Uhuru ni muhimu katika mahusiano

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
23,381
29,627
Ukiona uko kwenye ndoa halafu hauna uhuru kabisa kuhusu mapato au matumizi, Mara nyingine unalazimika kutoa maelezo yakina kwenye kila kitu kihusucho hela uliyotumia au uliyopata, tena unatoa maelezo ukiwa umesimamiwa.

Hauna kitu ambacho unaweza kuwa huru kununua bila kuuliza au kuomba ruhusa, kila wakati unajihisi kama vile hauaminiwi au kama vile unaonekana mwizi.

Hakuna unachofanya halafu usilaumiwe kuwa unatapanya pesa. Ukiona unanunua au unapata kipato na unajiuliza mara mia hivi nitasemanimepata wapi hii hela? Au nitasema nimetumiaje?

Basi ujue jela kuna uhuru kuliko kwenye hiyo ndoa yako. Usifikiri ni hadi uvae uniform ya magereza ndio uitwe mfungwa, wewe tayari ni mmojawao.

Na Dr. ChrisMauki
 
Ila bhana kasema kwenye ndoa. Mambo ya ndoa yanakuwa magumu pale ambapo unakuwa hauko huru. Tuchukulie upande wa mwanamke huwezi hata toka na wanawake wenzako kisa mume hapendi. Duuuh maisha ya hivyo bora kuwa single kabisa
 
Daaaaaah

husi promote watu kuwa single , ndoa tamu bwana. Sijaoa though.
 
Sasa kukiwa na uhuru kuna ndoa hapo? Kama ndoa ina mawasiliano mazuri lazima uhuru ukosekane pia.
 
Back
Top Bottom