Wengi waliomba sana kupata jasiri muongozaji akapatikana amefyagia kwelikweli baadaye kapingwa, oooh siyo huyu tuliyepewa, aya ngoja twende soon tu hapa hapa we'll.Kila kilichokuwa kimewekwa kwenye msingi kitasukumiwa mbali na giza na vuru vuru kuanza kukita mizizi
Sent using Jamii Forums mobile app
Thubutu! Wao hawajatuuzia miwa, wametuuzia sukari. Na sisi tuwauzie kahawa iliyosindikwa!! Tukitaka hivyo hapo ndipo picha halisi itakapoonekana, atanuna! Hata Kenya tukitaka kuwauzia unga watanuna! tulipaswa kuwauzia unga wala si mahindi. Tusipoangalia tutakuwa koloni la kuzalisha mali ghafi kwa nchi jirani. Wananchi wetu waelimishwe na wawezeshwe!!Wawaruhusu na nyie muuze kahawa huko Uganda
Ova
Kumbe viwanda havijaimarika??? Kwa hiyo tusubirie mpaka viimarike???Tuimarishe viwanda ikiishakuwa ya kutosha sukari nchini ndio tutajuwa tukoshafika mtoni...
Nyuma yake yupo Dr.Mpango.Huyu mama ni mkurupukaji sana, sijui hana washauri au hao washauri ndo wanamuingiza chaka, mweeeeeh
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
JPM hakutaka Tz tuendelee kuuza mazao yasiyosindikwa, bali tuyaongeze thamani kwa kuyasindika ndio tuyauze. Lakini majirani zetu wanapenda tuwauzie mazak ghafi halafu wao wayasindike halafu watuuzie tenà sisi kwa bei juu!! Kahawa iliyosindikwa itoke Kenya na Uganda kuja Tanzania!! Ni mjinga tu anayeweza kuona jambo hili ni sawa!! Ukiuza mazao ghafi maana yake huna ndoto za kukuza viwanda!!Kaulize wakulima wa kahawa wa Kagera watakutajia
Huijui Kenya! Viwanda vingi Kenya ni vya mabeberu wa kigeni na mabeberu wazalendo wachache. Waliobaki ni manamba!!PRIVATE sector ya Tanzania inapenda zaidi uchuuzi kuliko Uzalishaji wa viwandani
Tatizo letu private sector yetu imejaa illiterates darasa la saba na wasiosoma kabisa ndio wanaoendesha private sector
Hata ukute mamilionea ni wachuuzi tu sio producers!!! au wazalishaji wa viwanda!!! Jirani zetu Kenya Private sector wasomi ndio wamejazana kuna viwanda balaa
Habari wadau!
Sasa kilio cha upungufu wa sukari kitapungua maana mama amefungua milango na kuamuru sukari iingie nchini.
Mubashara toka Kololo Uganda kupitia TBC 1 kwenye uapisho wa Rais Museveni .Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven leo katika hotuba yake amemshukuru Rais wa JMT mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kwa kumruhusu kuuza sukari nchini Tanzania.
Asante mama tuna imani na wewe endelea kufungua milango yote iliyofungwa ili kazi iendelee.
Mitano tena kwa mama
Hiki kibonzo hakina tija kwa Taifa. Kinapotosha!
Tuzalishe yetu ipambane ikiwezekana na sie tuwapelekee yetu.. acheni kuwa na fikra za kibinafsi.Hayahaya tuliyakataa, nchi haiwezi kuendelea kwa kuimport tu. Sasa pesa yetu ya madafu inaenda kuzorota zaidi.
Ni Bora Kuagiza Sukari Kutoka Uganda kwa Majirani zetu EA kuliko ilivyo sasa ambapo Sukari inayoingizwa kutoka nchi za Nje inatoka Brazil na Nchi nyingine za Asia.
Umewahi peleka unga Kenya ukazuiliwa au kahawa iliyosagwa ukazuia uganda.Tusijiduni Sana hivyo.Thubutu! Wao hawajatuuzia miwa, wametuuzia sukari. Na sisi tuwauzie kahawa iliyosindikwa!! Tukitaka hivyo hapo ndipo picha halisi itakapoonekana, atanuna! Hata Kenya tukitaka kuwauzia unga watanuna! tulipaswa kuwauzia unga wala si mahindi. Tusipoangalia tutakuwa koloni la kuzalisha mali ghafi kwa nchi jirani. Wananchi wetu waelimishwe na wawezeshwe!!