The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Na: McWenceslaus
01/10/2020.
Habarini za muda ndugu wanabodi wenzangu! Poleni kwa kazi na majukumu mengi ya siku. Baada ya kukaa kwa muda hivi, tukiwa tunatathiminu hali ya kampeni tangu mwanzo hata hivi leo, zikiwa zimesalia siku 27 kufika siku ya kufanya maamuzi ya kamchagua Rais, wabunge na madiwani. Kila mtu atakuwa ashapata kuona uelekeo sahihi wa nani ni Rais ajaye wa Tanzania. Na bila shaka asilimia kubwa ya watanzania wengi, wanauhakika na ushindi wa kishindo wa Rais Dkt. John Magufuli dhidi ya wagombea wengine kwa nafasi ya Rais Tanzania, msioamini subirini siku inakuja nanyi mtaamini. Ni kama ilivyokuwa kwa Thomaso mmoja wa mitume wa Yesu Kristo, ambaye hakuamini mwanzo lakini mwishowe aliamini. Leo ninakuja kuwa fahamisha Siri ya kauli ya HAKI na UHURU kama ambavyo imetumiwa na CHADEMA katika kampeni zake; na ukweli kuhusu UHURU na USAWA, katika kuleta AMANI na Maendeleo ya Watu. Nikuache uendelee....
Uhuru + usawa = Amani
Haki bila usawa ni sawa na mwili uliokosa chakula na matunzo, ni lazima mifumo yake ya mwili ifarakane na mwishowe ijifie yenyewe.
Na kwamba, haki ilikuwepo hapa nchini hata kabla ya uhuru. Moja ya sababu ya msingi ya kudai uhuru katika miaka ya 1960, ilikuwa ni kupigania haki na usawa katika mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, na hatimaye kuleta amani ndani ya taifa. Na hilo lilifanikiwa mnamo 09 disemba, 1961 ambapo watanzania walitambuliwa katika usawa na huru, hata hivi leo.
Leo hii tumeanza kusikia habari ya kuwa kuna kundi la watu wanaendelea kusikika humu nchini, wakisema "Amani ni tunda la Haki!" Huu ni uongo wa mchana kweupe peee. Hivyo basi, ni lazima tukawaambie wananchi kuwa, pasipo na usawa hakutakuwepo na amani. Ili kukanusha uongo huo. Tuseme kwa mfano, Paka anayo haki ya kumfukuza na kumtafuna panya; ni katika hali hiyo Panya ameshaonekana ni mnyonge mbele ya Paka, ni kwa sababu eti Paka anaitumia haki yake hiyo! Na kwa kusema ukweli, Panya huyu hawezi kufanya lolote la kumzuia Paka asitekeleze haki yake hiyo. Ni kwa sababu, nguvu hiyo ataitoa wapi, yeye ni mdogo paka ni mkubwa.
Hivyo katika jamii ya watu wenye hali tofauti ya kiuchumi, kiafya, kisiasa, rangi, itikadi n.k mfano wa Paka na Panya huyu, ni lazima msukumo mkubwa uwepo kwenye sera ya USAWA kuliko HAKI, kwa maana HAKI kwa asili huambatana na UHURU zaidi kuliko USAWA. Maana Palipo na HAKI pana UHURU; Na kwa sababu hiyo, ndiyo ilipelekea ndani ya azimio la Arusha 1967 chini ya chama cha TANU na baadaye CCM. Chama kilihimiza na kusisitiza kuwa ujamaa na kujitegemea ni siasa yenye lengo la kujenga jamii ya watu walio SAWA na HURU. Msukumo huo uliwekwa kwa sababu ya kutambua kuwa haki alikuwa nayo mkoloni ya kumnyonya mwafrika, lakini hakukuwepo na usawa wa kutambua kwamba mwafrika ni mtu ambaye anastahili heshima ya kutambuliwa utu wake. Na ndio maana palipo UHURU na USAWA ni lazima pawepo na AMANI, lakini palipo na haki na uhuru amani haiwezi kuwepo kabisa, ni sawa na yule Panya kwa Paka. Amani hiyo ipo kwa Paka pekee, lakini ni nani atakayeweza kusema kwamba Panya yule anayo amani, ukweli hayupo mtu huyo. Kwa Panya kukosa Amani, kwa sababu ya kuwepo kwa haki yake ya kukimbizwa na kutafunwa na Paka, inaifanya Amani ikosetafasiri nzuri kwa hakika.
Kwa kumalizia; katika kampeni za mwaka huu kuna ushindani baridi baina ya siasa ya ujamaa na siasa ya kibepari. Na ndio kwa sababu hiyo, Mgombea Lissu kupitia CHADEMA, amekuja na kauli mbiu ya uhuru na haki, na anajificha kwenye kivuli cha maendeleo ya watu kwa lengo la kuficha dhamiri yake ya kuukaribisha ubepari ndani ya Tanzania. Msukumo katika siasa za kibepari upo katika HAKI maana yake ni hivi, mfanyabiashara mkubwa na mfanyabiashara mdogo wote ni wafanyabiashara hawa hivyo watalipa kodi sawa kwa jina la biashara hiyo, hiyo ni HAKI sawa kwa wote na sio USAWA kwa wote. Katika ujamaa, msukumo mkubwa upo katika USAWA kwa wote, hii maana yake ni kwamba kila mfanyabiashara atalipa kodi kwa kadiri ya mapato yake yatokanayo na biashara yake... Huu usawa unafanya kuwepo kwa AMANI kwani kila mtu atachangia kwa kadiri ya uwezo wake. Na kila mtu atamuona mwenzake kuwa ni sawa kama alivyo yeye, vivyo hivyo kwa makundi na jumuiya zingine. USAWA ni mbegu bora ya kuleta AMANI ya kweli kwa wote.
Na katika kuendeleza nia hiyo ya dhati ya kudumisha UHURU pamoja na USAWA kwa ajili ya kuimarisha AMANI ya nchi yetu, serikali chini ya CCM na uongozi imara wa viongozi wa chama pamoja na Mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi Dkt. John P. Magufuli; imeweza kuimarisha usawa kwa makundi yote na watu wa hali zote kwa kuwapatia haki za muhimu za huduma ya jamii. Ikiwa ni pamoja na elimu bure, huduma za afya nafuu na kuimarisha huduma ya mfuko wa TASAF, upatikanaji wa maji katika meneo yote ya mijini na vijijini na maeneo yenye viwanda na yasiyokuwa na viwanda n.k. Hivyo imeweza kuendeleza hali ya AMANI nchini hata sasa.
Uhuru + usawa = Amani
#chaguaCCM
#chaguaUjamaanaKujitegemea
#chaguaUsawanaUhuru
#chaguaMagufuli
Kazi inaendelea 2020-2025
Sauti ya Mdodomia.
01/10/2020