Uhuru katika mahusiano ni muhimu sana, kabla ya kua katika mahusiano yenu kila mtu alikua na mambo yake na ratiba zake au aina yake fulani ya maisha aliyokua anaishi, ukiingia katika mahusiano zipo ambazo ratiba au aina fulani ya maisha itapungua lakini sio yote..
Mfano hai kwangu: niliwahi kua katika mahusiano na mwanamke mmoja hivi basi alikua anakaba hadi penati, atanichatisha na kunipigia simu muda wote, always tuwe karibu kama sio physical basi through simu (nadhani kwa akili yake alijua hayo ndio mapenzi lakini kwangu ilikua ni kero)
Kuna muda nakua bize na kazi, kuna muda naenda zangu kucheki mpira either taifa au ligi ya wenzetu (ligi kuu ya uingereza) sometimes inabidi nijichanganye na wana sasa huyo mwanamke ukimwambia tu unafanya moja kati ya haya ananuna, anaona ni kama humpendi kwake alikua na mindset ya 50%-50% kama anavyofanya vile basi na mimi nifanye hivo hivo hadi nikawa najiuliza mapenzi gani haya ya kuchekiana kila dakika as if umebandika maharage jikoni.
Kwa experience niliyoipata mtu huru namuona ni yule aliyepo single mbali na hapo ni uhuru wa bendera tu.