Uhuru na Siasa Tanzania

Tohoa

Member
Sep 13, 2021
28
17
Tanzania bado ina shida kubwa sana katika kipengele cha siasa. Matatizo ya siasa za Tanzania yanasababishwa na Mambo makuu yafuatayo;

1) Katiba yetu imepitwa na wakati
2) Katiba za vyama vya siasa vyote Ni kandamizi kuliko hata Katiba ya nchi
3) Unafiki na ubinafsi
4) Mihemko na uelewa mdogo wa wanasiasa hasa vijana
5) Watu wanapenda zaidi vyama vya siasa kuliko siasa
6) Elimu ndogo miongoni mwa wanasiasa

Leo nitajikita katika Katiba za vyama vya siasa havitoi mwanya kwa wanachama kutoa hoja kinzani na viongozi wao.

Ukifanya hivyo unafukuzwa uanachama au kutopewa fursa ya uongozi ndani ya chama.

Hali hii imesababisha taifa kuwa na wanafiki wa kiwango kikubwa Sana. Kama tunataka kuponya taifa kweli tuanze na vyama vyetu kuheshimu mawazo ya wanachama wote ili tupunguze uchawa wa kusifiwa kila kitu au kukosoa Kila kitu.

Mfano mtu Kama Msigwa anadiliki kuwa Nivueni uongozi baada ya kutoa maoni juu ya Ngorongoro. Vipi kiongozi wa chini si angefukuzwa kabisa .

Katiba ya nchi ni muhimu sana pengine kuliko chochote kwa sasa lakini na kwenye vyama vyetu kuna mambo ya ovyo sana
 
Ndio maana kuna umuhimu wa Katiba mpya ila WAGOMBEA BINAFSI waruhusiwe kikatiba.
Pia Rais,Wabunge, madiwani waruhisiwe kuhama vyama bila kupoteza nafasi zao.Kwenye demokrasia za kweli inaitwa "Crossing the floor".

Back
Top Bottom