Uhalisia wa taifa la Israeli

Tena biblia haikuandika awalaaniye wayahudi naye atalaaniwa. Makabila 10 yaliyounda Israeli hayapo hapo Israeli ya sasa bali kuna Wazayuni/khazar waliojipachika uyahudi wa mchongo. Israeli ya kubarikiwa ni ile ya mkusanyiko wa makabila 12 ya uzazi wa yakobo sio hawa waandaji wa mpinga kristo
 
Tena biblia haikuandika awalaaniye wayahudi naye atalaaniwa. Makabila 10 yaliyounda Israeli hayapo hapo Israeli ya sasa bali kuna Wazayuni/khazar waliojipachika uyahudi wa mchongo. Israeli ya kubarikiwa ni ile ya mkusanyiko wa makabila 12 ya uzazi wa yakobo sio hawa waandaji wa mpinga kristo
kwakweli ipo siku ukweli dhidi ya hawa mashoga utamuingia kila mtu tutawachapa bakora aise warudi kwao huko birmingham,washington watuachie nchi yetu sisi waisrael halisi
 
Ndugu yangu MAKOSHNELI nimeusoma "uzi" wako mwanzo mpaka mwisho, nimecheka sana.
Well, somehow you have a point. Ni ukweli kwamba miongoni mwa zile Kabila 12 za Israeli kuna ambao ni weusi, hilo halina ubishi.
Na kingine ambacho hujakizungumzia ni kuhusu kabila mbili zilizotoka kwa Yusufu yaani watoto wawili wa Yusufu ambao ni Efraimu na Manase, hawa walikuja kuwa makabila mawili tofauti, soma MWANZO 48:8-20
Efraimu na Manase ni mataifa makubwa mawili yaliyopo duniani kwa sasa, Efraimu ni UK na Manase ni USA. Hiyo ni siri inayojulikana na wachache sana, lakini huo ndiyo ukweli ulivyo.

Nakubaliana na wewe kuhusu baadhi ya points zako, mfano, ni kweli kuwa wale waluopo pale Israeli sasa hivi siyo Wayahudi halisi, hiyo ni kweli, lakini siyo wote, baadhi yao ni Wayahudi halisi kabisa kutoka kwa uzao wa Yuda. Kumbuka imeandikwa kuwa Bwana atajibakizia mabaki wachache ambao hawatachukuliwa kwenda utumwani.

By the way, uzi wako umenifurahisha. Hata Yesu Kristo pia hakuwa "Mzungu" kama tulivyoaminishwa bali alikuwa ni mtu mwenye sura na muonekano usiovutia. Soma ISAYA 53:1-5
"Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, na kama mzizi katika nchi kavu, yeye hana umbo wala uzuri na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko. Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu, lakini tulimdharau ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu na kuteswa. Ball alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona".

Inawezekana kabisa moja ya sababu ya Wayahudi kumkataa YESU kuwa ni MESSIAH, ni kutokana na yeye kuwa mtu mweusi, mwenye sura isiyovutia na umbo lisilovutia. Wayahudi ni watu waliokuwa na tabia za kum-judge mtu kutokana na muonekano wake wa nje (superficiality). Rejea jinsi walivyomchagua Sauli kuwa Mfalme wao, kutokana na muonekano wake na wakamdharau Daudi kutokana na muinekano wake.
kabila mbili zinatoka kwa yusufu ni UK na USA,ila hawa USA ni muunganiko wa states 50+ hiyo imekaaje?
 
Kwahiyo wale wayahudi wote siyo halisi? Halisi ni wapi sasa na wako utumwani nchi gani? Vipi kuhusu wale ethiopian Jews waliorudishwa Israel mwaka 1991, je na wao siyo halisi? lakini pia vipi kuhusu wale aliowaua Adolf Hitler kule Ujerumani wakati wa WW2 hawakuwa halisi? duuh! Kumbe Adolf Hitler aliua wayahudi fake? Nauliza tu!
NANI ALIBADILI NGUVU YA ULIMWENGU KWA RANGI NYEUPE?

Na: Joseph Mihangwa.

Tunaambiwa, mara ya mwisho kijana Yesu alionekana hekaluni akijadiliana na Mafarisayo na Masadukayo, Yerusalemu. Kuanzia hapo hakuonekana wala kusikika hadi miaka 18 baadaye alipotangazwa na Nabii Yohana [Mbatizaji] na kwa ubatizo uliofuatia, kabla kuanza kuhubiri Injili juu ya Ufalme wa Mungu; kifo, ufufuo na uzima wa milele. Alikuwa wapi; Misri au Ethiopia, kama hapo mwanzo?. Akifanya nini?. Je, alikwenda kujinoa juu ya dhana hiyo ambayo ilikuwa na mizizi, ibada na miundombinu maelfu ya miaka kabla ya kuingia Uyahudi?.

Hapana shaka kwamba dini ya Mussa, “Uyuda” [Judaism] na Ukristo, umechukua na kubakiza mengi kutoka Afrika ambayo hayakuwepo katika Jamii hizo kabla ya hapo. Mfano, ni imani juu ya Mungu mmoja, imani juu ya kifo na ufufuo na juu ya utatu mtakatifu na “siku ya hukumu” mbele ya kiti cha enzi [Soma kwa makini: “When Egypt Ruled the East” cha Profesa Steindorf; na “The Tempest and the Exodus” cha Ralf Ellis na pia Biblia takatifu, hasa Agano la Kale].

Sasa imeanza kudhihirika kwamba, Mwafrika alitawala dunia, kutoka Afrika hadi Yerusalemu, Uajemi, Amerika na India kabla ya kugeuziwa kibao na weupe hao. Jambo lililodhahiri leo ni kwamba, jamii zote za kale, kuanzia “Oldupai”, Misri, Yerusalemu, hadi Mesopotamia, ziliabudu mungu au miungu weusi, na kwamba “Ueusi” ulikuwa rangi ya kiungu na malaika, tofauti na leo ambapo tunaambiwa na kuaminishwa kinyume chake.

Mwafrika aliipiga na kuiteka Asia ya Kati yote na Palestina [Uyahudi] pia; nchi hizo zikawa zinalipa kodi na kutii mamlaka ya Mfalme “Pharao”. Ile vita kuu ya “Armagedon” ndiyo iliyozifanya nchi mateka wa Farao, na masaibu hayo ya kutawaliwa na Taifa la kigeni [gentiles] na matumaini ya kujikomboa kwa nguvu ya utaifa, yameelezewa vyema kimsahafu wa Kiebrania, Ufunuo 13: 1- 13; Isa 10:28-32].

Tunaweza kusema, kwamba juhudi za kabila la Kiebrania [Wayahudi] za kujitanua kisiasa na kiutamaduni baadaye zilikuwa za kidini [utamaduni] kwa kuongozwa na utaifa [Jewish nationalism] kwa nyumba [ukoo] ya “Israeli”. Tunaandika haya si kwa lengo la kukanusha uwepo wa Mungu muumba wa vyote, bali kwa lengo la kuimarisha hisia za uwepo wake na mpango wake wa makusudi kwa mwanadamu. Zaidi, ni kuhoji usahihi na namna Injili juu ya kumwelewa Mungu huyo, inavyowasilishwa kwetu kwa mzania wa upande mmoja wa historia ya mwanadamu; kwa kukweza [to glorify] zaidi utamaduni wa jamii moja dhidi ya jamii zingine kana kwamba Mungu ni mbaguzi kwa kuwaweka wanadamu na ubinadamu wao katika madaraja.

Hapo mwanzo, adui mkubwa pekee wa dini alikuwa “ukweli wa kisayansi” [facts of science] kwa kutoa changamoto juu ya mifumo na miundombinu ya kidini isiyo na majibu tosha juu ya maendeleo ya binadamu; lakini leo, ameongezeka adui mwingine ambaye ni “ukweli wa historia” [facts of history] ambayo lazima upate majibu juu ya maendeleo haya, kinyume chake “mkanda” wa kidini utazidi kulegea. Kinachokera zaidi ni juu ya namna Injili inavyowasilishwa kwetu, kwa kufuta ubao juu ya historia ya “uungu” kwa Mwafrika na mchango wake katika ustaarabu na maendeleo ya binadamu. Kero hii, isipopata jawabu sahihi, inaweza kuzaa kile kinachoweza kuitwa “Mgongano wa kitheolojia, kati ya ukale wa kimisahafu na uhalisia wa sasa” kutokana na tafiti, maendeleo ya sayansi na teknolojia. Na hili linazikabili zaidi dini kuu za mapokeo; Ukristo na Uislamu zenye chimbuko moja [lakini kwa nyakati tofauti] Uyuda [Judaism]; wote wana wa Abraham, au “Watu wa Kitabu” kwa maana “Agano la Kale”. Tofauti ya dini hizi mbili si juu ya Mungu anayeabudiwa kwa ibada; bali ni juu ya namna utamaduni wa Kiyuda na ibada zake, unavyowasilishwa kwa watu wengine wasio wa utamaduni huo [gentiles]; kutoka ukale wa misahafu [Agano la Kale] kwenda jamii [tamaduni] ambazo tangu kuumbwa kwa dunia, hazijashabihiana na utamaduni huo [Uyuda] wa kigeni.

Hiyo ni historia ya kale ya ustaarabu wa binadamu inayotaka kufunikwa kwa nguvu chini ya zulia la ubeberu na ubabe wa kiroho wa nchi za Magharibi kudhihirisha ubabe wao.

Lakini pamoja na historia hiyo ambayo utafiti wake huru unazidi kupata kasi zama hizi za sayansi na teknolojia, historia ya zama zetu na masalia yake inawasuta pia, kama tutakavyoona hivi punde.

Wataalam wa kwanza wa sayansi ya nyota na anga duniani [astronomers] walikuwa Waethiopia [Afrika]. Nao Wagiriki wa kale walijifunza elimu ya hesabu za maumbo [geometry] kutoka Ethiopia. Tena, tunafahamu sasa kwamba, Wamisri ndio waliobuni na kuanzisha kalenda ya mwaka wenye siku 365 inayotumika hivi leo ambapo mwaka ulianza mwezi wa uonekana angani kwa nyota “Sirus” iliyokwenda sambamba na kufurika kwa mto Nile. Mwaka ulikuwa na miezi 12 na siku ilikuwa na saa 24 zilizohesabiwa kwa saa ya maji [water clocks] na saa ya kivuli [sundial]. Mwanahistoria Fabre d’Olivet anatanabahi kwamba, hapo zama za kale, “Waafrika walitawala na kuongoza ulimwengu na dunia katika nyanja zote [sayansi, teknolojia, nguvu na uwezo], na walidhibiti Afrika na sehemu kubwa ya bara la Asia”.

Anafafanua kuwa, wakati Waafrika wakiongoza katika nyanja hizo, kabila la watu weupe lilikuwa lingali legelege, lisilo na ustaarabu kiwango cha kufananishwa na wanyama [savages]; hawakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri wala matumaini katika maisha. Kuhusu uvumbuzi wa nchi mpya [New lands], ni Waafrika waliovumbua Amerika na Visiwa vya “West Indies”, na si Mzungu Vespucci Amerigo [ambaye Amerika imetokana na jina lake], na Christopher Columbus, kama inavyoelezwa na Wanahistoria wa Kizungu.

Profesa Leo Weiner, katika kitabu chake kiitwacho “Afrika na Uvumbuzi wa Amerika” [Africa and the Discovery of America], anabainisha kuwa, Waafrika walizifikia nchi za Magharibi mapema kabla ya Wavumbuzi wa Kizungu, na huko waliendesha biashara na wenyeji wa nchi hizo kwa mafanikio makubwa. Anabainisha kuwa, Waafrika waliwahi kuifanya Amerika Koloni lao na kuitawala kama ambavyo tu Wazungu walivyokuja kutawala nchi zetu baadaye. Vivyo hivyo, “Wavumbuzi” wa Kihispania wanakiri, walipofika kwenye “nchi mpya” [Amerika na West Indies], walikuta makazi na himaya ya Kiafrika katika nchi hizo ambapo Makao Makuu ya Kudumu ya Himaya hiyo ya Waafrika, yalikuwa katika mji wa Darien, mwaka 1513. Naye mwanahistoria Harold G. Lawrence, katika kitabu chake kiitwacho, “Wavumbuzi wa Kiafrika wa Dunia mpya” [African Explorers of New World], anaeleza kuwa, alipofika katika visiwa vya “West Indies”, Christopher Columbus alifahamishwa na wenyeji wa visiwa hivyo juu ya uhusiano wa kibiashara uliokuwapo, kati yao na Waafrika. Lawrence ameandika ukweli huu kwa kutumia shajara [diaries] za Columbus za enzi hizo na ambazo zimehifadhiwa hadi leo.

Hizi si habari za kubuni au kubahatisha, bali ni historia sahihi kuhusu ukuu na ustaarabu wa Mwafrika dhidi ya, na kabla ya ustaarabu wa Mataifa mengine duniani. Si hayo tu, bali nafasi ya Mwafrika katika kuustaarabisha ulimwengu ilitambuliwa pia na Wafalme wengi miaka mingi kabla ya Kuzaliwa Kristo.

Alexander the Great, Mtawala na Jemadari Mkuu wa himaya ya Uyunani ya kale, alikuwa na Jenerali Kiongozi wa Jeshi Mwafrika katika jeshi lake, miaka ya 330 Kabla ya Kristo. Jenerali huyu aliitwa “Clitus the Black”. Vivyo hivyo, jeshi la Wayunani la enzi hizo liliongozwa na Majenerali na Ma- “Brigadier” wa Kiafrika. Na katika historia ya hivi karibuni [karne ya 18], Mwafrika aliyeitwa Abraham Hannibal, alikuwa Amiri Jeshi Mkuu [General-in-chief] wa Jeshi la Urusi chini ya Binti wa Mfalme [Empress] Elizabeth; na aliendelea kushika cheo hicho cha ukuu wa jeshi hadi utawala wa Mfalme “Peter the Great”. Kwa ushujaa wake, alitunukiwa nishani ya medali ya “The Red Ribbon of Order of Saint Alexander Newski”. Mmoja wa watoto wake aliongoza majeshi na kushinda vita kati ya Warusi na Waturuki huko Navarin, mwaka 1770. Mwafrika mwingine, Michael Egypteous, alikuwa Meja Jenerali katika Jeshi la “Peter the Great” ambaye, bila mipango, sayansi na mbinu zake za kisheshi, Jeshi la Urusi halikufanya kitu.

Kuhusu uongozi wa Kanisa, Mwafrika hakuwa nyuma. Kati ya mwaka 189 na 496 Baada ya Kristo [BK], Kanisa Katoliki, ambalo ndilo lilikuwa Kanisa pekee la Kikristo duniani enzi hizo, liliongozwa na Ma-papa [Popes] Waafrika. Hawa walikuwa ni Papa Victor, aliyeongoza ] kati ya mwaka 189 na 199; Papa Melchiades, 311 – 312; na Papa [Mtakatifu] Gelasious, mwaka 496. Katika kipindi kifupi cha utawala wake, Papa Gelarious anakumbukwa kwa kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wa Kanisa. Alirekebisha kalenda ya Watakatifu baada ya kutafakari upya nafasi za Watakatifu kwa waumini na Kanisa; akaondoa katika orodha hiyo majina ya Watakarifu Magreth na George. Aliingiza badala yake katika Biblia Takatifu, vitabu vipya vya “Hekima [ya Mfalme Sulemani]”, Yudith, Makabayo, Tobit, na Mhubiri ambavyo havikutumiwa na Mapapa waliomtangulia. Alipiga marufuku sherehe za kipagani kuhusishwa na Kanisa [Soma: Book of the Popes: Liber Pontificulis].

Itaendelea wiki ijayo. The post Nani kabadili nguvu-dunia nyeusi kwa rangi nyeupe? appeared first on Gazeti la Rai.
 
Back
Top Bottom