Uhakiki wa bima za magari!

Uhakiki wa bima za magari!

Itachukua muda bima zote kuingia kwenye data base. Kama umekata bima kwenye kampuni inayoeleweka huna sababu ya kuwa na wasiwasi.
But kama bima ako haijaonekana kwenye system si kuna haja ya kufatilia? Au unamute?
 
My experience with Jubilee has been wonderful. Nilipata shida ya windscreen (I had it insured). I got my payment within a very shortest time bila usumbufu!

So I recommend them. Niliwapenda kweli. Maana kwa hii bongo yetu vitu vingi ni figisu figisu!
daa mkuu kuna watu wanaitwa Britam mkoa fulani uko kwa chama kingine hawa jamaa full wababaishaji asee...
ujanja ujanja tu hamna lolote wezii.
yani ni shida tupu kabisa.
 
But kama bima ako haijaonekana kwenye system si kuna haja ya kufatilia? Au unamute?
Unajua kwa kanuni mpya kuanzia mwaka Jana, taarifa zote za stika lazima ziingizwe kwenye data base za kamishna wa Bima (Tira).

Inawezekana kabisa broker wako amekupa cover genuine na akapeleka malipo yako kwenye Kampuni yako ya Bima lakini pengine taarifa zako hazijawasilishwa Tira.
 
Bima- baada ya bima litakuja lingine kwa sasa tujiandae na matukio killa siku. Kila wakati na kitabu chake. Mungu asaidie.
 
Nlijua peke yangu kumbe wengi mana nlichanganyikiwa unalipa hela nyingi halafu bima haitambuliki
 
Kampuni yoyote ya Bima yenye leseni inatoa Bima halali ....tatizo watu wamekuwa wakikata ovyo kwa mawakala ambao wengine si waaminifu. Dawa hakikisha unapokata bima umepewa covernote/policy na receipt halali ambayo itakuwa attached na EFD receipt. Ukikamatwa kwasababu ya Bima kutokuwa halali lakini una vielelezo hivyo utakuwa salama na utaisaidia TIRA/Polisi kumkamata huyo wakala. Otherwise kuondoa hizo risk zote nenda kakate Bima direct kwenye Insurance Company badala ya mawakala.
Huo uwe ni utaratibu mpya,lakini miaka yote tumekuwa tunakata kwa hao mawakala na unapokwenda kukaguliwa gari lako Trafik wanazikubali.Cha muhimu mawakala waendelee kukatisha ila watoe risiti za EFD kama alivyosema mchangiaji hapo juu ili kuwapunguzia wenye magari usumbufu.
 
Makampuni makubwa kama Bumaco,Mgen,Sanlaam,Britam,Metropolitan,UAP,TANRE,CRDB,NIC,ZIC.
Nimekata ZIC miezi miine sasa mpaka sasa hazionekani mtandaoni baada ya kuwafuata wakasema ziko makao makuu wanaingiza, so hakuna cha kampuni kubwa wala ndogo zote bashite
 
Kwa siku kadhaa sasa mitandaoni kumekuwa na habari kuwa wenzetu wa usalama barabarani wanataraji kuanza uhakiki wa bima za magari, nimeona kuna link pia imewekwa ili kujua kama bima ni halali au la.
Kwa wenye taarifa tunaomba watueleweshe vizuri, au wenzetu wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari muwaalike hawa waheshimiwa walielezee ili tujue kinachotakiwa.
Mfano, nimejaribu kuingiza namba za gari hiyo link ikasema gari halina bima. Nimeshindwa kuelewa kuwa je si halali, kampuni nilikata bima haitambuliki auni nini!
Na je bima halali zinapatikana wapi, na je wakikuta si halali wanataraji kufanya nini!
Nawakilisha!

Inachotakiwa ni kule ulikokatia bima wsingize detail zako kwenye hiyo database.
Inasemekana huo utaratibu umeanza few weeks back, wengi hawajaingiza lakini sio kwamba bima yako ni feki, wape presdure waingize.
 
Aris ni broker Mkubwa sana wa Bima, hawawezi kucheza na hilo.

Umekata kwenye ofisi zao Sea cliff? Unaweza pia kuuliza kampuni yako ya Bima kama cover note number IPO kwenye system yao

walishahama sea cliff.. wako kwenye jengo lao jipya ARIS house next to KFC oysterbay
 
Hizo Bima zenu mmekata kampuni gani? Msitegemee hiyo system kufanya kazi.
TIRA ni wazembe sana,hiyo system ilitengenezwa ili kupunguza fraud lakini mpaka sasa haiwezi kufanya kazi.
Jambo la msingi ni kukata bima kwenye makampuni yanayojulikana.

Ni vyema ukatulia ujulishwe kuliko kuja na taarifa za uongo..

Makampuni makubwa kama Bumaco,Mgen,Sanlaam,Britam,Metropolitan,UAP,TANRE,CRDB,NIC,ZIC.

Makampuni makubwa hujataja hata moja hapo..

Ndio maana nilisema hiyo system ni mbovu bado haijakaa sawa. UAO ni kampuni kubwa sana na haina ubabaishaji.

Sio ubovu wa systems.. ni kwamba hili zoezi limearakishwa sana kabla halijakamilika vizuri..

Kampuni za bima pamoja na wakala wao wanapaswa kuweka taarifa za bima (za magari) kwenye "database ya TIRA inaitwa TIRA MIS

Changamoto ni kwamba kuna "sticker numbers" zinapaswa kuwekwa na TIRA kwenye iyo system (TIRA MIS) ila bado hawajaziweka..

Pia sticker za zamani hazipo kabisa kwenye hiyo sytem..

Mawakala wengine hawana hata computer kama kitendea kazi..

Bado mapema sana polisi kusumbua watu.. tuwape mda TIRA na makampuni ya Bima kwa ujumla..

Ukikamatwa na polisi kwamba bima yako sio halali waambie tu bado kampuni husika hawajaweka taarifa za bima yako kwenye system.. pia tembea na "Cover note" ile karatasi uliyopewa ulipokata bima kama dharura tu..
 
Yap, ila KWA sababu wewe mbongo kama Mimi huwa hatusomi wala kuuliza kuhusu policy zetu.

Kwa mfano unafahamu kuwa kwenye malipo ya madai unakatwa 5% ya malipo?

Kuna baadhi ya kampuni policy zao zinalipa limit ya 10 milioni ikiwa utasababisha uharibu (third party) na kama uharibifu ni zaidi ya hapo kinachobaki unalipa wewe!!

Kuna policy ukipata loss na dereva ana leseni iliyo chini ya miezi sita unapigwa 15% deduction kwenye malipo yako!
Mkuu upo sawa kabisa ila kwa makampuni mengi "Limit ya third party property damage" ni Tsh 30m.

Elimu ya bima bado ipo chini sana nchini kwetu..
 
Hapana system ya Tira wanaendelea kuload majina kulingana na makampuni ya bima yalivyowasilisha orodha na malipo kulimgana na sticker walizotoa, nina bima Metropolitan comprehensive bado haijasoma, ns hata kwenye maelezo yao kwenye website ya Tira wameekeza kuwa tuwe na subira wanafanyia kazi
 
Kwanza wangehakiki makampuni ya bima. A wrong foot again.
 
Kuna broker wangu aliniambia hii kitu. Yaani nikikata kwake ikitokea issue watashughulikia haraka kwasababu yeye anawapelekea wateja wengi, ila mimi wanaweza kunisumbua kwasababu ni individual tu.
Mkuu tupe contact za broker wako, mobile namba hasa yenye whatsapp, please...
 
Back
Top Bottom