Uhamiaji kubadilisha tena hati za kusafiria

Uhamiaji kubadilisha tena hati za kusafiria

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
Membe.jpg
images
images

​

Idara ya Uhamiaji nchini imesema inatarajia kubadili pasipoti za kusafiria kutokana na kuwapo kwa matumizi mabovu kwa baadhi ya wananchi.

Akizungumza kwenye banda la Uhamiaji katika viwanja vya maonyesho ya 38 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa idara hiyo, Tatu Buruhani, alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na changamoto kubwa iliyopo kwa wananchi ya kuwa na hali ya udanganyifu katika uwasilishaji wa vitu ambavyo vinahitaji kupata hati hizo za kusafiria.

Alisema, wananchi wengi wamekuwa wakiwatumia mawakala maarufu kama vishoka wa idara hiyo kwa nia ya kupatiwa huduma hiyo kwa haraka na hivyo kuwasababishia wengi wao kutapeliwa ikiwa ni pamoja na kubadilishiwa vyeti vyao.

"Kinachotokea hapa ni kwamba, mwingine anachukua ile pasipoti anakwenda kuweka rehani, mwingine anauza, halafu anakuja kukwambia kwamba ameibiwa. Katika uchunguzi tuliofanya tumebaini kuwa hawaibiwi bali wanazitumia vibaya pasipo kutambua umuhimu wake," alisema Buruhani na kuongeza:

"Wengine wanapotaka pasipoti hawafiki huku, wanaishia kwa wale mawakala wetu, wanadanganywa kule, kule mtu anamwambia nipe labda laki tatu, nitakutafutia utapata, kitu ambacho hana uwezo nacho.

Matokeo yake wanakuja kulalamika kuwa wameibiwa, na hii ni kutokana na watu kutaka mambo ya haraka, na imani walizo nazo kuwa wakija huku ni lazima watoe rushwa, hiyo kwetu haipo."

Kwa mujibu wa Buruhani, utaratibu wa kubadilisha huduma ya hati za kusafiria ulianza mwaka 1961 kutokana na changamoto hizo na kwamba walifanya mabadiliko mengine katika miaka ya 1992 na 2005 na kwamba matarajio mengine ya kufanya hivyo ni mwaka huu.

Chanzo: Nipashe
 
haya sasa sijui watataka nini manake wanasumbua hawa watu,mara cheti cha baba chakuzaliwa mara cha bibi,mashaka tele...............
 
Wanatafuta hela za kustaafia wakina aaaaaaaaachikawe!!!!
 
Sababu za mabadiliko last time ilikuwa kuendana na mfumo wa kimataifa passport iwe readable kwenye database kimataifa, zoezi hilo lilifanyika kwa ufasaha na kwa ufanisi na sinazomeka po pote duniani. Hili la sasa halina uzito wa kutosha vinginevyo kuna ajenda nyuma ya pazia isiyowekwa wazi hadharani.
 
Serikali yangu ya CCM naipongeza kwa jitihada za kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao
 
Naomba Mungu hilo zoezi lianze pale yangu inapokaribia ku expire cause pasipoti ya Bongo ina masharti kama vile inapatika kwa mganga wa kienyeji.
 
Hapo UHAMIAJI kumejaa RUSHWA kuanzia watendaji wadogo hadi wakubwa. Pia kuna upendeleo sana wa waziwazi Kwa watu, ukifahamiana na mtu hapo ofisini kwao haupangi foleni na utachukua pasipoti Kwa siku si chini ya 2. Na Kwa taarifa yenu Ni laki 1 tu unapata pasipoti.
 
Huu ni wizi ntupu sasa,sababu za kipuuzi sana,kubadilisha ndio kuwaondoa vishoka??!! Urasimu wa kuipata passport ndio kumezalisha vishoka na hao vishoka ni mtandao wa wafanya kazi hapohapo migration,kweli watanzania tunapelekwa tu kama mizoga,miaka 10 tangu wabadilishe haijapita tayari wanatangaza wizi unakuja tena!!!
 
Hizo pesa bora wangepeleka hata wizara ya afya au elimu ,hii kero tu tu,
 
Kwa nini wasisubiri mchakato wa katiba mpya uishe ndio waje na hizo passport mpya? Viongozi wetu wa serikali hawana uchungu na fedha za walipa kodi hata kidogo. Je zikija serikali tatu na mwisho wa siku Zanzibar wakajitenga, hawaoni uwezekano tena wa passport mpya? Tunaweza tukawa na muungano na kila nchi ikawa na passport zake vile vile. baada ya bendera, wimbo wa taifa nk Zanzibar wamebakisha passport tu ili waende zao!
 
Sababu za mabadiliko last time ilikuwa kuendana na mfumo wa kimataifa passport iwe readable kwenye database kimataifa, zoezi hilo lilifanyika kwa ufasaha na kwa ufanisi na sinazomeka po pote duniani. Hili la sasa halina uzito wa kutosha vinginevyo kuna ajenda nyuma ya pazia isiyowekwa wazi hadharani.

CCM imeamua kukusanya pesa za kampeni kwa hiyo ngojeeni muone yatakayo tokea .Maana CCM bila kuhonga hakuna kitu , matokeo ni hayo sasa siku mambo mapya .Kwa nini mwaka huu na ghafla hivi ?
 
CCM imeamua kukusanya pesa za kampeni kwa hiyo ngojeeni muone yatakayo tokea .Maana CCM bila kuhonga hakuna kitu , matokeo ni hayo sasa siku mambo mapya .Kwa nini mwaka huu na ghafla hivi ?


Maisha yako yote unawaza chaguzi tu mkuu?
 
CCM imeamua kukusanya pesa za kampeni kwa hiyo ngojeeni muone yatakayo tokea .Maana CCM bila kuhonga hakuna kitu , matokeo ni hayo sasa siku mambo mapya .Kwa nini mwaka huu na ghafla hivi ?

Mradi wa Passports Mpya.

Mradi Vitambulisho vya kupigia kura vipya.

Mradi wa vitambulisho vya mkazi/uraia kupitia NIDA.

Halafu miradi yote hiyo ya mabillioni ya shillings hupamba moto pale tu uchaguzi unapokaribia,uchaguzi ukiisha kimyaaa!!!

CCM wanabaka uchumi wa Taifa hili kwa mbinu nyingi sana,zabuni ya hiyo miradi yote itapitia tu mikononi mwa makampuni ya kihindi lakini kati kati yenye venture na kampuni za makada wa CCM,ni aina nyingine tu ya EPA!!!
 
Hıı nchı nı ınaongozwa kıpumbavu sana, huu nı wızı unatengenezwa hapa, tutaambıwa lakı tena ya kubadılı, yn sıku uoga ukıtuısha watatutambua hawa
 
haya sasa sijui watataka nini manake wanasumbua hawa watu,mara cheti cha baba chakuzaliwa mara cha bibi,mashaka tele...............

Na hapo bado hujaambiwa kuonesha makaburi ya babu na bibi yako wa 7 ili kuthibitisha uraia wako!! Awamu ya wezi hii, hapo wanatafuta hela tu,:maana hatutabadilishiwa bure! Jamani Mr. dhaifu tuonee huruma wenzio!!!
 
Back
Top Bottom