TADPOLE
JF-Expert Member
- Nov 18, 2015
- 2,801
- 9,042
Kuna mshamba MATAGA anakubishia hapo juu anafikiri Mzee Mbowe alikuwa fukara kama alivyo baba yake huko kijijini kwao Iringa,Mwambie kwamba Mzee Mbowe alikuwa anaingia Ikulu muda wowote kuonana na Nyerere na alikuwa ni tajiri kabla hata ya uhuru,Nyerere alimpenda haswaa kwakuwa alikuwa ni kiungo muhimu kuunganisha wazee wa kimila wa kaskazini na TANU..Gari ya kwanza ya Aikaeli kumiliki ni BMW 520i hii wakati inaingizwa nchini kulikuwa na magumashi kibao yaliyokwamisha mchakato mzee akamvutia waya Nyerere na kumwambia kijana wangu anakwamishwa kuingiza gari naomba umsaidie order ikatoka ikulu chap gari ikaingia..Hilo halina ubishi,wanadhani umasikini wao umesababishwa na matajiri
Pia watu hawajui sababu ya Mbowe kuacha kazi BOT,Mbowe aliacha kazi BOT hili kusimamia biashara za baba yake ambapo mwanzo ilimuwia vigumu kwenda kwenye ajira na same time kusimamia biashara akaamua achague moja(mpaka hapa tunaona jinsi hii familia ilivyo na ukwasi)..
Siku Mbowe anaacha kazi BOT aliingia ofisini kwa naibu GAVANA Bob Makani akamwambia nataka kuacha kazi Bob akamwambia "sikia we dogo unaona huu mlango potea fasta nisikuone usiniambie ujinga ujinga mimi" Mbowe badala ya kwenda kuendelea na kazi alipitiliza nyumbani moja kwa moja na ikawa ndio siku yake ya mwishk BOT..Enzi hizo Gavana alikuwa Edwin Mtei na naibu Gavana ni Bob Makani ambao ndio baadae wakaanzisha CHADEMA