Uingereza yapaswa kuachana na mawazo ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”


Waziri wa Biashara wa Uingereza Dominic Johnson hivi karibuni alifanya ziara mjini Hong Kong, China, akiwa na lengo la “kuihimiza Uingereza kupata uwekezaji na biashara zaidi”. Hata hivyo, bado hakuacha kufuatilia mambo ya ndani ya Hong Kong, na kudhihirisha kuwa ni vigumu kwa Uingereza kuacha mawazo ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”.

Hivi sasa Uingereza ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya uchumi wake. Mwezi Januari, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilitabiri kuwa uchumi wa Uingereza utashuka kwa asilimia 0.6 mwaka huu, huku Shirika la Goldman Sachs likitabiri kuwa, utapungua kwa asilimia 1.2. Uchumi wa Uingereza unakabiliwa na changamoto mbalimbali zisizoweza kusuluhishwa kirahisi, zikiwemo upungufu wa nishati, mfumuko wa bei, na ukosefu wa uwezo wa kuboresha maisha ya watu. Hii pia ni moja ya sababu kuu zilizoifanya Uingereza kutuma afisa wake wa juu kwenye Hong Kong kuomba ushirikiano.

Johnson alitoa ajenda yake mjini Hong Kong kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, na pia alichapisha makala katika Gazeti la South China Morning Post, akisema anatumai kuimarisha uhusiano wa uwekezaji kati ya Uingereza na Hong Kong wenye thamani ya Paudi bilioni 94 za Kiingereza. Johnsona anafahamu vizuri kwamba Hong Kong ni moja ya vitovu vya kimataifa vya fedha, na kuna nafasi kubwa ya ushirikiano na mkoa huo katika nyanja za fedha, miundombinu, na uhifadhi wa mazingira. Ushirikiano na China unaweza kupunguza mzozo wa kiuchumi nchini Uingereza na kuleta fursa nzuri ya maendeleo, kwani China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Uingereza barani Asia, na Uingereza ni nchi ya pili inayovutia uwekezaji wa China barani Ulaya. Mwaka 2021, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Uingereza ilikuwa dola bilioni 112.6 za Kimarekani.

Hata hivyo mwanasiasa huyu wa Uingereza ambaye alikuja China kutafuta ushirikiano, hakuacha mawazo yake ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”, na kwa mara nyingine tena, aliingilia kati mambo ya ndani ya China. Wakati wa ziara yake mkoani Hong Kong, alisema Uingereza haitakwepa kile kinachoitwa “wajibu wake wa kihistoria” kwa Hong Kong, haitafumbia macho "ukiukwaji wa uhuru" mkoani humo, na kuitaka China kutekeleza “haki za binadamu”.

Hong Kong ina historia ndefu ya kuteseka na utawala wa kikoloni wa Uingereza. Mnamo mwaka 1841, Waingereza walianzisha Vita vya Afyuni dhidi ya China, na kukalia Hong Kong, na kuitawala kwa zaidi ya miaka 150. Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, kutokana na kubadilika kwa nguvu ya kitaifa, Uingereza ililazimika kukubaliana na China kurejesha mamlaka ya utawala wa Hong Kong kwa China mwaka 1997. Hata hivyo, baada ya Hong Kong kurudi kwa China, Uingereza imeshindwa kubadilisha mawazo yake ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”, na kuingilia kati mambo ya Hong Kong mara kwa mara.

Kama nchi kubwa zaidi ya zamani ya Kikoloni duniani, Uingereza iliwahi kutawala nchi nyingi karibu katika mabara yote isipokuwa Antaktika. Wakoloni wa Uingereza walipora mali, kutesa watu na kuwaua kikatili wale waliojaribu kuwapinga katika nchi hizo. Sasa ukoloni umeondolewa kwa miaka mingi, lakini badala ya kuomba msamaha kutokana na vitendo viovu vya kikoloni, Uingereza bado inachukulia historia ya ukoloni kama ni fahari yake, na kutaka kuendelea kuwa na ushawishi katika nchi na sehemu ilizotawala kikoloni.

Katika suala la ushirikiano na China, Uingereza inapaswa kuwa na busara ya kujua inachohitaji kufanya, na kuacha kabisa ndoto ya kuendelea kuingilia mambo ya ndani ya China, huku ikitarajia kuzidisha ushirikiano na China.
Mseng€ wewe , Hongkong imeteseka chini ya mwingereza ? ,Unajua unachoandika wewe au unaharisha tu hapa ?
 
Back
Top Bottom