Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Naandika hoja hii hapa kufuatia mijadala inayoendelea mitandaoni kuhusu tafsiri ya uraia wa Bw. Manji. Naamini amekuja nchini kuendeleza miradi yake lakini pia ameletwa na mfumo kwa ajili yakurejesha imani ya wageni waweze kurejea nchini baada ya miaka kadhaa diplomasia yetu kimataifa kuwa na mrengo usioelewe.
Lakini nakumbuka Mara ya mwisho alikuwa raia wa Marekani na alipoondoka hapa alikwenda kuishi Marekani. Leo tunaambiwa karudi,well and good. Ila karudi Kama raia wa nchi gani?
Ni vyema Uhmiaji wakatoka adharani na kutuambia huyu Bwana ni Raia wa Tanzania, ni Raia wa Marekani au amepewa uraia pacha japo hakuna sheria inayompa uraia pacha kwa umri ule. Kukaa kimya kwa Uhamiaji, kukaa kimya kwa wizara ya mambo ya nje inayosimamia Ubalozi wetu wa Marekani ambao naamini wanahaki yakujua taarifa za uraia wa huyu mtu nikumfanya Mhe. Rais amwamini nakumshirikisha huyu Bwana akiamini ni Mtanzania kumbe sivyo.
Haya siyo mawazo yangu haya ni mawazo ya wanetu wanaoishi nje na ambao kwa bahati mbaya waliukana Utanzania wakapata uraia wa nje na Sasa awawezi kuupata tena Utanzania. Wanauliza Mbona Kuna tetesi kwamba Manji naye aliukataa Utanzania Kama Singo nakubaki na Umarekani, kwanini mitandao iandike yeye ni Mtanzania? Na Kama ana haki ya Utanzania mbona juzi Kati Mmarekani Mtanzania mwana Diaspora alipoteuliwa na Rais mitandao ikahoji inakuwaje Mmarekani anateuliwa na Rais, kwanini uteuzi wake ulifutwa japo kimya kimya?
Naamini kwa mwandiko wangu mchafu na ujinga wangu kwenye taaluma ya Uraia nimefungua mjadala kuwawezesha viongozi wetu kudemka na kucheza kwa kuzingatia due diligence kwa binadamu hawa wenye matatizo ya Uraia.
Uraia wetu ni zaidi ya fedha za mtu, ni zaidi ya rasilimali zetu hivyo tuitekenye sheria ya Uraia kwa ueledi itusaidie kuwadhibiti wasio Watanzania kujipa Utanzania wa muda.
Naamini tukiziba masikio nakuona potentiality ya Manji leo kuliko kuangalia Kwanza uraia wake tutafungua mjadala mkubwa huko mbeleni ambao utaligawa Taifa. Tujadiliane, tufunguane macho,tuelimishane na tumsaidie Rais na viongozi wengine kulitumikia Taifa kwa misingi Bora. Tusipowaambia tukaamini wanajua tutakua hatulitendei haki Taifa letu.
Uhamiaji tunawaomba mtoke adharani mseme ni raia au siyo raia. Msifanye Siri na msikubali kuambiwa na mwanasiasa nini mseme zingatieni sheria kumshauri mkuu wa nchi kwa lengo lakumwezesha afanye biashara,amtumie huyu mwekezaji na aruhusu taasisi nyingine kushiriakiana naye kwa hadhi sahihi ya Uraia siyo kwa adhi ya muda ambayo Samia akiondoka au kabla hajaondoka wanaweza kuibuka watu wakaiumbua serikali.
Nimechokonoa, endeleeni kutufunda.