Uhusiano wa Franco na Mobutu

Historia ya africa ina complications nyingi,,nimependa conclusion yako mkuu
 
dah Jamaa alikula bata
Sana,,alikua na nyumba zingine inapita hata miaka 3 hajazitembelea,

Mkewe anatajwa kuwa na nguo zaidi ya elfu moja,
Mkuu ukitaka mengi kitafute kitabu kinaitwa a la cour de mobutu,kimeandikwa na pierre jansen,mpwa wake
 
naam huyu ukimwi ulimuua mwaka 1998 pale Monaco
aligegeda kila aina ya binti aliempenda na alikuwa na uwezo wa kwenda shule fulan anaopoa binti anaenda Ku gegeda bila MTU yoyote kumuiliza,alikuwa moja ya ma body guard wa Mobutu Babae
Jamaa naitafuta historia yake mtandaoni ipo fupi mno,but siku moja ntaenda kinshasa nikapige stori na jamaa zake nimjue vizuri
 
Mkuu Lucas Mobutu sina nia ya kukosoa bandiko lako but hapo kwenye wimbo Candidat Na Biso Mobutu naomba niongeze nyama kidogo kuhusu huu wimbo.

Baada ya kutoa wimbo wa kumtuhumu rais Mobutu kwa uongozi wake wa mkono wa chuma iliamriwa Frànco akamatwe atiwe jela,kisha Mobutu akampa options mbili either atumie kipaji chake kutunga wimbo mzuri utakaomfanya azidi kupendwa na wananchi wake au aendelee kukaa jela{tukumbuke huu wimbo wa kum-dis Mobutu ulipokelewa vizuri sana na masahabiki wa Frànco so nikama aliambiwa atafute kitu cha kuyafuta yale mawazo mabaya kwa wananchi kisha apandikize mazuri yanayomuhusu yeye}.

Ndipo alipotunga huu wimbo canditad na biso Mobutu na inasemekana Mobutu alipousikiliza kwa mara ya kwanza tu aliamuru Frànco atolewe jela upesi sana na apelekwe ikulu ambako ilifanyika sherehe ya kukata na shoka kwa muda wa siku tatu kisha Mobutu akataka ampe Frànco madaraka ya kisiasa ambapo aliyakataa akaomba apewe ruhusa ya kufanya shughuli zake za kimuziki kwa uhuru tu.

Copied.......
 
Sor buroho ivi Mobutu ni mzee wako wa kukuzaa?
 
Ahsante sana mkuu kwa mchango wako
 
Mkuu ktk hili una point ila tusisahau hata sasa ukipimwa ukakutikana na maradhi haya doctor ktk moja ya masharti atakayokusisitiza sana ni wewe kuifunga zipu yako na kufanya yale ya muhimu tu kwa ajili ya afya yako.

Hawa wazee wetu kwa umaarufu waliokuwa nao na nyimbo za mapenzi walizokuwa wanaimba ziliwafanya wanawake wawapende mno,mnoo!ilifikia kipindi wakishuka jukwaani tu wanawake wanawagombania mpaka kuchaniana nguo ili wakawape mzigo.

Sasa ktk mazingira kama haya angekaaje miaka 10 hali yakuwa kila siku alikuwa anachuja nafaka na lady's tofaut tofauti huku akiishi maisha ya starehe pombe na misigara,kuna mwaka nilisikiliza interview ya marehem Dr Remmy akisema kipindi anawika ilikuwa kawaida kwenda msalani na kukutana na mrembo akimsalimia tu anam'bong'olea mzee anapiga show kisha anamwachia pia wakati wa kuondoka anakokota mmoja au wawili wa kuspend nae mpaka asubuhi.

Zamani watu walijitoa ufahamu sana...
 
Hahahaha,,
 
labda umesahau,hebu fwatilia historia ya mpongo love,mwaka 1977 Franco alimsajili mpongo ktk band alikaa miaka miwili okk jazz,hata wimbo wake "ndaya"aliutunga kwa msaada wa Franco,hebu fwatilia
mpongo love alifariki 1994
Google wanasema alikata moto 1990 nadhani ilitokana na shock ya mzee baba nae kuonekana ameenda kwa maradhi yasiyo ya starabu.walipishana miezi tu!
 
Huu uzi mtamu sana baada ya miaka mingi kupita na wote kuwa marehemu leo ndani ya jf nakutana na Lucas mobutu(akiwakilisha rais mobutu)
na wewe bwana luambo makiadi (ukimwakilisha franco luambo makiadi)

Long live jf
..........Bila kumsahau Thomas @sankara,huyu walimuuwa ila alikuwa rais kijana mwenye muono wa mbali sana.inafurahisha sana mkuu na hawa ni watu kwa kiasi kikubwa wametupa heshima kubwa kimataifa ila Mobutu alizingua sana.
 
..........Bila kumsahau Thomas @sankara,huyu walimuuwa ila alikuwa rais kijana mwenye muono wa mbali sana.inafurahisha sana mkuu na hawa ni watu kwa kiasi kikubwa wametupa heshima kubwa kimataifa ila Mobutu alizingua sana.
Thomas sankara kiongozi kijana kabisa mwenye maono ya mbali sana akishika uongozi wa juu kabisa wa burkina fasso wakati huo ikiitwa upper volta akiwa na miaka 31 tu.

Huku akitawala miaka 4 tu 1983-87
Akiuwawa na rafiki yake kipenzi aliyekuja baadae kuwa rais wa nchi hiyo blaise compaore.

Lakini angalia ajabu ya mungu nae baada ya miaka 27 ya kutawala Compaore ndani ya mwezi ule ule wa oktoba aliompindua na kumua rais Sankara ndani ya mwezi huo huo japo miaka na siku tofauti naye alipinduliwa na kulazimishwa kukimbia burkina fasso.

Kwa hakika ndani ya maisha ya rais huyu kijana Thomas Sankara tunayo ya kujifunza mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…