Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,607
- 3,191
Eti magari manne?? Jana huo msafara wa Kenyata umesababisha wamama wa watu wachelewe nyumbani ...hapakuwa na gari la kwenda Tengeru,Ngulelo na kuendelea ..barabara ya kwenda kijenge na Moshono zote zimefungwa. Nikiwa kama muhanga wa tukio la jana sioni kama ana sifa zote hizi alizotajiwa kwa kweli. Hata kama ni magari ya Tanzania yalimpokea lakini sio kuleta foleni kiasi kile cha jana. Inalindwa roho moja wakati wengine 100 hawajui hata watalala wapi..
Viongozi wenu kwa kiherehere chao ndio waliamua kufunga barabara Arusha wala sio Kenyatta. Yeye alikuwa ni mgeni na wenyeji ndio waliamua kufunga barabara sasa Kenyatta unamlaumu kwa lipi hapa?. Yeye hata kule Nairobi hatembei na msururu mrefu hata kidogo. Ulisikia kisa yeye na escort wake walipozuiliwa na traffic polisi Nairobi akafungua dirisha kumuomba traffic police awaruhusu wapite? Hapendi makuu huyu jamaa.
Tiba