Ugonjwa wa akili

Tiger

JF-Expert Member
Nov 30, 2007
1,747
386
Wana jf,
naamini kuwa binadamu huwa tunapenda kujiuliza maswali kulingana na mazingira na matukio.
Leo nilikutana mtu ambaya anaonekana kuwa na "ungojwa wa akili" basi nikajikuta najiuliza, ni kwa nini mtu anapokuwa na haya matatizo anakuwa violent(sio wote)?
Unakuta anataka kupiga watu,anakimbiza/fukuza magari, wengine wanaua au kijiua, kujipiga makofi na vitu kama hivyo.
Kwa wenye ufahamu, mnaweza kuniambia nini hasa kinatokea kwenye ubongo na part gani hasa ya ubongo inapelekea yote haya?
Usisite kutoa detailed information i will be ready to comprehend.
Asanteni.
 
magonjwa mengi ya akili husababishwa na kupungua au kuongezeka kwa vichochezi vya ubongo (dopamine, serotonin na catecholamines) sasa mara nyingi vikizidi mtu anakuwa na kichaa cha kuchangamka (mania) vikipungua anakuwa na kichaa cha upole (depression), au anaweza kuwa anaswitch upole na kuchangamka (bipolar disorder). pia hivi vichochezi huwa vina athari kutokana na eneo la ubongo lililoathirika mfano ubongo wa mbele unaohusika na kufikiri ikiathirika mtu mtu anakuwa na ufikiri mbovu, sehemu ya ubongo inayohusika na motio (striata nigra kama sijakosea) basi mtu anashindwa kumove kama wale wenye parkinsonism. hope you will comprehend.
 
magonjwa mengi ya akili husababishwa na kupungua au kuongezeka kwa vichochezi vya ubongo (dopamine, serotonin na catecholamines) sasa mara nyingi vikizidi mtu anakuwa na kichaa cha kuchangamka (mania) vikipungua anakuwa na kichaa cha upole (depression), au anaweza kuwa anaswitch upole na kuchangamka (bipolar disorder). pia hivi vichochezi huwa vina athari kutokana na eneo la ubongo lililoathirika mfano ubongo wa mbele unaohusika na kufikiri ikiathirika mtu mtu anakuwa na ufikiri mbovu, sehemu ya ubongo inayohusika na motio (striata nigra kama sijakosea) basi mtu anashindwa kumove kama wale wenye parkinsonism. hope you will comprehend.

Heshima kwako mkuu.
Hiyo bipolar disorder inajibu swali langu kwa sehemu kubwa.
Ila naomba kuuliza tena, je, kuna therapy inayoweza kufanyika kwa mgonjwa bila kutumia vidonge au sindano? Hii inawezekana kwa stage gani?
Na kama ipo hiyo therapy how does it take effect to the chemistry of the brain?
Thank u.
 
kuna kitu inaitwa cognitive therapy, ni tiba ya kisaikolojia sababu hizi mental illness mara nyingi zinakuwa triggered na psychological problems ukiachana na wale waajali. hapa mgonjwa hufanyiwa psychoanalysis kugundua kitu kinachomsumbua na ndipo njia ya utatuzi hutafutwa matokeo hutegemea adherence ya mgonjwa kwenye maelekezo na kama tatizo lililogunduliwa ni lenyewe, nahisi inakuwa effective zaidi kabla ugonjwa haujamuathiri sana mgonjwa kiasi ashindwe kujitambua. ni tiba yenye matokeo kwa watu waliochanganyikiwa sababu ya mapenzi, ugumu wa maisha, masomo na mambo kama hayo
 
Katika sehemu ya kwanza ya makala ya upungufu wa akili tuliona makundi ya upungufu wa akili, ukubwa wa tatizo hili, visababishi na pathofiziolojia yake.
LOBES%20OF%20THE%20BRAIN.jpg

Sehemu hii ya pili tutaangalia dalili, vipimo vya uchunguzi, tiba yake pamoja na jinsi ya kujikinga na tatizo hili la upungufu wa akili.



Dalili na Viashiria vya Upungufu wa Akili

  • Kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza
  • Upungufu wa kumbukumbu (deficits in memory skills)
  • Matatizo katika kufahamu mambo ya kijamii
  • Upungufu wa uwezo wa kutatua matatizo
  • Kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe (kama kufunga vifungo vya shati nk)
  • Kuendelea kuwa na akili za kitoto
  • Kupungua uwezo wa kusoma
  • Lack of social inhibitors
  • Kushindwa kufikia vigezo vya ukuaji wa kiakili
  • Kushindwa kumudu masomo shuleni
  • Lack of curiosity
Utambuzi wa Upungufu wa Akili
Utambuzi wa upungufu wa akili huusisha

  • Historia ya mgonjwa – Kuhusu mazingira ya sehemu anayoishi, matumizi ya madawa ya aina yoyote, historia ya magonjwa ya akili, tabia ya awali na ya sasa ya mgonjwa, tiba aliyowahi kupata kuhusu ugonjwa wa akili, jinsi familia na wahudumu ya afya wanavyomchukulia kuhusu hali yake na nk.
  • Vipimo vya afya
  • Vipimo vya mfumo wa fahamu
  • Mental status examination –Hufanywa na daktari
  • Vipimo vya uchunguzi – Vipimo vya ugonjwa wa kaswende, Rubella, Toxoplasmosis, Cystomegalo virus, Herpes simplex, vipimo vya mkojo (kuangalia phenylketonuria), kipimo cha EEG kama amewahi kupata degedege, vipimo vya damu na nk.
  • Vipimo vya saikolojia - The Bayley Scales of Infant Development, The Stanford-Binet Intelligence Scale, The Wechsler Intelligence Scale for Children-III, and The Wechsler Preschool and Primary Scale of Intelligence-Revised.
Vigezo vinavyotumiwa na tabibu wa magonjwa ya akili kutambua mgonjwa wa upungufu wa akili kwa watoto {DSM IV (diagnostic and statistical manual) for mental retardation coded on AXIS II (paediatrics)}

  1. IQ ya 70 au chini yake wakati mgonjwa anafanyiwa kipimo cha akili (IQ test). kwa mtoto mchanga, hupimwa uwezo wa ufanyaji kazi kwa vipimo vya kliniki (clinical judgement)
  2. Kutokuwa na uwezo au upungufu katika kujihudumia mahitaji yake ya kimaisha kutokana na umri wake au utamaduni wake, kuwepo kwa angalau vigezo viwili kati ya hivi basi mgonjwa ndio anatambuliwa kuwa na upungufu wa akili, vigezo hivyo ni kama vifuatavyo;
a. Kushindwa kuwasiliana na watu,
b. Kushindwa kujihudumia katika suala zima la usafi, mavazi, chakula (self care) na kushindwa
c. Kuishi nyumbani
d. Kujumuika na watu
e. Kutumia huduma za jamii
f. Kutokuwa na muelekeo (self direction)
g. Kutokuwa na akili darasani au kushindwa kumudu masomo
h. Kushindwa kufanya kazi
i. Kushindwa kustarehe (leisure)
j. Afya (health)
k. Usalama (safety)
l. Kutokea kwa tatizo hili kabla mtu kutimiza miaka 18



Tiba ya Upungufu wa Akili
Tiba ya mtu mwenye upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili


a. Huduma za mtu mwenye upungufu wa akili

  • Muathirika kuhudumiwa nyumbani na familia pamoja na familia kupewa elimu ya kijamii
    Dysmorphic%20Features%20of%20MR.jpg

    ili kuweza kumhudumia
  • Muathirika kuishi katika nyumba za kijamii (foster home) au group home
  • Rehabilitation centers
  • Asasi za kijamii kusaidia familia ili kuweza kumudu gharama za kumhudumia ndugu au jamaa yao wenye upungufu wa akili.
  • Ushauri nasaha kwa familia ili kuweza kuhimili msongo wa mawazo pamoja na tabia za mtu mwenye upungufu wa akili
  • Tiba sahihi kwa matatizo ya kisaikolojia pamoja na tabia za mtu wa upungufu wa akili
  • Behavioral modification (using positive and negative reinforcement principle)
  • Matatizo ya kiafya kama degedege yanahitaji tiba sahihi
  • Kumpima uwezo wake wa kiakili mara kwa mara ili kujua ni mahitaji gani ya shule muathirika anahitaji. Kupima mara kwa mara ni njia sahihi kwani wengi hupata nafuu au huonesha maendeleo mazuri na hivyo mahitaji kubadilika kadri muda unavyokwenda
b. Tiba yenyewe

  1. Shule maalum
  2. Tiba ya sauti au lugha (speech/language therapy) kutoka kwa madaktari bingwa wa kutibu sauti (Speech/language therapists)
  3. Behavioral therapy – Matibabu ya kurekebisha tabia ya muhusika
  4. Occupation therapy
  5. Huduma za kijamii kwa familia na muhusika
  6. Kubadilisha mfumo wa maisha (health lifestyle) kula lishe bora, kufanya mazoezi, kujihudumia, kupunguza msongo wa mawazo kwa wenye upungufu wa akili
  7. Ushauri nasaha mara kwa mara au kuhudhuria program maalum za ushauri nasaha na mambo ya kijamii
  8. Dawa za ugonjwa wowote wa akili muhusika alionao (antipsychotic medications)
  9. Dawa za maumivu kulingana na kiwango cha maumivu
  10. Mawasiliano kwa kutumia maandishi, sauti au picha na hata lugha ya vitendo kwa watu wenye upungufu wa akili ili kuleta maelewano wakati wa tiba na kumfanya muathirika kupata hamasa ya kuendelea na tiba
  11. Kuwafanyia uchunguzi kama wananyanyaswa kijinsia kama kubakwa nk. Watu wenye upungufu wa akili mara nyingi hubakwa na hivyo kuwafanya kuwa wakali au kuwa na hasira. Daktari anahitajika kugundua anapoona ishara hii kwa mgonjwa wakati wa kumpima.
  12. Kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga watu wenye upungufu wa akili
Je, kinga ya Upungufu wa Akili ni Nini?
Kinga ya upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili


1. Kinga ya awali (Primary Prevention)

  • Kuboresha huduma za afya na kijamii ili kuondoa tatizo la utapia mlo, kuongeza uhamasishaji, kuondoa tatizo la kuzaa watoto njiti, na kutoa elimu kwa kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya, unywaji pombe, magonjwa ya zinaa na nk wakati wa ujauzito
  • Kuboresha huduma za afya za kina mama, tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuzuia maambukizi, ajali (trauma), madhara mbalimbali wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba, na magonjwa ambayo yanaweza kumuathiri mtoto kabla, wakati na baada ya kuzaliwa.
  • Mtoto kupata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa wa polio, ugonjwa wa surua na nk.
  • Kuwaelimisha kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya na umuhimu wa kuhudhuria kliniki
  • Kutoa ushauri nasaha kwa wazazi ambao wanaathari za viashiria vya asili (genetic counseling to high risk group)
  • Kufanya tafiti juu ya sababu au vyanzo vya upungufu wa akili pamoja na tiba yake.
  • Kuwaelimisha mama wajawazito jinsi ya kujifungua salama na umuhimu wa kuwasikiliza wahudumu wa afya wakati wa kujifungua kwani mara nyingi kina mama huwakosesha watoto wao hewa na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata upungufu wa akili na ndio sababu wahudumu wa afya wanakuwa wakali sana kwa kina mama wanaofanya hivyo kuchelea mama asipate mtoto mwenye tatizo hili. Hii itasaidia kuondokana na ile dhana ya kwamba kujifungua hospitali za serikali kwa mama mjamzito ni adhabu kwani huwa wanapigwa.
2. Kinga ya baadae (Secondary Prevention)

  • Ugunduzi wa mapema na tiba sahihi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika kama phenylketonuria, hypothyroidism nk.
  • Ugunduzi wa mapema wa matatizo katika mfumo wa fahamu, mabadiliko ya tabia na hisia ili kukabiliana nayo mapema.
  • Ugunduzi wa magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa kaswende, Rubella nk mapema kabisa ili muathirika apate tiba haraka
  • Kufanya kipimo cha Ultrasound, CT, MRI, mapema ili kuweza kugundua kama mtoto ana kilema chochote katika maumbile, hii itasaidia kupanga na kumhudumia mapema zaidi ili kudhibiti tatizo.
  • Ugunduzi wa upungufu wa akili mapema zaidi kwani kuchelewa kutambua huchelewesha tiba yake..
Mara nyingi watu walio na upungufu wa akili uliopitiliza (profound mental retardation) hufa katika umri mdogo au kabla ya kutimiza miaka 20. Wale wenye upungufu wa akili aina ya mild na moderate, umri wao wa kuishi hupungua sana (reduced life expectancy)


Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Mirembe Psychiatry Referral Hospital (Dodoma, Tanzania) anayefanya shahada yake ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Akili
 
MATATIZO YA AKILI (MENTAL RETARDATION)



Brain_(1).jpg

Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya utambuzi na kutafakari (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.


Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology)
Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.


Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV) kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18. Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).


Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni nini?


Tabia za kuendana na mazingira ni jinsi mtu anavyoweza kumudu matakwa ya kujihudumia mwenyewe kila siku pasi na kumtegemea mtu yoyote kutokana na umri wake, tabaka lake, utamaduni pamoja na jamii inayomzunguka kutokana na vipengele viwili kati ya hivi vifuatavyo;

  • Mawasiliano (Kuweza kuwasiliana na watu)
  • Kuweza kujihudumia katika shughuli zinazohitaji kutumia akili (functional academic skills)
  • Kuweza kuishi mazingira ya nyumbani na kazini
  • Kuwa na uwezo wa kuchanganyikana na jamii katika masuala ya afya na usalama wake
  • Kuweza kutumia huduma za jamii ambazo zitamfanya kuishi maisha ya furaha
Ni vizuri kutambua ya kwamba tabia hizi hutegemea sana elimu, uhamasishaji, tabia za mtu binafsi, kupewa fursa za kijamii na za kiufundi (vocational skills), matatizo ya akili na magonjwa mbalimbali ya akili.


Intelligence kitaalamu ni uwezo wa ubongo katika kufikiri, kutatua matatizo, kuchagua au kuwa na busara (reason), na kuelimika.


IQ= Mental age (Umri wa akili) × 100
Chronological age (Umri wa kawaida wa binadamu)


Makundi ya Upungufu wa Akili Kipimo cha IQ


Upungufu wa akili uliopitiliza kabisa (Profound Mental Retardation) Chini ya 20
Upungufu wa akili mkubwa (Severe Mental Retardation) 20-34
Upungufu wa akili wa kati (Moderate Mental Retardation) 35-49
Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) 50-69
Upungufu wa akili wa kawaida (Borderline Intellectual Functioning) 70-84


Mtu aliye kwenye kundi la upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) anaweza kuelimika, na Yule aliye na upungufu wa akili wa kati, mtu huyu anaweza kufunzwa kazi za kumuwezesha kumudu maisha yake ya kila siku. Wale walio na upungufu wa akili mkubwa (Severe MR) na kundi la waliopitiliza (Profound MR) hawawezi kufunzwa chochote na kufundishika.


Kwa hiyo mtoto aliye na umri sawa wa akili na umri sawa wa kibinadamu atakuwa na kipimo cha akili 100 (yaani IQ=100). Kwa wale watoto wenye vipaji maalum, kipimo cha akili yao huwa zaidi ya 100 (IQ>100), na kwa wale wenye akili ya kawaida kipimo cha akili huwa chini ya 100 lakini hakishuki chini ya 85.


Upungufu wa Akili wa Kawaida (Borderline Mental Retardation)


Huwa na akili yakipimo cha IQ= 70-85%. Wanauelewa mdogo shuleni (Slow learners) lakini wanaishi maisha ya kawaida yaani bila kupata taabu yoyote katika maisha yao ya kila siku na wanaweza kuajiriwa.


Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation)


Huwa na akili ya kipimo cha IQ=50-70. Asilimia kubwa ya watu wenye upungufu wa akili huwa kwenye kundi hili (asilimia 85-95). Wanatambulika kama wanaoweza kuelimika. Wanaweza kujifunza kusoma, kuandika, na kufanya hesabu rahisi rahisi (simple arithmetic calculations). Hawa wanahitaji shule maalum ili waje kuweza kumudu majukumu yao ya maisha ya kila siku baada ya muda mrefu.Wanakuwa na upungufu mdogo katika uwezo wao wa kuhisi na utambuzi wa vitu (minimal sensorimotor deficits) na ni vigumu kutambua kwamba wanaupungufu wa akili mpaka baadae maishani. Katika ujana wao wanaweza kupata elimu hadi darasa la sita.Ukubwani, hupata uwezo wa kujihudumia wenyewe katika mahitaji yao ya kila siku lakini wanahitaji uangalizi, ushauri, kupewa mwongozo katika majukumu yao ya kifamilia na hasa wanapopata msongo wa mawazo au wakati wamepata matatizo ya kiuchumi.


Upungufu wa Akili wa Kati (Moderate Mental Retardation)


Huwa na akili yakipimo cha IQ=35-50. Asilimia 10 tu ya watu wote wenye upungufu wa akili ndio huwa kwenye kundi hili.Wanatambulika kama wasioweza kufundishika (untrainable) ingawa wengi wao wanaweza kuelimika. Utotoni mwao wanakuwa na mawasiliano mabaya ya kijamii, lakini wanaweza kujifunza kuzungumza, kutambua majina yao na baadhi ya maneno rahisi ambapo kutokana na haya ambayo nimeelezea hapo juu, kwa sasa wanatambulika kama kundi linaloweza kufundishika.Kawaida, huacha shule baada ya kufika darasa la pili (Standard 2). Wanaweza kufundishika katika kazi ambazo hazihitaji kutumia akili ama kazi za mikono.Msongo wa mawazo huathiri mafunzo yao hivyo ni muhimu kuboresha mazingira yao na kuwahudumia vizuri ili wasipate msongo wa mawazo.


Mara nyingi, uwezo wao wa kuelewa watu wanapozungumza ni mzuri kuliko uwezo wao wa kuzungumza na hii huwafanya kupata msongo wa mawazo. Uzungumzaji wao ni wa kawaida na hueleweka vizuri na wale wanaoishi nao au wale wanaofahamiana nao vizuri. Vitendo kama uvaaji nguo, kula, na kujiweka msafi, huchukua muda mrefu kwao kujifunza. Wanahitaji msaada katika matumizi ya hela na hata kuvuka barabara.


Upungufu wa Akili Mkubwa (Severe Mental Retardation)


Huwa na akili ya kipimo cha IQ=20-35 na huonekana kwa watu wenye upungufu wa akili kwa asilimia 5 tu. Hutambulika mapema kwa kutokuwa na uwezo wa kutambua vitu mbalimbali (Poor motor development). Watu hawa hawana uwezo wa kuzungumza na kuwasiliana au hupata uwezo huo baadae maishani. Huitaji shule maalum pamoja na wataalamu wa tiba ya sauti ili waweze kujifunza kuzungumza.Chini ya uangalizi, huweza kujifunza shughuli ndogondogo.


Upungufu wa Akili Uliopitiliza (Profound Mental Retardation)


Huwa na akili ya kipimo cha chini ya 20 yaani IQ<20. Asilimia 1-2 ya watu wenye upungufu wa akili ndio walio kwenye kundi hili. Mara nyingi wanakuwa na ugonjwa au matatizo ya sehemu ya mishipa ya fahamu ambayo husababisha upungufu wa akili.Dalili za kuwa na uwezo finyu wa kutambua na kuhisi mambo mbalimbali, kushindwa kuelimika, kujihudumia, kufanya kazi, kujitunza huonekana mapema sana. Huitaji msaada wa kijamii pamoja na kuhudumiwa katika maisha yao ya kila siku.


Aina za Upungufu wa Akili


Kuna aina mbili za upungufu wa akili ambazo ni;

  1. Syndromic mental retardation – Hii ni upungufu wa akili (intellectual deficits) unaoambatana na magonjwa mbalimbali pamoja na viashiria na dalili za kitabia (behavioral signs).
  2. Non syndromic mental retardation – Upungufu huu wa akili hausiani na magonjwa au ugonjwa wowote.
MENTAL%20RETARDATION%20PIC_(1).jpg

Pathofiziologia (Pathophysiology)


Upungufu wa akili ni mjumuiko wa matatizo katika mfumo wa fahamu (CNS functions) ambapo sehemu inayojulikana kama cortical structures (ambayo huusisha pamoja na sehemu zingine kama hippocampus na medial temporal cortex) ndio huathirika. Watu wengi wenye upungufu wa akili hawaonyeshi kuathirika katika mfumo wao wa fahamu. Ni aslimia 10-15 ya watu wote wenye upungufu wa akili ambao ndio wanaonyesha kuathirika katika mfumo wao wa fahamu.


Matatizo katika mfumo wa fahamu ambayo huonekana sana ni kichwa maji (hydrocephalus), neural tube defects, microcephaly na (disorders of migration- the lissencephalis na muunganiko wa mwatuko wa ubongo {agenesis of corpus carlosum} ambayo huonekana mara chache).


Watu wengi wenye upungufu wa akili aina ya mild mental retardation na wenye matatizo mengine ya ufahamu (other learning disorders), huwa hawana matatizo katika mfumo wao wa fahamu, madhara katika neva na dysmorphisms lakini wana uwezekano mkubwa wa kutoka katika familia zenye hali duni ya kiuchumi, familia yenye kipimo cha akili ndogo (low IQ), na elimu duni.


Nini husababisha upungufu wa akili?


Zipo sababu nyingi ambazo husababisha upungufu wa akili ambazo ni kama ifuatavyo;

  • Matatizo ya kurithi (genetic factors)
  • Antenatal factors
  • Postnatal factors
  • Matatizo ya kijamii na kitamaduni (socio-cultural factors)
  • Magonjwa ya akili (psychiatry disorders)
Thuluthi moja (1/3) ya watu wenye upungufu wa akili chanzo hasa hakijulikani.


Matatizo ya viashiria vya urithi (genetic factors)

  • Chromosal abnormalities kama down syndrome, fragile X syndrome (mgonjwa anakuwa na kichwa kikubwa, masikio makubwa kama ya popo, uso mrefu, korodani kubwa kupitiliza na nyayo zinakuwa bapa {flat feet},huwa na matatizo ya lugha na sauti, hii husababishwa na matatizo katika ncha ya mkono mrefu wa chromosome)
  • Metabolic disorders kama phenylketonuria, homocystinuri, galactosemia nk.
  • Magonjwa kwenye ubongo (Gross disease of the brain) kama cerebral dysgenesis, tuberose sclerosis, neurofibrosis nk.
  • Madhara ya kwenye ubongo (brain malformations) kama nueral tube defects, kichwa maji na microcephalus
Antenatal factors


Matatizo ambayo hutokea wakati mtoto bado hajazaliwa (yaani yanayompata mtoto wakati bado yupo tumboni mwa mama yake). Haya yanaweza kuwa;

  • Magonjwa kama ugonjwa wa kaswende (syphilis), TORCH
  • Sumu (intoxications) kama madini ya risasi (lead), madawa ya kulevya, unywaji pombe wakati wa ujauzito nk.
  • Physical damage – Tiba ya mionzi au vipimo vya mionzi, injury, ukosefu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto (hypoxia).
  • Matatizo ya kondo la uzazi (Placental dysfunctions) – Toxaemia, ukosefu wa virutubisho sahihi katika ukuaji wa kondo (Nutritional growth retardation).
  • Matatizo katika mfumo wa vichocheo mwilini (Endocrine disorders) – Hypothyroidism (ugonjwa wa tezi la koo), ugonjwa wa kisukari kwa mama mjazito, hypoparathyroidism.
Perinatal factors


Matatizo yanayotokea wakati mtoto anazaliwa (wakati wa kujifungua kwa mama mjazito)

  • Ukosefu wa hewa ya oksijeni (Birth asphyxia), cerebral palsy nk
  • Madhara ya mtoto kuzaliwa njiti (complications of prematurity) kama uvujaji damu ndani ya ubongo (intraventricular haemorrhage).
  • Hypoxic Ischemic encephalopathy
Post-natal factors


Matatizo yanayotokea baada ya mtoto kuzaliwa

  • Injury – Head injury (kuumia kichwa)
  • Sumu (Intoxication) kutokana na madini ya risasi, mercury nk.
  • Magonjwa kama ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), encephalitis (maambukizi kwenye ubongo)
Socio-cultural factors (Matatizo ya kijamii na kitamaduni)


Kutokuwa na uwezo wa kujumuika na jamii huchochewa na ukosefu wa elimu, kiwango duni cha uhamasishaji, tabia ya mtu, ucheshi wa mtu,utapia mlo, mimba za utotoni (kwani huleta umaskini, utapia mlo, afya duni, kuathirika kwa mama na hivyo kumuathiri mtoto), vocational opportunities pamoja na magonjwa ya akili na magonjwa mbalimbali. Kukosekana kwa vichocheo hivyo au kuwepo kwa magonjwa ya akili na baadhi ya magonjwa mbalimbali huweza kusababisha upungufu wa akili. Ikumbukwe ya kwamba akili ya mtoto huwa inakuwa kwa hiyo ni muhimu apewe fursa ya kuweza kukuza akili yake.


Magonjwa ya akili (Psychiatric disorders)

  • Pervasive developmental disorders (Autistic spectrum disorders)
Akili
 
Asante mzizi ila sijui kama sijakuelewa au maelezo yako ndiyo hayajajibu swali husika.
 
kuna kitu inaitwa cognitive therapy, ni tiba ya kisaikolojia sababu hizi mental illness mara nyingi zinakuwa triggered na psychological problems ukiachana na wale waajali. hapa mgonjwa hufanyiwa psychoanalysis kugundua kitu kinachomsumbua na ndipo njia ya utatuzi hutafutwa matokeo hutegemea adherence ya mgonjwa kwenye maelekezo na kama tatizo lililogunduliwa ni lenyewe, nahisi inakuwa effective zaidi kabla ugonjwa haujamuathiri sana mgonjwa kiasi ashindwe kujitambua. ni tiba yenye matokeo kwa watu waliochanganyikiwa sababu ya mapenzi, ugumu wa maisha, masomo na mambo kama hayo

Mkuu nimekuelewa vizuri kiasi kwamba 'am ready for the challenge from you just to test how much have been absorbed out of it.
Karibu uniulize nijipime.
 
Back
Top Bottom