SoC03 Uhai wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

Sia Kanje

Member
Jun 13, 2023
26
22
Uhai maana yake ni Yenye pumzi ,katika maisha ya Mwanadamu uhai upo ndani ya nafsi ambapo Kuna Akili ,hisia na roho ,na kwa namna ya nje Mwanadamu Amebeba mwili . Ili Mwanadamu awe na uhai ni muhimu nafsi yake Yaani Akili ,roho na hisia viweze kufanya kazi vizuri .

Uhai wa Taifa ni jumla ya vitu vilivyo ndani ya Taifa ambavyo kwa hivyo vinaijenga taswira ya Taifa kwa nje Yaani mwili Wa Taifa , mwili Wa Taifa umeundwa na maliasili na rasilimali hivyo basi uhai wa Taifa la Tanzania upo ndani ya nafsi ya Taifa ambayo ni Elimu .

Kwa upande Wa Mwanadamu nafsi ni kama injini ndiyo inayosababisha vitu vingine vikafanya kazi ndani ya mwili vivyo hivyo katika Taifa Elimu ni injini ndiyo inayosababisha utendaji mzuri katika nyanja zote ndani ya Taifa ,na katika Taifa Elimu ni kama chumvi inatia ladha kwenye nyanja zote za kimaendeleo kama vile mfumo Wa uzalishaji , biashara,uongozi na utawala Bora ,kilimo na uwekezaji .

Maendeleo ya Taifa huletwa na maendeleo katika nafsi ya Taifa ambayo ni Elimu , hatuna budi kuleta maboresho ya Elimu inayotolewa nchini katika ngazi zote ili tuweze kupata uongozi na utawala hai ,uchumi hai, kilimo hai , na biashara hai kwasababu nafsi hai huzaa hai na nafsi iliyokufa huzaa mapooza .

Tanzania kama Taifa lenye nguvu Duniani likifanikiwa kutoa Elimu ambayo italandana na Hali halisi ya Mwanadamu na mazingira ya nchi ,taifa hili litazalisha viongozi Bora watoa suluhu ,wachumi wabobezi watakao ongeza thamani ya fedha ,wanasheria na mawakili wazuri Wa kuitetea katiba na haki za Wananchi .

Hata hivyo hakuna Mwanadamu anaeweza kufanya kazi vizuri Ikiwa nafsi yake imekufa ni lazima matokeo ya kazi yatakuwa mapooza , vivyo hivyo katika Taifa Letu hakuna maendeleo tutakayopata Ikiwa Elimu tunayotoa imekufa ni lazima tutapata matokeo mapooza kama vile viongozi mapooza ,biashara ,viwanda ,uchumi ,uwekezaji vyote mapooza na pia tutatengeneza vizazi mapooza Karne kwa Karne .

Katika Taifa Letu La Tanzania Tunahitaji zaidi Elimu ya maendeleo binafsi , elimu ya maendeleo binafsi ni Elimu inayomsaidia mtu kupata maendeleo ndani ya nafsi yake kabla ya Yale maendeleo ya nje kama vile maendeleo ya kiuchumi, biashara,kazi Bora .

Elimu ya maendeleo binafsi ni elimu Inayogusa mtu Wa ndani Yaani utu ,Ikiwa ni pamoja na nafsi ,Akili na hisia (moyo) .
elimu hii ni muhimu sana kwasababu inamsaidia mtu kujitambua yeye ni nani ?, Kutambua nguvu aliyonayo ndani , kutambua kipaji chake na kuanza kuishi ndani yake ,ubunifu ,uvumbuzi,na pia watu wengi wakipata hii elimu itakuwa ni suluhisho la matatizo sugu yanayolisumbua Taifa kama vile ukatili Yaani ubakaji, ulawiti ,rushwa , mauwaji ,matatizo ya afya ya akili ,wanyanga'nyi ,uhujumu uchumi na wasomi mapooza . Hivyo basi elimu ya maendeleo binafsi inamsaidia mtu kutenda mema kwasababu ni mema na kuacha mabaya kwasababu ni mabaya hadharani na sirini .

Elimu ya maendeleo binafsi imegawanyika katika makundi mengi lakini Mimi nitaeleza makundi manne tu ;

Elimu ya nafsi ; hii ni elimu inayohusiana na utu Wa ndani Wa mtu mwenyewe , mwili ni kama bebeo tu ila mtu halisi ni nafsi . Ndani ya nafsi ndipo MUNGU alipoweka nguvu kubwa sana ,ndipo penye utajiri mwingi ,Ipo thamani kubwa kuliko dhahabu na Tanzanite ndani ya nafsi ya mtu , Kuna vipawa vikubwa , ubunifu , Wa Kutisha , ni muhimu watu wafundishwe guvu iliyopo ndani ya nafsi kazi za nafsi ,na jinsi ya kutumia nguvu walizonazo ndani ya nafsi katika kutumia rasilimali tulizonazo Ili kupata maendeleo. Kwa kumalizia niseme hata hivyo ubunifu ,uvumbuzi ,makampuni ,viwanda , uwekezaji uongozi na utawala Bora ,uchumi ,kilimo vyote vipi ndani ya nafsi za watu .

Elimu Ya Akili ; hii ni elimu ambayo itamuwezesha mtu kutumia Akili yake vizuri na kutambua upeo wake Wa Akili aliyozaliwa nayo kutoa taarifa ,kupokea taarifa ,kufanya maamuzi na kutoa suluhisho ,jinsi ya kuilinda Akili ,kuihuisha Akili na kuzidi kuboresha Akili .

Elimu Ya hisia ; hii ni elimu ambayo itamsaidia mtu kudhibiti hisia zake na hisia za watu wanaomzunguka ,ni muhimu sana wafundishwe kuwa zipo nguvu za Ajabu Sana Ndani ya Hisia zao Ambazo zikitumika vizuri zitaleta matokeo chanya ,watu wapewe uelewa kwamba ndani ya Hisia zao siyo mahali pa kujaza maumivu ,hasira ,Chuki ,visasi ,wivu Bali ni pa kukaa nguvu laini kama vile Upendo ,furaha ,huruma ,unyenyekevu , hivyo basi watu wakifundishwa jinsi ya kudhibiti hisia zao hatutasikia tena mauaji,ukatili ,uhujumu uchumi ,ubakaji ,kwa kumalizia niseme hivi watu wakiweza kuzilinda hizi nguvu laini zilizopo kwenye hisia zao nchi Yetu itakuwa mahali salama ,vinginevyo tutajikuta tunaweka Sheria Kali juu ya haya huku tunazalisha waalifu Kila siku .

Elimu ya rohoni ; hii ni elimu ambayo watu wanafundishwa jinsi ya kumtegemea MUNGU na kuishi kadiri ya Mapenzi ya MUNGU , watu wajue nguvu za MUNGU katika maisha Yao ya Kila siku , kwasababu watu wakiwa na hofu ya MUNGU ni rahisi Sana kuliombea taifa na pia watu wakiwa na hofu ya MUNGU ndani ya mioyo Yao siyo rahisi kutenda Ukatili .

Hivyo basi Ili tuweze kupata maendeleo na mabadiliko chanya ndani ya Taifa Letu Elimu ya maendeleo binafsi ipewe kipaombele katika ngazi zote za Elimu kwasababu viongozi Bora ni wale walioendelea binafsi , ni wale wenye utulivu Wa nafsi , watendaji kazi Bora ni wale wenye utulivu Wa nafsi hata hivyo muogope Sana mtu mwenye Akili alafu mtulivu Wa nafsi .
 
Naombeni kura zenu katika andiko langu hili
 
Back
Top Bottom