SoC02 Uhusiano kati ya usafi wa mazingira na maendeleo

Stories of Change - 2022 Competition

Tims Uchumi

New Member
Aug 30, 2022
4
4
Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka mfano miti,mito,miamba,hewa safi.

Utunzaji wa mazingira ni kitendo kinachohusisha uhifadhi wa mazingira asilia,kuyalinda yasiharibike kutokana na shughuli za kibinadamu mfano utupaji hovyo wa Taka.

Usafi wa mazingira Inauhusiano mkubwa sana katika kutunza mazingira kwani mazingira safi asili ya mazingira haipotei lakini pia mazingira safi ni chanzo cha maendeleo.

Maendeleo ni ukuaji kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine,maendeleo yanahusisha Jamii,Uchumi na Siasa.

Uhusiano wa Mtu Mmoja Mmoja katika usafi wa mazingira,Tunaangazia sehem kuu mbili ikiwemo
Utupaji Tata na Matumizi ya vyoo.

Utupaji Taka(Jijini Tanga,Tafiti binafsi),Katika jiji la Tanga maeneo mengi hususani maeneo ya makazi ya watu,biashara ndogondogo na sehem za starehe kunachangamoto kubwa ya utupaji taka holela licha ya jitihada za serikali katika kusimamia usafi wa mazingira jijini Tanga ikiwemo kuwa na vifaa vya kutunzia taka bado kuna changamoto kubwa ya watu kutojali swala zima la usafi wa mazingira hasa linapokuja swala la utupaji taka,watu hutupa taka katika mitaro ya maji,wengine hutupa barabarani.

Changamoto hii huleta athari ikiwemo harufu mbaya hivyo kusababisha kero kwa watumiaji wa barabara, kuziba kwa mitaro ya maji ,kusababisha milipo ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuhara,kipindupindu lakini pia ongezeko la mazalia ya mmbu waenezao malaria.

Kwa tafiti nikwamba watu katika maeneo tofaut tofaut jijini Tanga bado hawana muamko juu ya umuhimu wa utupaji taka lakini pia vifaa vya kutunzia taka bado havijawa katika maeneo hayo hivyo kusababisha watu kutupa taka kiholela,

Matumizi Ya Vyoo
Nikweli usiopingika kua choo ni moja kati ya sehem muhimu sana katika jamii,serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali pamoja na wananchi wameweza kuandaa programu maalumu ijulikanayo kama "Nyumba ni Choo" kuhakikisha katika mitaa na sehem zingine kuna vyoo kwa ajili ya watu kupata huduma hii imesaidia sana kuondoka na kadhia ya uchafu wa mazingira lakini..!

Usafi wa vyoo hivyo ni changamoto,sehemu za makazi hasa nyumba za kupanga na sehemu za
starehe vyoo vimekua vichafu sana kiasi cha kusababisha kero kwa watumiaji,licha ya uchafu vya vyoo kumekua na matumizi mabaya sana ya vyoo ikiwemo watumiaji kutupa taka ngumu kama makopo,vyupa,mabox hivyo kufanya vyoo hivyo kuziba na kusababisha athari ikiwemo kuzibuka kwa chemba za vyoo hivyo na madhara ikiwa ni pamoja maji machafu kutuama katika makazi ya watu ambayo huleta madhara ikiwemo milipuko ya magonjwa adhari kama harufu mbaya pamoja na kuharibika kwa miundombinu lakini zaidi ni gharama za magari ya kuvuta taka hizo ,ikumbukwe shughuli za uzibuaji wa vyoo hivyo husababisha kero nyingine kwani watu hawatotumia choo husika kutokana na kua na matengenezo hivyo huishia kwenda kutoa haja ndogo au kubwa katika sehem za wazi ikiwemo vichochoroni na kando ya barabara ambayo huleta athari za kimazingira.

AFF2620B-F0DC-4767-B88B-56EFE7F1DC08.jpeg

a)Moja kati ya vyoo Jijini Tanga katika moja ya sehem ya starehe

Ni wajibu wetu wananchi kwa kushirikiana na wadau wengine pamoja na serikali kuhakikisha kunakua na usimamizi wa mazingira ili kuepukana na matatizo yatokayao na uchafu wa mazingira.

Uchafu wa Mazingira na Maendeleo
Madhara yote hayo katika sehem zote mbilo yana athari kubwa katika maendeleo kwani,mlipuko wa magonjwa husababisha watu kuumwa na kupoteza maisha lakini pia wengine kulazwa au kubaki nyumbani hivyo kuathiri moja kwa moja maendeleo ya kiuchumi,pia katika miundombinu ikiwemo mitaro ya maji uchafu wa mazingira husababisha maeneo kutopitika hivyo wa wale wanaofanya shughuli za maendeleo katika maeneo hayo ikiwemo biashara kutopata wateja hivyo kuathiri moja kwa moja ukuaji wa maendeleo yao.
516C4B80-5416-4C55-A2EB-C4E07733AA8C.jpeg

b)Moja ya mitaro katika mitaa ya jiji la Tanga
Ahsante, naomba kuwasilisha.
 
View attachment 2342318

View attachment 2342322
b)Moja ya mitaro katika mitaa ya jiji la Tanga
Ahsante, naomba kuwasilisha.
Hello Tims
Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Back
Top Bottom