Uhakiki wa bima za magari!

Uhakiki wa bima za magari!

Shedafa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2008
Posts
802
Reaction score
175
Kwa siku kadhaa sasa mitandaoni kumekuwa na habari kuwa wenzetu wa usalama barabarani wanataraji kuanza uhakiki wa bima za magari, nimeona kuna link pia imewekwa ili kujua kama bima ni halali au la.

Kwa wenye taarifa tunaomba watueleweshe vizuri, au wenzetu wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari muwaalike hawa waheshimiwa walielezee ili tujue kinachotakiwa.

Mfano, nimejaribu kuingiza namba za gari hiyo link ikasema gari halina bima. Nimeshindwa kuelewa kuwa je si halali, kampuni nilikata bima haitambuliki auni nini!

Na je bima halali zinapatikana wapi, na je wakikuta si halali wanataraji kufanya nini!
Nawakilisha!
 
Hata mimi na jamaa zangu kama 6 hivi wote tumecheki inasema gari zetu hazina bima.Sijui tutachukuliwa hatua sisi au vile vi ofisi vilivyotukatia hizo bima?
 
Hizo Bima zenu mmekata kampuni gani? Msitegemee hiyo system kufanya kazi.

TIRA ni wazembe sana,hiyo system ilitengenezwa ili kupunguza fraud lakini mpaka sasa haiwezi kufanya kazi.
Jambo la msingi ni kukata bima kwenye makampuni yanayojulikana.
 
Hizo Bima zenu mmekata kampuni gani? Msitegemee hiyo system kufanya kazi.

TIRA ni wazembe sana,hiyo system ilitengenezwa ili kupunguza fraud lakini mpaka sasa haiwezi kufanya kazi.
Jambo la msingi ni kukata bima kwenye makampuni yanayojulikana.
Unaposema makampuni yanayojulikana, una maana gani?

Unaweza kufafanua please!
 
Issue hapa nadhani sio makampuni ya BIMA ila ni hizo kampuni zinapeleka michango sehem husika!? Mfano umekata bima yako kwa wakala wa bumaco,je huyo wakala anapeleka huo mchango makao makuu ya hiyo kampuni!? Maana wakala wengi hua wanakula hizo hela sasa ukipata ajari na kuanza kufuatilia ndio utakapo shangaa na kuzungushwa kutakako jitokeza.
 
Makampuni makubwa kama Bumaco,Mgen,Sanlaam,Britam,Metropolitan,UAP,TANRE,CRDB,NIC,ZIC.
Kampuni yoyote ya Bima yenye leseni inatoa Bima halali. Tatizo watu wamekuwa wakikata ovyo kwa mawakala ambao wengine si waaminifu. Dawa hakikisha unapokata bima umepewa covernote/policy na receipt halali ambayo itakuwa attached na EFD receipt. Ukikamatwa kwasababu ya Bima kutokuwa halali lakini una vielelezo hivyo utakuwa salama na utaisaidia TIRA/Polisi kumkamata huyo wakala. Otherwise kuondoa hizo risk zote nenda kakate Bima direct kwenye Insurance Company badala ya mawakala.
 
Pesa inatafutwa na tochi sasa, wanamulika kila uchochoro.

Ngoja nisubiri vipimo nipo NIC.
 
Yani jamani hawa wanasumbua hadi basi..mi nimekata ARIS na sijaona!

Haki ya Mungu haya mambo yana mwisho asee..
 
Hivi tunahakiki vipi? Maana sina uhakika kama gari yangu ina bima ya kweli kweli.
 
Mimi pia nilihakiki sikuona. Nilikata bima ya Jubilee kupitia kwa wakala. Nilienda ofisi ya wakala kuwaulizia kulikoni wakanieleza ndio wanaingiza data za wateja waliokatakwao wapeleke Jubilee then Jubilee waziupload TIRA. nadhani makampuni mengi ya bima ndio yatakua kwenye process hiyo ya ku-upload hizo info za wateja wao, pia wamesema mtandao wa TIRA sometimes unasumbua.....
 
Aris ni broker Mkubwa sana wa Bima, hawawezi kucheza na hilo.

Umekata kwenye ofisi zao Sea cliff? Unaweza pia kuuliza kampuni yako ya Bima kama cover note number IPO kwenye system yao
Yap nilikatia sescliff kabla hawajahama (nasikia wamehama)
 
Makampuni makubwa kama Bumaco,Mgen,Sanlaam,Britam,Metropolitan,UAP,TANRE,CRDB,NIC,ZIC.
Naomba kukusahihisha kuwa crdb siyo kampuni ya bima ila ni wakala wa bima,pili tan re ni kampuni ya bima ila haifanyi kazi moja kwa moja na mteja (tunaiita reinsurance company).

Kama huoni bima yako kuwa imesajiliwa nenda ulipokatia au kampuni husika utafanyiwa uhakiki na kusajiliwa hapo hapo.
 
Back
Top Bottom