Ugomvi na mke wangu kila nikipata pesa

Ugomvi na mke wangu kila nikipata pesa

Nilikuwa nae mwanamke wa hivyo tulidumu miaka 6, na ndio alikuwa mke wangu wa ujanani tuliachana tayari tukiwa na watoto wawili. Aisee ukiwa na hela kelele kinoma mpaka unawaza bora nisiwe na kitu kbs. Ilifika hatua hata uchakalikaji kwangu ukapungua nikawa nakaza tu pale kodi ya nyumba imekalibia kuisha.

Nikasema ngoja nikufungulie kigenge uwe unajitafutia tuone... Kumbe hapo ndio nikawa nimeharibu kbs yalizuka madharau acha kbs... Kuna kipindi nilikuwa na laki 6 ndani nimezidunduliza ili niangalie namna ninunue bati, pesa akawa anazitolea macho mara nunua gesi, mara ninunulie nguo mpya nikawa nakaza mwisho wa siku nimetoka mihangaikon usiku nakuta tv haiwaki kumbe wameivunja. Nikamuuliza akasingzia kijana wangu nikamwamusha kijana akasema ni mama kavuja hapo ndio likozuka bifu la kufa mtu

Kufupisha stry baadae nilichukua zile hela nikaenda kununua tv mpya na vitu vyake vyote alivyokuwa anapigia kelele kila muda nikabak sina hata sent nadhan ndio ikawa furaha yake mim kubaki sina kitu

Tuliachana 2021
 
Yaani imekuwa kila mara nikipata pesa mke wangu analeta kamzozo.. Mpaka imefika mahala nawaza au hapendi nipate pesa!

Nikipokea mshahara mara zote anasema nitoe pesa yote benki nilete mezani. Ofcourse anaweza akawa na hoja zake kuwa hata zikikaa benki huwa tunazitumia na zinaisha haibaki hata senti. Nikimwambia pesa hazitolewagi zote benki haelewi hata kidogo anakuwa mkali sana na anazira

Pia analalama sana kuwa mimi ni mbinafsi kwenye suala la pesa; kitu ambacho nikijitathimini naona kama ananionea tu, over 90% of my income inaishia kwenye matumizi ya familia, sinywi pombe wala sihongi. I am a family man with three sons

Nikimuuliza mke wangu mbona unakuwa mkali kuhusu suala la pesa anazira huku akiniambia kwa kejeli "Samahani nimekuingilia kwenye pesa zako".

Na mara nyingi sana huwa ananilalamikia kuwa nafanya maamuzi yanayohusu pesa mwenyewe kwasababu yeye hana mchango wowote wa kipesa anaounesha kwenye familia; mke wangu ni mama wa nyumbani by default analea watoto watatu.

Imefika mahala mpaka natamani tubadilishane majukumu. Nikae nyumbani yeye akatafute hizo pesa ambazo huwa natafuta ili aridhike na aone kuwa ana mchango kwenye hii familia.

NIFANYAJE WANA JF?
Wewe ni Jinsia gani kwanza. Tuanzie hapo.
 
Anatambua kwamba wewe ndiye "fazahausi"?Unamdekeza.
 
Hayo ndio maisha ya ndoa za kiafrika, Sasa hapo inabidi umcontrol wewe... Ndio uanaume Sasa.
 
2022 mwezi wa 12 nikaoa mwanamke mwingine tulimake kwa mwaka mmoja tu tukawa na kijumba chetu ampo nikiwaza kwa huyu mwenzangu nilieachana nae kwamba niweze kuhifadhi zaidi ya mil 5 ndan chumban na anaziona na bila kelele hapana aisee
 
Mfungulie biashara imkeep busy, na yeye anatamani kushika hela usimfanye tu awe golikipa.
 
Yaani imekuwa kila mara nikipata pesa mke wangu analeta kamzozo.. Mpaka imefika mahala nawaza au hapendi nipate pesa!

Nikipokea mshahara mara zote anasema nitoe pesa yote benki nilete mezani. Ofcourse anaweza akawa na hoja zake kuwa hata zikikaa benki huwa tunazitumia na zinaisha haibaki hata senti. Nikimwambia pesa hazitolewagi zote benki haelewi hata kidogo anakuwa mkali sana na anazira

Pia analalama sana kuwa mimi ni mbinafsi kwenye suala la pesa; kitu ambacho nikijitathimini naona kama ananionea tu, over 90% of my income inaishia kwenye matumizi ya familia, sinywi pombe wala sihongi. I am a family man with three sons

Nikimuuliza mke wangu mbona unakuwa mkali kuhusu suala la pesa anazira huku akiniambia kwa kejeli "Samahani nimekuingilia kwenye pesa zako".

Na mara nyingi sana huwa ananilalamikia kuwa nafanya maamuzi yanayohusu pesa mwenyewe kwasababu yeye hana mchango wowote wa kipesa anaounesha kwenye familia; mke wangu ni mama wa nyumbani by default analea watoto watatu.

Imefika mahala mpaka natamani tubadilishane majukumu. Nikae nyumbani yeye akatafute hizo pesa ambazo huwa natafuta ili aridhike na aone kuwa ana mchango kwenye hii familia.

NIFANYAJE WANA JF?
Asilimia 90 ya wanawake wana tamaa ya pesa na hata ukifa ila umeacha pesa anazozifahamu huwa halii sana.

Huyo mkeo hizo tabia we ndio umezilea tangia mwanzo Kwa kutaka kuendekeza mapenzi ya kizungu ndio maana leo anakupanda kichwani na wewe umekuwa legelege.

Vumilia tu hayo maisha maana kila familia wana utaratibu wa maisha waliojiwekea.

Mi Kwa familia yangu mi ndio nasimamia shoo ya familia Kwa 90% japo mke wangu ni mwajiriwa wa serikali.

Ada za watoto, chakula , mavazi ya familia pamoja na ukarabati wa nyumba sijawahi omba msaada wa mwanamke. Kwangu hakuna utaratibu wa kuulizana kipato changu ama kumdai mwanamke pesa yake. Japo Kuna wakati mzumguko wangu unayumba hivyo naweza kukopa kiasi fulani ambacho najua Kiko ndani ya uwezo wako na huwa namrudishia .
 
Unamkopa mke wako hela? Something might be wrong somewhere, japo inawezekana ni mtazamo wangu tu.

Kwangu mimi, pesa za mke wangu ni zangu pia. Nikizitaka nazitumia. Simwombi, namwambia anipe, na ananipa bila kinyongo.

Kuna raha mkiwa mnaaminiana mpaka kwenye masuala ya hela.
 
Kwa hiyo ulishamwonyesha mkewe salary slip yako.
Hilo wala si tatizo.

Mshahara wako unaweza ukawa , tuseme, sh 3,000,000/= kwa mwezi (take home).

Mwisho wa mwezi ufikapo, ukishapokea, unaupeleka wote 3,000,000/= nyumbani na kumpatia akutunzie.

Kesho yake Asubuhi unapotaka kwenda kazini, unamwambia akupatie sh 500,000/=, na inayobaki, unamwambia kiasi cha kutumia kwa matumizi ya nyumbani na kiasi kitakachobaki, aitunze mpaka utakapotoa maelekezo mengine.

Kuna shida gani ukifanya hivyo?
 
Kama ni bajeti mpange pesa ikiwa benki si lazima ulete mezani. Aseme anataka mfanye nini? Ulete pesa mezani kwa mpango gani?
 
Sikiliza

Toa Hela nusu ya mshahara panga name bajeti ya mwezi mzima halafu mpe hiyo nusu aongozane na watoto wake wote kununua mahitaji ya mwezi mzima!!

Wanawake wanapenda kununua nunua sana Ili waonekane na WA awake wenzao kwamba Wana nunua!!

Halafu uone uelekeo!

Kama unampa Hela kidogo kidogo ya chumvi atakua omba omba !nyingine ummpe kama ya ziada hivi in case of emergency!

Nyingne mwambie naweka akiba for future!!

Wanapenda kujazwa manoti wanunue nunue!!!

Jaribu!
Hata akimfanya ndiye mtunzaji wa hela yake ni sawa tu. Mwingine atajisikia vizuri sana. Unampatia hela yako yote, siyo atumie, bali aitunze tu. Siku ukihitaji unamwambia akupatie. Wengi hujisiia vizuri kupewa hiyo "heshima"
 
Back
Top Bottom