Uhakiki wa bima za magari!

Uhakiki wa bima za magari!

Hizo Bima zenu mmekata kampuni gani? Msitegemee hiyo system kufanya kazi.
TIRA ni wazembe sana,hiyo system ilitengenezwa ili kupunguza fraud lakini mpaka sasa haiwezi kufanya kazi.
Jambo la msingi ni kukata bima kwenye makampuni yanayojulikana.


Kama yepi Mkuu, maana ukifika kwenye ofisi zao unaona wana vibali vya serikali kuoperate insurance agency business. Nitajuaje kuwa hii no ofisi ya bima fake na ile pale ni original
 
Kama yepi Mkuu, maana ukifika kwenye ofisi zao unaona wana vibali vya serikali kuoperate insurance agency business. Nitajuaje kuwa hii no ofisi ya bima fake na ile pale ni original

Nenda kwenye kampuni ya bima na sio kwa agent, bumaco, Metropolitan, mgen, Zanzibar insurance, britam, jubilee ni kampuni nzuri ambazo hazisumbui kwenye kufatilia madai yako.
 
Wakuu tunaomba wenye kujuwa quote ya comprehensive cover kwa mwaka ya Nissan Cube 2007, 1500cc, petrol, miaka ya dereva 49, milage 100,000, thamani ya gari 12m/=, tafadhali...
 
Kuna mfumo wa kuhakiki bima za magari kwa kutumia application ya TIRAMIS, inapatikana playstore, ukitumia app hii unaeka tuu namba ya gari utaona kabisa bima ni ya kampuni gani na inaisha lini. Mi nikikata tuu bima sitoki kwenye ofisi ya wakala mpaka nione imesomeka kwenye system,,. Usipoona hivyo ndio maswali yoote yaende kwa aliyekukatia bima.
 
Back
Top Bottom