikisimama na kupita njia yake nje ya ubepari na ujamaa au kufuata ujamaa kwa sababu ni mchanga na hujakomaa sana, ndio siku ubepari utakufa.
Msiangalie ujamaa kwa kuiangalia Korea Kaskazini, ule ni udikteta. Uangalie ujamaa wa China ambao umeibadilisha China kwa muda mfupi sana na kuendeleza historia ya China.