Uhamiaji Tanzania, lisaidieni Taifa kuhusu Yusuf Manji. Ni raia wa Tanzania au Marekani?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,979
Naandika hoja hii hapa kufuatia mijadala inayoendelea mitandaoni kuhusu tafsiri ya uraia wa Bw. Manji. Naamini amekuja nchini kuendeleza miradi yake lakini pia ameletwa na mfumo kwa ajili yakurejesha imani ya wageni waweze kurejea nchini baada ya miaka kadhaa diplomasia yetu kimataifa kuwa na mrengo usioelewe.

Lakini nakumbuka Mara ya mwisho alikuwa raia wa Marekani na alipoondoka hapa alikwenda kuishi Marekani. Leo tunaambiwa karudi,well and good. Ila karudi Kama raia wa nchi gani?

Ni vyema Uhmiaji wakatoka adharani na kutuambia huyu Bwana ni Raia wa Tanzania, ni Raia wa Marekani au amepewa uraia pacha japo hakuna sheria inayompa uraia pacha kwa umri ule. Kukaa kimya kwa Uhamiaji, kukaa kimya kwa wizara ya mambo ya nje inayosimamia Ubalozi wetu wa Marekani ambao naamini wanahaki yakujua taarifa za uraia wa huyu mtu nikumfanya Mhe. Rais amwamini nakumshirikisha huyu Bwana akiamini ni Mtanzania kumbe sivyo.

Haya siyo mawazo yangu haya ni mawazo ya wanetu wanaoishi nje na ambao kwa bahati mbaya waliukana Utanzania wakapata uraia wa nje na Sasa awawezi kuupata tena Utanzania. Wanauliza Mbona Kuna tetesi kwamba Manji naye aliukataa Utanzania Kama Singo nakubaki na Umarekani, kwanini mitandao iandike yeye ni Mtanzania? Na Kama ana haki ya Utanzania mbona juzi Kati Mmarekani Mtanzania mwana Diaspora alipoteuliwa na Rais mitandao ikahoji inakuwaje Mmarekani anateuliwa na Rais, kwanini uteuzi wake ulifutwa japo kimya kimya?

Naamini kwa mwandiko wangu mchafu na ujinga wangu kwenye taaluma ya Uraia nimefungua mjadala kuwawezesha viongozi wetu kudemka na kucheza kwa kuzingatia due diligence kwa binadamu hawa wenye matatizo ya Uraia.

Uraia wetu ni zaidi ya fedha za mtu, ni zaidi ya rasilimali zetu hivyo tuitekenye sheria ya Uraia kwa ueledi itusaidie kuwadhibiti wasio Watanzania kujipa Utanzania wa muda.

Naamini tukiziba masikio nakuona potentiality ya Manji leo kuliko kuangalia Kwanza uraia wake tutafungua mjadala mkubwa huko mbeleni ambao utaligawa Taifa. Tujadiliane, tufunguane macho,tuelimishane na tumsaidie Rais na viongozi wengine kulitumikia Taifa kwa misingi Bora. Tusipowaambia tukaamini wanajua tutakua hatulitendei haki Taifa letu.

Uhamiaji tunawaomba mtoke adharani mseme ni raia au siyo raia. Msifanye Siri na msikubali kuambiwa na mwanasiasa nini mseme zingatieni sheria kumshauri mkuu wa nchi kwa lengo lakumwezesha afanye biashara,amtumie huyu mwekezaji na aruhusu taasisi nyingine kushiriakiana naye kwa hadhi sahihi ya Uraia siyo kwa adhi ya muda ambayo Samia akiondoka au kabla hajaondoka wanaweza kuibuka watu wakaiumbua serikali.

Nimechokonoa, endeleeni kutufunda.
 
Mtu kazaliwa Tanzania 🇹🇿 halafu leo unataka kumwita Mmarekani kwasababu ya kibali. Watanzania ni wajinga sana wakati mwingine utu wa mtu sio makaratasi yake.

Kila Mtanzania anajijua popole alipo mimi nimekaa US miaka 20 lakini mpaka leo wanasema mimi ni Mtanzania hakuna mtu anaweza kunitaja bila kuhusisha na Utanzania wangu maana Utanzania ni utu sio makaratasi siku hizi ndiyo watu wanataka kubadilisha Utanzania kuwa vitabu na vibali.

Mtu kazaliwa Tanzania ni Mtanzania awe na passport ni mambo ya sheria tu na yanabadilika kila siku lakini Manji ni Mtanzania na hakuna binadamu anaweza kubadilisha hilo passsport unapewa na watu lakini utaifa unapewa na Mungu.
 
Naona Jf inarudi kwenye ubora wake, umewasilisha hoja kubwa na inayohitaji intelligence kubwa kung'amua madhara ya utata wa Uraia katika uwekezaji au uchumi wa nchi.

Nakumbuka Abromovich bosi wa Chelsea alilazimika kuomba uraia wa Israel ili tu aweze kuingia Uingereza bila usumbufu baada ya kutokea mgogoro wa kidiplomasia na Urusi.

Watawala wetu hasa Wataalamu wa Uhamiaji wanapaswa kuliangalia hili suala kwa angle hizi:

1. Huyu mtu alishadhalilika na naamini ana hasira na hofu yakuweka fedha zake nchini.

2. Alipata hasara kubwa

3. Kesi nyingi alizotuhumiwa nazo zilibaki kwenye majalada

4. Akiwa na haki ya Utanzania huku akiwa pia Mmarekani anaweza kujimilikisha Mali au akapewa tenda itakamlazimu akope au Kampuni zake zikope. Aki default akakimbilia Marekani tutalazimika kulipa Kama garantor

5. Wapo Watanzania na wageni wanaomjua na wenye Siri ya Uraia wake, siku wakitoka adharani huku tukiwa tumedanganywa atafedheesha dola na kiti Cha Rais pia.

6. Binadamu uishi na uondoka Duniani, tusipotenda haki tukiamini tuna miaka mia ya mashirikiano Mwenyenz Mungu anaweza akawa ametupa miaka michache, uongo wetu utawarithisha wasiostahili kuirithi nchi yetu

7. Uraia siyo Siri

8. Uraia uliofichwa unaweza kutumika kutubomoa dhidi ya mataifa mengine

9. Tusiruhusu upendeleo kwa msukumo wa rangi Wala fedha tutende Kama tunavyowatendea wasio na kitu machoni pa waona Mali.

10. Tanzania ya kesho inategemea maamuzi yetu ya leo

Kama ni raia apewe haki yake, kama aliukana Utanzania aishi nakuwekeza kama mgeni.
 
Hahahah yani leo hadi mashabiki wa simba mmekuja huku kujaribu kumsagia kunguni Manji 😂😂 hebu acheni hizo, Manji karudi kusaidia ujenzi wa taifa.

Ni Mtanzania mwenzetu yule, huko Manyara kuna kioindi mavubo yote ya mbaazi alikuwa ananunua, aje ajenge nchi.
 
Mtu kazaliwa Tanzania 🇹🇿 halafu leo unataka kumwita Mmarekani kwasababu ya kibali. Watanzania ni wajinga sana wakati mwingine utu wa mtu sio makaratasi yake. Kila Mtanzania anajijua popole alipo mimi nimekaa US miaka 20 lakini mpaka leo wanasema mimi ni Mtanzania hakuna mtu anaweza kunitaja bila kuhusisha na Utanzania wangu maana Utanzania ni utu sio makaratasi siku hizi ndiyo watu wanataka kubadilisha Utanzania kuwa vitabu na vibali.

Mtu kazaliwa Tanzania ni Mtanzania awe na passport ni mambo ya sheria tu na yanabadilika kila siku lakini Manji ni Mtanzania na hakuna binadamu anaweza kubadilisha hilo passsport unapewa na watu lakini utaifa unapewa na Mungu.
Sasa Kama utanzania wa mtu unatokana na kuzaliwa Tanzania kwanini ukaukana na unasema makaratasi siyo kitu, hebu nenda airport bila hayo makaratasi na useme mi ni Mtanzania kama utapita.
 
Mtu kazaliwa Tanzania 🇹🇿 halafu leo unataka kumwita Mmarekani kwasababu ya kibali. Watanzania ni wajinga sana wakati mwingine utu wa mtu sio makaratasi yake. Kila Mtanzania anajijua popole alipo mimi nimekaa US miaka 20 lakini mpaka leo wanasema mimi ni Mtanzania hakuna mtu anaweza kunitaja bila kuhusisha na Utanzania wangu maana Utanzania ni utu sio makaratasi siku hizi ndiyo watu wanataka kubadilisha Utanzania kuwa vitabu na vibali.

Mtu kazaliwa Tanzania ni Mtanzania awe na passport ni mambo ya sheria tu na yanabadilika kila siku lakini Manji ni Mtanzania na hakuna binadamu anaweza kubadilisha hilo passsport unapewa na watu lakini utaifa unapewa na Mungu.
Hapana.

Wewe huwa ninakupinga sana juu ya hili, na unaelewa kwa nini, kwa sababu ya historia yako.

Sasa kuwa mTanzania kuishie kwenye utu?

Hakuna anayetumia uTanzania kwa fursa tu, bila hata ya kuujali huo uTanzania wa makaratasi?

UTanzania ni zaidi ya kuwa na makaratasi, ambayo wakati wowote mtu anaweza kuyatupilia mbali na hata kulihujumu taifa lake hilo la makaratasi, huo ndio tuuite utu?

Kuvaa uraia wa nchi kama nguo inayovuliwa wakati wowote, huo siyo uraia.

Inafahamika, sasa hivi watu wanachukua, si uraia wa nchi moja, mbili au hata tatu, mradi tu wafanye mambo yao.

Lakini naomba nirudi nyuma kwenye andiko lako, hasa hapo unapozungumzia uraia wa kuzaliwa.

Ndiyo, inafahamika kuna baadhi ya kundi hili wanaoweza kulisaliti taifa lao la kuzaliwa kwa maslahi yao binafsi au hata ya nchi yao mpya, lakini kawaida ya wengi ni kwamba nchi ya kuzaliwa mara nyingi ndiyo huwa inachukua nafasi kubwa zaidi bila kujali uraia wa nchi nyingine ya kujiandikisha kwa ajili ya maslahi.

Kwa mfano, itakuwa ni vigumu sana kwa mtu aliyezaliwa Tanzania, halafu ahamie na kuchukuwa uraia wa Kenya. Mtu huyu, mara nyingi itakuwa vigumu kwake kuondoa uTanzania ndani yake. Hali ni hivyo hivyo na kwa mtu toka Kenya aje achukue uraia Tanzania, ukenya wake huwezi ukauondoa.

Nimalizie kwa kusema kuweka msemo huu maarufu wa viongozi wetu wa zama hizi:

Wakati huu tulionao sasa hivi ni kutekeleza ile dhana mashuhuri ya "Kula na wewe ukubali Kuliwa" Hii ndiyo phylosophy inayotawala kwa sasa hivi. Sahau yote ya "Uraia na Utu"

You ain't seen nothing yet!
 
Kuna kanuni moja ktk taaluma ya sheria hususani sheria ya ushahidi ambapo wajibu wa kuthibitisha ni kwa yule anayesema ati jambo fulani lipo kwa namna aisemayo.

Mathalani, anayesema Manji ni raia wa Marekani yeye ndo apaswa kuthibitisha alisemalo.

Suala la Manji sio public concern, maana si kila mjadala unaoibuka mtandaoni na kujadiliwa kwa kasi ati ndo uchukuliwe kama jambo nyeti linalohitaji ufafanuzi kutoka Mamlaka ya nchi.

Kikubwa, ama awe Raia ama la suala ni kufuata sheria za nchi, maana nchi yetu ina raia wa nchini na wa kigeni, sasa tatizo lipo wapi?
 
Hoja namba 4 haina mashiko kabisa.

Nafikiri wewe ni maamuma ktk sheria, suala la mtu kukopa ama kuchukua tenda ni la kimkataba na mara nyingi, mikataba inayohusisha shughuli hizo baina ya pande mbili, huwekwa vifungu maalumu ili kukidhi matakwa na mambo yote nyeti yanayoweza tokea kama hilo unalo hofia.

Mfano wa kifungu kinachowekwa kwenye mkataba ni choice of law clause, ambapo mkataba utasema sheria ipi itumike baina ya pande mbili za mkataba, maana yumkini pande hizo zina uraia tofauti, je mahakama ipi itumike ya nchi gani? ect. hapa

Hakuna namna ya kukimbia ama uraia wa kigeni si kichaka cha kuepuka wajibu wa kimkataba na wa kisheria sababu mkataba uliokidhi vigezo vya kisheria na kitaalam una vifungu vya kueleza yote hayo.
 
Msitake kutupotezea muda na nyie Watu wa UHAMIAJI kujifanya hamjui Kitu wakati inajulikana wazi kuwa Manji aliwatoroka Kininja.

Hivi nyie UHAMIAJI pamoja na Polisi Tanzania si mliambiwa na Mwendazake kuwa hakikisheni Manji hatoroki? Ilikuwaje akawachoropoka?

au UHAMIAJI mnadhani wenye Akili hatujui ni hatua gani baadhi ya Watendaji wenu Waandamizi za Kinidhamu walichukuliwa?

Manji aliwatoroka kwa Mbinu za 'Kimedani' kabisa tena kwa Kuvalia ' Baibui ' akapita Tanga na kuibukia zake Kenya na kusepa.

Namalizia kwa kuwaambia Manji alitorokea (yupo) sasa nchini Canada kwa Dada yake akiwacheka tu na hana mpango wa kurejea kwa sasa.

Siku zingine msitupotezee muda sawa?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom